Kama CAG amewaonea Clouds Media atashindwaje kuzionea taasisi nyingine kama ATCL n.k?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,821
141,732
Jana alisikika meneja wa fedha wa Clouds media akidai kuwa taasisi yake iliwasilisha kwa CAG risiti zote za kielectronic kama alivyoagiza na siyo kweli kwamba kuna utata katika malipo waliyolipwa na wizara ya maliasili na utalii.

Ndiposa natafakari kama meneja huyo wa fedha bwana Masoud anasema ukweli basi kuna tatizo kubwa kwenye hiyo taarifa ya CAG ihusuyo ukaguzi.

Ni vema CAG mheshimiwa Kichere akalitolea ufafanuzi hili jambo.

Ukinizingua Nitakuzingua!
 
Kwan CAG ameenda kukagua Clouds au Wizara ya maliasili .?? ... Anayetakiwa kuonyesha list ni Yule aliyelipa au aliyelipwa? Nafkri CAG hahusiki kabisa na Clouds ,yeye anahusika na wizara ya Malia asili...kama clouds walitos rist haina shida , maliasili mbna hawakumpa hzo rist
 
Dogo, kila siku unani aibisha JamiiForums, kwa kuwa na kichwa kigumu kuelewa.

CAG alisema malipo yalifanyika ila bila "MKATABA (Makubaliano Ya Kisheria)". Hajasema kwamba hakuoneshwa receipts za malipo, alioneshwa hizo receipts, ila malipo yalifanyika bila makubaliano yoyote baina ya Wizara Ya Maliasili na hivo vyombo husika.

Kivipi, hela walizolipwa "Clouds TV/Wasafi TV/TBC" zililipwa "KIENYEJI". Makubaliano yalifanyika kienyeji either kwa kutumia mdomo au sms au facebook au instagram au twitter (Ulingo anaopenda Waziri husika kuutumia) ila sio kisheria, hazikuwa na maandishi ya mkataba kisheria kuthibitisha kwamba kiasi hicho cha pesa kimelipwa kwa mantiki gani na kwa kazi gani na kwa muda gani hio kazi ifanyike. Baada ya mambo kuharibika ndio wakakimbilia kusema kwa mdomo tu zililipwa kwaajili ya matangazo.

Wizara kufanya kazi yenye thamani ya Mamilioni na taasisi binafsi, bila mkataba. Imekaaje hio!!! 10% au 50% ya ulaji kwa Waziri inakosekana hapo!!!

SWALI KWAKO:

1) Unaweza ukampa mtu milioni 800 akufanyie kazi fulani bila maandishi??? Umpe hela kiasi hicho halafu umwambie kwa mdomo nifanyie kazi fulani??? Na asipofanya hio kazi uliomwambia afanye utamfanya nini au utampeleka mahakama gani kudai hela yako???

2) Mfanyakazi wako akitoa kiasi hicho cha fedha na kumpa mtu afanye kazi fulani kwa niaba ya ofisi kwa kutumia mdomo, bila maandishi yoyote kuthibitisha malipo yamefanyika kwa sababu zipi. Utafanya nini kama sio kumfunga jela yeye na familia yake???

3) Wizara inayo ongozwa na mtu anaejiita msomi kufanya kazi (Yenye thamani ya 800 Millioni) na taasisi binafsi bila mkataba. Sio ujuha wa kiwango cha lami huo???

4) Je, kama Waziri alitumia kivuli cha malipo hayo yasio na mkataba kama njia ya kufanya ufisadi wa hela, akishirikiana na vyombo hivo???

SWALA la ATCL na TTCL kuendeshwa kwa hasara ya mabillioni usiseme CAG anayaonea hayo mashirika, achana nalo kabisa, huliwezi na hautakuwa na hoja ya kuzijibu.

# Dogo acha mihemko, mwendazake ndio ameshakwenda, alikua fisadi pamoja na watendaji wake, acheni kumsifia marehemu asie na msaada kwenu tena. Pamoja tujenge taifa lenye matumaini sio kutetea mafisadi wa CCM.

Nawasalimia kwa jina la CAG - (Mnatakiwa kuitikia ""Tumeibiwa sana wanyonge, ila bado hatujakoma"").
 
Jana alisikika meneja wa fedha wa Clouds media akidai kuwa taasisi yake iliwasilisha kwa CAG risiti zote za kielectronic kama alivyoagiza na siyo kweli kwamba kuna utata katika malipo waliyolipwa na wizara ya maliasili na utalii.

