Kama CAG anaweza, kwanini TAKUKURU na DPP Washindwe?! Hawa waondolewe mara moja

Pongezi kwa mawazo mema na yenye nia ya kujenga.mawazo haya ndiyo yanajenga nchi nafurahi kusema your a great thinker.busara yako inatukuza pia vijana naamini kazi ulotupa wanajf tunastahili kuianza mara moja.dci,takukuru,courts,dpp na wananchi kila mmoja atimize wajibu wake pasipo kumtegea mwingine we can move kwa kweli.
 
TAKUKURU NA DPP wanashindwa sababu Rais anaweza kuamka asubuhi akawatimua au kuwastaafisha Ila kwa CAG ni tofauti.Akishateuliwa C AG hata Rais hana mamlaka ya kumchomoa kirahisi. Tafuta maelezo ya termination process ya CAG ujue siri

Hiyo tu inaweza kuwa moja ya sababu ya utedajii tofauti wa hivyo vyeo . Huyo Uttoh akiwa "Hosea" wa TAKUKURU hizo mbwembwe hawezi kuwa nazo.
 
Mleta mada umechanganya ndimu na machungwa. Kazi ya CAG ni kuorodhesha tu lapses za kihasibu. Kwamba utaratibu ulikuwa hivi hawa wamefanya hivi.kazi ya DPP ni completelly tofauti yeye lazima aandae kesi atafute ushahidi wa kutosha. Takukuru halikadhalika kumshitaki mtu nao lazima wajipange sana kwakuwa ukimtuhumu mtu kimakosa inashusha reputation ya mtu.
 
Wala sijachanganya, na ninfahamu ninachokiandika! Na wala sikatai hicho unachokisema! Nitakuja kujibu hoja yako kwa undani hapo baadae, ila tu kwanza tuangalie aya moja wapo kutoka kwenye Dibaji ya Ripoti ya CAG:
"Ni vyema kutambua kuwa wakati ofisi yangu inatoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni mbalimbali na udhaifu katika mifumo ya udhibiti wa ndani kwenye taasisi za Umma na hasa Serikali Kuu, lakini wajibu wa kuhakikisha kuwepo kwa mifumo thabiti ya udhibiti wa ndani ni jukumu la Maafisa Masuuli." Mwisho wa nukuu.
Hapo kwenye taarifa kuhusu huo ukiukwaji ndipo hatimae anakuja ama TAKUKURU au DCI. Endapo ukiukwaji huo utaonesha dalili za wizi, basi DCI anaingia. Na endapo patakuwa na dalili za rushwa, TAKUKURU anachukua nafasi! DCI akashaingia ndipo anatakiwa kutafuta ushahidi kuthibitisha kwamba ni wizi umefanyika. halikadhalika ni hivyo kwa TAKUKURU!

Na kwa kuonesha anachofanya CAG ni zaidi ya Ordinary Auditing ambao unafanyika hata kwenye taasisi binafsi, CAG anaeleza hivi kwenye Ripoti ya Kifanisi na Kichunguzi ambayo inawasilishwa kwa Rais: "Sheria hii imepanua mawanda ya ukaguzi kwa kunipa mamlaka kufanya kaguzi za ufanisi (utendaji), uchunguzi mazingira na ukaguzi maalumu mbali ya ukaguzi wakawaida wa taarifa za fedha."

Mkuu NasDaz naamini hawa kina Falesh na Hosea hawana Muda,wakati vuguvugu hili la mawaziri halijapoa turudi ktk halmashauri zote zilizofanya ufisadi wasimamishwe kazi na iundwe mahakama Maalum ya mafisadi so kila alietajwa na ripoti ya CAG akajibu mashtaka yake kwa ushahidi wa CAG bila kujali ni nani,hii itarudisha ndhamu ya matumizi ya Fedha za Umma.
 
TAKUKURU NA DPP wanashindwa sababu Rais anaweza kuamka asubuhi akawatimua au kuwastaafisha Ila kwa CAG ni tofauti.Akishateuliwa C AG hata Rais hana mamlaka ya kumchomoa kirahisi. Tafuta maelezo ya termination process ya CAG ujue siri

Hiyo tu inaweza kuwa moja ya sababu ya utedajii tofauti wa hivyo vyeo . Huyo Uttoh akiwa "Hosea" wa TAKUKURU hizo mbwembwe hawezi kuwa nazo.

