Kama CAG anaweza, kwanini TAKUKURU na DPP Washindwe?! Hawa waondolewe mara moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama CAG anaweza, kwanini TAKUKURU na DPP Washindwe?! Hawa waondolewe mara moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NasDaz, Apr 21, 2012.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kwa vyovyote iwavyo, ufisadi ndani ya nchi hii hautaisha wala kupungua endapo Edward Hossea na TAKUKURU yake pamoja na Eliezer Felleshi kama DPP wataendelea kuwa dhaifu katika utendaji wao! Tukiacha siasa za bingwa ni nani ambazo kimsingi zinatufanya tusiangalie upande wa pili wa mafanikio ya utendaji wa uongozi uliopo, basi utaona kwamba Rais Kikwete alijitahidi sana kutengeneza mfumo wa kitaasisi unaolenga kuzuia na kupapambana na ufisadi nchini.

  Tukiangalia historia ya TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa), kabla ya JK ilifahamika kama TAKURU, yaani Taasisi ya Kuzui Rushwa. Ikaonekana kwamba kuzuia rushwa peke yake haisaidii, bali wanatakiwa pia kupambana nayo….na hapo ndipo ikabadilishwa toka Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) na kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Kiukweli, TAKUKURU wamepewa meno yote yanayostahili ili waweze kufanikisha malengo yake, lakini hata hivyo wameishia kupambana na vila na vitoa rushwa vidogodogo huku mapapa wa rushwa wakiachwa waendelee kuitafuna nchi. Badala yake, Edward Hossea amekuwa akipambana na rushwa kupitia vyombo vya habari pamoja na kwenye midaharo huku matokeo ya mapambano yake yakiwa hayaonekani! Wapo wanaoshawishika kuamini kwamba kiongozi wa nchi hampi uhuru Edward Hossea katika kutekeleza shughuli zake. Jambo hili haliingii akilini hata kidogo! Je, kwanini Edward Hossea azuiwe na Ludovick Utto aachwe kutenda shughuli zake kwa uhuru?! Amini amini nawaambia, ikiwa JK aliweza kumtosa Swahiba wake Mkuu Edward Lowassa, basi hawezi kuacha kumtosa yeyote ndani ya nchi hii; labda mwanafamilia wake!

  Tukirudi katika uwezeshwaji wa kitaasisi katika suala zima la kutokomeza rushwa nchini, Mkagauzi Mkuu wa Hesabu Serikali (CAG) nae akapewa meno zaidi. Katika kuhakikisha Ofisi ya CAG haiishii katika kutoa ripoti za mapungufu ya mahesabu peke yake; humo wakajumuishwa TAKUKURU pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchni, yaani DCI. Lengo hapa lilikuwa kwamba, baada ya ukaguzi kupitia CAG kufanyika na madudu kuonekana basi madudu hayo moja kwa moja yapelekwe ama TAKUKURU au kwa DCI au wote kwa pamoja kutegemeana na aina ya madudu yaliyoanishwa na CAG. Hii maana yake ni kwamba, endapo pataonekana dalili za kuwepo kwa wizi, basi moja kwa moja DCI ishughulikie suala hilo na kuwafikisha mahakamani wahusika. Na endapo pataonekana kuwepo kwa dalili za rushwa ndani ya ukaguzi huo, basi moja kwa moja iripotiwe kwa TAKUKURU! Kwa bahati mbaya sana, si DCI wala TAKUKURU ambao wameonekana kwenda pamoja na kasi hii ya CAG. Endapo TAKUKURU na DCI wangefanya kazi zao ipasavyo, hivi leo kungekuwa na kesi nyingi mahakamani au majalada mengi yangekuwa yamewafikishwa kwa DPP.
  Hata hivyo, DPP ni kansa nyingine na tena hatari zaidi ndani ya nchi hii! DPP amepewa nguvu kubwa sana kisheria kuhakikisha anaendesha shughuli zake pasipo na kuhofia! Hata hivyo, hii ni moja ya taasisi nyeti kabisa ndani ya nchi hii zenye kiongozi dhaifu asiyefaa kwa Alifu wala Be! Takribani miaka mitatu sasa, Edward Hossea amekuwa akiueleza umma kwamba wamepeleka majalada ya kesi kubwa sita kwa DPP. Hata hivyo, hakuna kesi hata moja mpaka sasa ambayo imepelekwa mahakamani kutoka ndani ya hizo kesi hizo sita KUBWA!

