Kama CAG anapuuzwa, ukaguzi ni wa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama CAG anapuuzwa, ukaguzi ni wa nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jun 17, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  YAMEKUWEPO madai kwamba, serikali hata kama haitaki kusikiliza kelele za wanasiasa, hususan wa kambi ya upinzani na wachambuzi mbalimbali wanaohimiza dhana ya uwajibikaji serikalini, basi ilipaswa kufanyia kazi kwa ukaribu na umakini mkubwa chombo chake yenyewe, yaani ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Kama serikali ingejikita katika kuhakikisha taarifa za CAG zinafayiwa kazi, pesa nyingi za umma zingekuwa zinaokolewa na kuelekezwa kwenye maeneo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
   
 2. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu

  Unaongea vyema, Lakini naomba ukumbuke kwamba, hata kwenye makampuni binafsi,
  ushauri wa Mauditor wa ndani/nje hueshemiwa katika makampuni ambayo uongozi wa
  juu kabisa wa Kampuni unaelewa umuhimu wa hicho kitengo.

  Serikali hii tuliyonayo sasa imejaa mambumbu wa maswala ya utawala, ni wasanii
  tupu waliopata madaraka kutokana na mbinu za rushwa, fitina na ushirikina.

  Serikali hii iko tayari kuwasikiliza waganga wa kienyeji kuliko wataalamu,
  katika tasinia yoyote.
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dhana ni kwamba pesa nyingi za umma zimekuwa zikipotea na takwimu zilizotolewa na kambi ya upinzani Jumatano wiki hii Bungeni zikikariri ripoti ya CAG, takriban asilimia 25 ya bajeti yote ya serikali imekuwa ikipotelea mifukoni kama si matumboni mwa wajanja wachache. Je, katika hali kama hiyo tunatarajia maendeleo gani?  Katika Bunge linaloendelea, Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, alisema hivi karibuni kwamba CAG alishapewa meno na Rais Jakaya Kikwete kwamba anaweza kumkamata ofisa wa serikali ambaye mamlaka anayoiongoza inaonesha kuiba ama kutumia vibaya pesa za umma. Je, hiyo kweli ni kazi ya CAG? Atapata wapi muda wa kushughulikia masuala yake ya msingi, yaani ukaguzi kama ataanza tena kufukuzana na kesi mahakamani? Zipo habari kwamba baadhi ya taarifa zinazoonesha ubadhirifu
   
 4. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu, hali ni mbaya kuliko inavyoweza kufikirika. Uchambuzi uliofanywa na NGO moja inaitwa Sikika unaonesha kwamba Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali amekuwa anafanya kazi nzuri sana ya kuonesha jinsi fedha za umma zinavyotumiwa, na amekuwa akitoa mapendekezo kadha wa kadha ili kuboresha mapungufu yaliyopo ila hakuna kinachofanywa.

  Kinachoumiza zaidi ni pale watanzania wanapoelezwa kwamba ukaguzi huu unafanywa kwa kutumia fedha za walipa kodi na bado matokea ya ukaguzi hayafanyiwi kazi. Ningekuwa na uwezo ningeifunga ofisi hii maana ndio nakubali inafanya kazi nzuri ila kazi yake haiisaidia serikali kuboresha matumizi yake ya fedha. Kwa mfano Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ripoti za mkaguzi za kuanzia mwaka 1999 hadi 2010 zinaonesha kiasi cha zaidi ya bilioni 200 zinauliziwa na mkaguzi maana hakuna justification ya matumizi yake! We have a lot to do with our country men!
   
 5. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red ungelikuwa umetumia uwezo wako vibaya. Natumai kuwa na uwezo una-refer mkuu wa kaya; kama ndivyo ukiwa na huo uwezo unatakiwa kuziamsha au kuwafukuza kazi wakuu wa hizi idara za TAKUKURU na DPP. CAG kesha piga yowe, vyombo vinavyohusika na kukamata vimepiga usingizi wa pono; wewe unatamani tena kumnyamizisha mpiga yowe!
   
Loading...