Na ndio maana nikatoa wito kwa Wabunge na Wana-JF kwamba washinikizwe kuondolewa kwa Felesh Na Edward Hossea. Hata wasipoondoka wenyewe na hata Rais asipowawajibisha, tayari ujumbe kwa Rais utakuwa umefika kwamba hata wabunge wa chama chake anachokiongoza hawawataki Hossea na Felesh. Ujumbe mkuu hapo ni kwamba watu hao wapo kwa maslahi ya aliyewateua na sio kwa maslahi ya taifa. Tunahitaji watendaji walio tayari kusurubiwa kwa niaba ya taifa lao! Hatuhitaji watendaji walio tayari kulinda maslahi ya ajira zao kwa gharama za watanzania. Kama nilivyosema hapo awali, pamoja na kwamba CAG ana-privellege zinazomlinda dhidi ya kuwa-fired lakini bado ujasiri wake ndio msingi mkuu!! Hajali kama muda wake ukiisha ataongezewa ulaji au hapana! Hiyo shaka shaka tu ya mustakabali wake pindi atakapoondoka ofisni ulitosha kabisa kwa kiongozi asiye jasiri kufanya madudu!
 
Hizi taasisi zimeanzishwa kwa ajiri ya watu kula na sio kuisaidia Tanzania. Tusitegemee lolote kutoka kwa hawa waheshimiwa maana sijui kwanza wanazo sifa gani za kuhalalisha kukaa kwenye viti wanavyokalia. Lakini ukichunguza sana utagundua JK ndiye anayewalea. Kama hawafanyi kazi inavyostahili wanakaa ofisini ili iweje sasa?
 
Nashauri vyeo kama hivi kwenye katiba mpya viwe vinathibitishwa na bunge maana kumpa Rais kila kitu bila kuwa na jicho lingine linaloweza kusema anafaa au la haitoshi na mpaka sasa imeshaigharimu sana Tanzania maana watu wengine wamekuwa mzigo usiobebeka. Hawana msaada wowote zaidi ya kupiga hela za umma
 
Nakubaliana na wewe kuhusu hili. Kuna kila dalili ya kuonyesha kuwa viongozi wengi wanateuliwa kama fadhila kwa kiongozi mkuu. Pamoja na mleta mada kueleza vizuri, kuwa JK amejitahidi kuvijenga vyombo hivi viwili kiutendaji lakini amefanya kosa katika kuteua watendaji wake. Inaweza kwa kwa kutojua au kwa makusudi.

Nakumbuka kabla ya uchaguzi 2005, Hosea alikuwa chini ya Mwanyika wakati ikiwa PCB, kuna tuhuma zilitoka kuhusu ukwasi wa waziri mkuu Sumaye, yeye aliwaambiwa waandishi wa habari kuwa PCB inachunguza tuhuma hizo. Lakini kama nakumbuka sawasawa ilikuja kupingwa na Mwanyika. Hoja yangu hapa ni kuwa kama aliweza kuwa na ujasiri akiwa hajashika nafasi ya juu kabisa PCB, na isiyo na meno kama ya leo, inakuwaje sasa anaishia kuwa kibogoyo? Jibu rahisi, Hosea (as Feleshi) amechagua upande kwa kuusimamia maslahi yake, kwa bahati mbaya sana upande aliochagua sio wa wananchi wengi wanaoteseka na madudu yanayofanywa na maofisa wa serikali.

Ni kweli kabisa, tufike mahali tusisherehekee madhambi ya viongozi wa serikali ya CCM kama ni njia ya kusaidia kuiondoa madarakani 2015, kwa kufanya hivyo hata sisi tutakuja kuhukumiwa na watoto/wajukuu zetu. Tuchukue hatua.
 
Naungana na wewe mkuu 100%.Makala nzuri sana .Kwa kuongezea ni kwamba CAG alipewa meno zaidi na Bunge kama sijakosea sana ni mwaka jana.
TAKUKURU ni taasisi ambayo haiko Independent.Licha ya kutokufanya kazi Independently ni taasisi ambayo mfumo wake haupo wazi kwa maana ya watendaji wake wanavyopatikana na sifa zako sio kitaaluma tu bali hata uwadilifu wao kwenye jamii.Taasisi kama TAKUKURU ambayo inasimamia mali za wananchi kwa kupambana na rushwa sio taasisi inayotakiwa iwepo kama pambo.Taasisi hii imejaza watu wasio na uzalendo na imekuwa ni kama kichaka cha vigogo kuwapatia watoto/ndugu/marafiki ajira.Ndio maana kumekuwa na tuhuma dhidi ya hii taasisi kuwa inatumiwa na watu/watawala kuhalalisha rushwa.