  Mapungufu ya Rais Jakaya Kikwete!
  Kwa bahati mbaya sana, pamoja na nia yake inayoonekana katika kuziwezesha taasisi tajwa hapo juu bado ana udhaifu mkubwa mmoja! JK ni aina ya mzazi anayetoa kila kitu kwa mtoto wake. Ni aina ya wazazi ambao watanunua sare safi za shule, vitabu, madaftari na kila kitu kinachohusiana na masomo. Si hivyo, atatoa hadi ni pesa ya kutosha kabisa ya matumizi (pocket money)! Akishafika hapa, anaamini kwamba ameshamaliza kwa vile mtoto wake ni mtu mzima anayefahamu nini anatakiwa kufanya! Baada ya hapo hajishughulishi kuangalia endapo mtoto anaingia darasani au hapana; na kama anaingia nini maendeleo yake darasani! Huu ni ubovu mkubwa wa Rais wetu ambae ile tu kujenga taaisisi zenye nguvu anazani tayari amemaliza kazi!

  USHAURI KWA JK!
  KAMA JK alizijenga taasisi hizo kwa nia ya dhati ya kupambana na ufisadi nchini basi wakati umefika wa kuwawajibisha DPP pamoja na Mkurugenzi wa TAKUKURU. Si hivyo tu, hata DCI nae ame-prove failure! Hii ndio njia pekee ya kusafisha takataka za ufisadi nchini. Edward Hossea na Feleshi hawastahili kubaki ofisni mwao hata kwa siku moja ya ziada. Hawa wanapaswa kuondolewa mara moja bila kusitasita. Wale watakaongia, waanze mara moja na ripoti iliyotolewa karibuni na CAG pamoja na Kamati za Bunge. Pale panapoonekana harufu ya rushwa, basi bosi mpya wa TAKUKURU aanze nao…na pale palipo na dalili za wizi; DCI afanye kazi yake mara moja! Wakati umefika kwa hawa watu kupewa time frame/schedule of activitie!

  USHAURI KWA WABUNGE:
  KWA vile imedhihirika wazi kwamba wakiamua kuacha ushabiki wa kichama wabunge wanaweza kuleta mabadiliko, basi waendelee na uzi ule ule kwa taasisi zingine. Waweke maslahi ya chama pembeni na kuangalia maslahi ya taifa! Kelele zilizopigwa bungeni dhidi ya Mkurugenzi wa TBS, tuzisikie zikipigwa dhidi ya Edward Hosea na DPP! Hawa watu ni kansa sugu ambayo katu haitaweza kupona kwa tiba ya mionzi! Hii ni kansa inayostahili kakata kiungo kizima kabla haijsambaa mwilini na kusababisha kifo chetu! Narudia, Edward Hossea na DPP hawafai….wabunge unganeni kuhakikisha kansa hizi zinaondolewa ikiwa Rais atashindwa kufanya hivyo. Ikibidi, onyesheni nia ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais ikiwa atashindwa kuwaondoa watu hao! Hata kama kura hiyo haitafanikiwa kutokana na sababu zilizo wazi, basi angalau mtakuwa mmeonesha hisia zenu kwamba hampo pamoja na rais kwa uwepo wa kansa hizi mbili nchini!

  USHAURI KWA MFUMO WA KIMAHAKAMA.
  Nchi hii kesi zipo nyingi kwelikweli na nyingine wala hazina dalili kwamba zitakuja kwisha! Matokeo yake, kesi zenye maslahi kwa taifa bado zimeendelea lurundikana mahakamani na hivyo kuwafanya watu wasitishike sana kiasi cha kuogopa kuacha ufisadi. Endapo kesi hizi zingekuwa zinatolewa maamuzi mapema wakati bado zipo hot, huenda baadhi ya watendaji wangeogopa! Ni kweli, zipo sababu zilizo wazi na za msingi zinazotokana na uchelewashwaji huu! Hata hivyo, ni lazima idara ya mahakama ijipange kuhakikisha kesi za ufisadi zinamalizwa mapema. Ikiwa ni vigumu kuanzisha mahakama maalumu za kushughulikia ufisadi basi tuwe na NIGHT COURTS ambazo zitashughulika na kesi hizi! Hii maana yake ni kwamba, hatutahitaji majengo mapya ya mahakama wala kuajiri mahakimu wapya! Hakuna sababu za mahakamani zetu kufunga ofisi saa tisa wakati bado kuna maelfu kwa maelfu ya kesi hazijafanyiwa kazi. Lazima shughuli za mahakama hivi sasa ziendeshwe kwa shift……mchana na usiku…..saa mbili hadi saa tisa na saa kumi hadi saa nne usiku! Hii itasaidia sana kupunguza mrundikano wa kesi!

  USHAURI KWA JF MEMBERS.
  TUACHE ushabiki wa kisiasa pembeni na kuangalia maslahi ya taifa kwanza! Tutumie jamvi hili kupiga kelele zisizo na mwisho kuhakikisha Edward Hossea na DPP wanaondoka! Zimwagwe hapa threads za mara kwa mara kuwachana live watu hawa! Tuache kuangalia upande wa viongozi wa kisiasa peke yake kwavile huko ndiko kutakosaidia kuvijenga vyama vyetu bali tuangalie na upande wa pili wa shilingi! Tuachane na ujuha wa kutamani serikali iharibu na kuvurunda zaidi ili iwe tiketi ya mafanikio ya kisiasa kwa upinzani!! Tunaweza kutamani hivyo na bado tukakuta CCM inarudi tena madarakani hapo 2015!

  MAKALA hii ni ndefu, lakini pamoja na mambo mengine imelenga kupunguza idadi ya wachangiaji mamluki ambao wengi wao ni wavivu wa kusoma!
  NAWAKILISHA!
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Mkuu NazDaz, asante tumekusikia umetufikia!. Makala hii inazo kila sifa za kuingia printing, naomba isiishie hapa!.
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu muhimu sana naona hujakizungumza, CAG ana kinga kikatiba, rais akimteua hawezi kumng'oa kirahisi. Hii ni "added advantage" kwake, either way, inahitaji na ujasiri pia. Unaweza using'olewe cheo chako, ukang'olewa uhai.
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  PCCB na DPP ni ufisadi.
   
 5. i

  isoko Senior Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu umesomeka
   
 6. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kama ulivyosema, hapa kikubwa ni ujasiri kuliko hiyo kinga! Hakuna watendaji ambao ni ngumu kuwango'oa kama majaji lakini tumeshuhudia mara kwa mara wakishindwa kutumia hiyo previllege na kuishia kufanya madudu tu!
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  makala ni nzuri, nashauri uipeleke kwenye magazeti ya kila siku au hata ya wiki ili isomwe na watanzania walio wengi.
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mawazo makubwa haya mkuu.
  Hapo kwenye mahakama maalum naomba kuunga mkono kwa utashi wangu wote!
  Pia suala la TAKUKURU, turudi kwa wabunge wetu ambao wameonyesha kuwa pamoja na sisi (japo kidogo) waitake serikali irudishe sheria iliyounda Taasisi ili wairekebishe, waitoe chini ya ofisi ya Rais maana huu mjadala haujafungwaga toka kipindi kile.
  Kwa kurejea taarifa ile ya WIKILEAKS nadhani Hosea ni aina watu "super mnafiki" kwamba uwezo wa kufanya kazi anao ila alipokutana na kigingi cha Ikulu basi kaamua kucheza na steps za Music!
  Pale kwa DPP ndio hamna kitu kabisa.
  Kweli JF tunahitaji kupigia kelele zaidi masuala haya kwani njia ya kuelekea kwenye kufumua mfumo fisadi uliojikitia mizizi kuanzi serikali kuu hadi kwenye mishipa ya damu ya watanzania na sasa inajenga utamaduni katika kumuelezea mtanzania.

  Nasdaz kama unaweza kuitafuta thread flan ya Sokoine inaweza kutupa a case study hapa, jinsi alivyodeal na wahujumu uchumi, itafute hyo thread mkuu ili kupanua mjadala, ningekusaidia ila natumia simu mida hii.
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa mchango wako ambao ni very contructive. Wacha niitafute hiyo thread ya Sokoine kwani sikupata kuiona b4
   
 10. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,064
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante sana kwa makala nzuri mno kwa mustakabali wa taifa letu. Labda mimi niongeze kidogo hapo kwenye red.