Suluhu kwenye hili ni katiba mpya,mbali na kupunguuza madaraka ya raisi bali kuweka wazi taasisi kama hizi ziwajibike moja kwa moja kwa wananchi.Haiwezekani taasisi inayosimamia mali wananchi iwe mikononi/inawajibika kwa watuhumiwa.Hapo ufanisi ni zero,na ndio tunayoyaona hapa kwa TAKUKURU.

Tanzania bila mfumo mbovu wa utawala wa CCM inawezekana.
 
Nashauri vyeo kama hivi kwenye katiba mpya viwe vinathibitishwa na bunge maana kumpa Rais kila kitu bila kuwa na jicho lingine linaloweza kusema anafaa au la haitoshi na mpaka sasa imeshaigharimu sana Tanzania maana watu wengine wamekuwa mzigo usiobebeka. Hawana msaada wowote zaidi ya kupiga hela za umma

Ni kweli mkuu, ila nazani ndani ya nchi hii panahitajika kitu kingine zaidi ya kuthibitishwa na bunge! Leo hii, huyu Pinda ambae analalamikiwa amethibitishwa na Bunge lakini tayari ame-prove failure. Labda tusema kwamba zile nafasi nyeti ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja katika kupambana na ufisadi nchini, nafasi hizo ziwe zinalindwa kikatiba dhidi ya watendaji wake kutimuliwa kiholela.
 
Hivi ni kwanini watumishi wa umma wanaonekana kama hawana nguvu tena ya kutekeleza kazi za umma? Maana hili tatizo sio la ofisi hizo mbili tu. Ni karibu ofisi zote
 
Kwani nani ni boss wa Pinda na wale mawaziri nane wanaotuhumiwa wajiuzuru? Ukiangalia vizuri, haionyeshi nidhamu kwa waziri kwenda kumtuhumu waziri mwenzake kwa press conference. Hawana cabinet meetings? Hiyo nayo ni weakness ya nani? Ndo maana ili mambo yaende, sio kila kitu kiwe kwa Rais. Yes Rais ateue ila bunge litibitishe na nafasi zao ziwe zinalindwa kisheria na mwingiliano wa wana siasa.

Skorpion, ambayo ilikuwa ndo Takukuru ya South Africa ilisambaratishwa sababu ya kumuweka Zuma kitanzini. Bado that independence katika kupigana na rushwa ndiyo tunayo ihitaji hapa.
 
Hivi ni kwanini watumishi wa umma wanaonekana kama hawana nguvu tena ya kutekeleza kazi za umma? Maana hili tatizo sio la ofisi hizo mbili tu. Ni karibu ofisi zote

Sina hakika kama nimekuelewa...lakini nijitahidi kukujibu kama ambavyo nilivyokuelewa. Kimsingi, si kwamba hawana nguvu bali utashi wa kuzitumia nguvu na mamlaka waliyonayo. Utashi huu mara nyingi kama sio zote huwa unafifishwa na maslahi binafsi. Kwamba, wengi wao wanalazimika kutotumia mamlaka yako kwa kuhofia kuondolewa kwenye nafasi zao....huu ni ubinafsi; kwamba ni heri mamilioni ya Watanzania waangamie kuliko wao kukosa ugali wao wa kila siku! Endapo pangekuwa na ujasiri pamoja na utashi, basi watendaji wengi wangeweza kusukuma gurudumu hili hata kama nafasi zao ni za kuteuliwa na kuwa fired!! Hapa panahitajika watendaji wenye uzalendo wa kweli. Ndiyo, mtu kama Hossea na Feleshi ni uteuzi wa Rais na Rais bado ana mamlaka nao, lakini bado endapo wangekuwa majasiri, wazalendo na wasio wachoyo ingekuwa tayari wameshafanya makubwa ndani ya nchi hii hata kama outcome yake wao wasingekuwa tena madarakani. Tunahitaji watu mithili ya Bradley Bellick wa Prison Breaker!
 
Mimi tatizo naliona lipo katika mfumo tuliouiga.UPELELEZI AU UCHUKUNGUZI KAMA UKITAKA UNAFANYWA NA TAKUKURU.
Wao wajibu wao ni kufanya uchunguzi tu na kutoa taarifa kwa DPP. Ambaye anafanya mapitio ya taarifa kutoka TAKUKURU na kuitolea uambuzi ama kesi iende mahakamani au uchunguzi urudiwe au taarifa za uchunguzi hazitoshelezi kupeleka kesi mahakamani.Kwa lugha nyepesi DPP ni mshitaki,mlalamikaji na hakimu kwa pamoja.Hapa ndipo penye matatizo ya msingi.
Mimi nilikuwa napendekeza kuwa Takukuru baada ya uchunguzi wao wakijiridhisha kuwa wao ushahidi wenye nguvu basi wapeleke na kuendesha kesi wao wenyewe.
Nilitagulia kusema tumeiga mfumo wa walioendelea ambao sisi hatuuwezi.
 