  Ni kweli tumekuwa (JF na waTz wengi) tukichukulia mambo kishabiki badala ya uhalisia wake na hii kwa muda mrefu sana imewapa serikali na CCM kiburi cha kuendelea kufanya mambo jinsi wapendavyo kwani wanajua wananchi wenyewe tumegawanyika hata kwa yale mambo msingi kwa taifa.

  Wananchi wa kawaida mara nyingi hawana tatizo, lakini USISHANGAE ama hapa JF, kwenye vyombo vya habari (baadhi ya magazeti na viredio uchwara), na taasisi za kidini wakalichukulia hili jambo kwa mtazamo tofauti wanavyoona wao.

  Usishangae baadhi ya watu wakaanza kuwatazama waliojiuzulu na wengine wanaotajwa kwa ufisadi kwa matazamo wa imani zao na baadaye ama kwa uwazi au vinginevyo hisia na "maamuzi" yao yakawa kwa mtazamo wa imani au urafiki wao na wahusika. Hili ndilo tatizo letu kuu.

  Hata kinachoitwa "harufu ya udini", "ukabila", n.k. vimeingizwa kwenye system kwa makusudi kwa lengo hilo hilo la kuwagawa wananchi kwa faida ya watawala hususan CCM na wakati huo huo kwa hasara ya taifa(wananchi) - rushwa, ubadhirifu, wizi, ukosefu wa haki kwa wanyonge, n.k.

  Otherwise, big up.
   
 11. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni ukweli usiopingika kuwa JF ndiyo site inayosomwa sana Tzna walio nje ya Tz.. Ina VICHWA, Ni Taasisi, ni zaidi ya Bunge, ina jua kuchambua nani mamluki na nani mpambanaji.. hata utumie aka bandia utajulikana tu... Big Up mkuu, Umesomeka vilivyo, ila kule Kijijini hakuna Ngeleja hata Kompyuta, watanufaika vipi na mautamu haya?

  Pamoja tutaipigania Nchi yetu.. CCM itapita CDM itapita Tanzania itabaki milele..Tuijenge Taz kwa vizazi vijavyo..
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  umetumwa kuja kumtetea kikwete?
  Wunaogopa kura ikibadilishwa na kuwa ya raisi badala ya waziri mkuu?
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Uliyonena mkuu ni sahihi kabisa....! Jana usiku niliona thread moja hapa ambayo ilikuwa na mwelekeo kama huo kama huo! Ilinikera sana thread ile (kutokana na heading) kabla hata sijaifungua....! Hata pale nilipo-settle ili nione nini kimeandikwa, sikuweza kuiona tena ile thread. Sina hakika endapo Mods waliitoa au hapana! Lakini kama waliitoa, basi walifanya uamuzi wa busara sana!
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  101%, well said mkuu....umesahau kusema kwamba hata jeshi linaweza kuingia madarakani lakini tanzania itabaki milele hata kama itabadilishwa jina kama ilivyo kwa ZAIRE>>>>DRC!
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Nilipata definition moja ya population diversity kutokana na thread ambayo ililetwa na Mwanakijiji akitaka kufahamu tafsiri sahii ya population diversity! Ni lazima watu kama wewe wawepo ili population diversity ienedelee ku-exist!
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani mumesahau uyu alikuwa implicated kwenye scandal ya akina Luhanjo akaponea chupu chupu
  Sasa akaamua awe serious ndo akatoa kitu icho apo ili mjue akiamua anaweza
   
 17. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kama hiyo ndo dawa, basi sindano ile ile itumike kwa wengine.....kuna mengi ya kumsurubu Dr. Hossea au DPP Feleshi kiasi cha kuwarudisha kwenye mstari!
   
 18. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  MKUU Pasco,
  Umesomeka na ushauri wako ni muafaka.
   
 19. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  na ndio maana nao wanapaswa kuondoka mara moja au kuondolewa!
   
 20. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  unaondoa PCCB na DPP au watendaji wakuu wao?
   
Loading...