Mleta mada umechanganya ndimu na machungwa. Kazi ya CAG ni kuorodhesha tu lapses za kihasibu. Kwamba utaratibu ulikuwa hivi hawa wamefanya hivi.kazi ya DPP ni completelly tofauti yeye lazima aandae kesi atafute ushahidi wa kutosha. Takukuru halikadhalika kumshitaki mtu nao lazima wajipange sana kwakuwa ukimtuhumu mtu kimakosa inashusha reputation ya mtu.

Mkalisheni jamvini mumfunde atakuwa barozi mzuri kwa waliomtuma, kesi ni ushahidi na uendeshwaji wake unatumia kodi ya maskini asiye na matumain ya kupata hata mlo mmoja kwa siku.
 
CAG wanatumia anafungwa na hitaji za kimataifa katika kufanya kazi kama ISA,ISSAI,AFROSAI,AFROSAI-E,IAS pamoja na hitaji la ndani kama NBAA,TAKUKURU NA DPP wanaongozwa matakwa ya watala katika kuamua la kufanya na kutofanya matokeo yake kama mfumo wa juu umeoza hauwezi kupata matokeo mazuri kwa sababu wamejikita katika kuridhisha watawala na siyo misingi ya taaluma
 
NasDas,

Tuko pamoja katika hili. Kama CAG anaweza kupata access ya files na documents ili kugundua ubadhirifu, Police, TAKURURU wanashindwaje?? Kwa kuongezea ninapendekeza haya:

a) DPP na TAKURURU ziwe taasisi za Kibunge badala ya serikali ambazo ziko chini ya wizara. Ingekuwa ni wajibu wa bunge kuiamuru taasisi moja au zote kufanya uchunguzi na kutoa taarifa za uchunguzi. Wakurugenzi wa vyombo hivo wawe vetted (kupitishwa) na Bunge.
b) Kuwe na mahakama ya makosa ya ubadhirifu (Fraud Marshal Court) mbali za mahakama za kiraia. Tuone ubadhirifu ni uhalifu dhidi ya taifa sawa na uhujumu uchumi na uhaini. Ni kwa elevation ya status hii tu ndio watu wanaweza kujifunza.
c) Kama tunasema kubaka, kuuza mihadarati na ujangiri vinafaa miaka 30, kwanini emblezzlement of public funds isiwe miaka 50 na mtu akishaonekana anakosa tunategemea adhabu hiyo na ufilisi wa mali zake zote?? Inaumiza kidogo Liyumba kufungwa 2 years kwa billions alizoiba na aliyekamatwa na gobore akiwa na swala mmoja eti miaka 30 jela!!
 
Mleta mada umechanganya ndimu na machungwa. Kazi ya CAG ni kuorodhesha tu lapses za kihasibu. Kwamba utaratibu ulikuwa hivi hawa wamefanya hivi.kazi ya DPP ni completelly tofauti yeye lazima aandae kesi atafute ushahidi wa kutosha. Takukuru halikadhalika kumshitaki mtu nao lazima wajipange sana kwakuwa ukimtuhumu mtu kimakosa inashusha reputation ya mtu.

You are the calibre of ppl we all think can help which actually cannot. There is a disconnect between what TAKURURU and DPP are doing on the one hand and what the CAG is doing on the other. Take the subject matter and connect with the body, then take your comments and connect with "what should have been done"!! The gaps are to be filled and this is what the poster is on!!! If money has been lost through malpractices that the CAG has unearthed do you thing the DPP has no evidence to take the culprits to the court of law???? TAKURURU works like a spy agency, how on earth did they miss all these malpractices while civil servants are getting rich overnight?? Okay they missed them, what about starting investigations now???

The reputation is not born with a person, it is earned!!! Usione tu kuwa wanapaswa kuwa nayo, wanapaswa kuitete ili wabaki nayo!!

You are one sorry dude, sorry to point this out. Expand on topic before reputation become first choice over many other important things. We are talking public funds in billions, not one hundred shillings. We are talking government failure, not one person.
 
Back
Top Bottom