Ndiposa natafakari kama meneja huyo wa fedha bwana Masoud anasema ukweli basi kuna tatizo kubwa kwenye hiyo taarifa ya CAG ihusuyo ukaguzi.

Ni vema CAG mheshimiwa Kicheere akalitolea ufafanuzi hili jambo.

Ukinizingua Nitakuzingua!
Siyo kazi ya Mkaguzi kutafuta risit zilizopote.Kama hakuona risit za kieletronic mpaka anatoa report yake ni juu yao walikaguliwa.Kama walipoteza ilikuwa ni jukumu la wizara kufuatilia na kumuonyesha mkaguzi.
 
Jana alisikika meneja wa fedha wa Clouds media akidai kuwa taasisi yake iliwasilisha kwa CAG risiti zote za kielectronic kama alivyoagiza na siyo kweli kwamba kuna utata katika malipo waliyolipwa na wizara ya maliasili na utalii.

Ndiposa natafakari kama meneja huyo wa fedha bwana Masoud anasema ukweli basi kuna tatizo kubwa kwenye hiyo taarifa ya CAG ihusuyo ukaguzi.

Ni vema CAG mheshimiwa Kicheere akalitolea ufafanuzi hili jambo.

Ukinizingua Nitakuzingua!
We pimbi lini CAG akakagua private company?
 
Hivi kwa nini hii report ya CAG imekuwa na changamoto mwaka huu? Maana CAG amekuwa akitoa reports kila mwaka na wala hatuoni hii interest kwenye hizo reports. Shida ni nini? Au ni kwa vile umeibuliwa ufisadi dhidi ya serikali iliyojinadhifu kwa usafi na kupigania wanyonge? Yaani naona kuna watu wako radhi kuhalalisha na kufumbia macho rushwa na ubadhirifu mwingine kwa vile tuu umemuhusisha mwendazake. Au ni kwa vile tumepata fursa ya kuyasikia haya?

Sasa sijui hawa watu watatoa wapi moral courage kukemea maovu huko mbeleni! Maana wanaamini kwenye selective justice!

Maybe wote tunaona haya mambo ni ya ajabu kwa sababu JPM hakuamini katika uhuru wa kupata habari. Ndo maana wengi hatuamini. Tuko radhi hata kumtosa CAG kwamba ana agenda ya siri dhidi ya mwendazake.

Siasa za Tz nimezivulia kofia!
 
Kwa mara ya kwanza nasikia CAG anakagua Private Companies, maajabu ya dunia haya🤣🤣🤣🤣
 
Dogo, kila siku unani aibisha JamiiForums, kwa kuwa na kichwa kigumu kuelewa.

CAG alisema malipo yalifanyika ila bila "MKATABA (Makubaliano Ya Kisheria)". Hajasema kwamba hakuoneshwa receipt za malipo, alioneshwa hizo receipt, ila malipo yalifanyika bila makubaliano yoyote baina ya Wizara Ya Maliasili na hivo vyombo husika.

Kivipi, hela walizolipwa "Clouds TV/Wasafi TV/TBC" zililipwa "KIENYEJI". Makubaliano yalifanyika kienyeji either kwa kutumia mdomo au sms au facebook au instagram ila sio kisheria, hazikuwa na maandishi ya mkataba kisheria kuthibitisha kwamba zimelipwa pesa kwa mantiki gani na kwa kazi gani.

Kisheria, kama hakuna makubaliano

SWALI KWAKO:

1) Unaweza ukampa mtu milioni 800 akufanyie kazi fulani bila maandishi??? Umpe hela kiasi hicho halafu umwambie nifanyie kazi fulani???

2) Mfanyakazi wako akitoa kiasi hicho cha fedha na kumpa mtu afanye kazi fulani kwa niaba ya ofisi kwa kutumia mdomo, bila maandishi yoyote kuthibitisha malipo yamefanyika kwa sababu zipi. Utafanya nini???
Masoud amesema malipo yaliyofanyika ni halali kwa mujibu wa nyaraka na sheria.

Aliyelipwa amekubali kuwa ni kweli amelipwa na risiti za kielektroniki alitoa

Na kama CAG nguvu yake inaishia kwenye kukagua upande mmoja tu bila kujiridhisha upande wa pili basi anatumia mbinu za kizamani sana.
 
Jana alisikika meneja wa fedha wa Clouds media akidai kuwa taasisi yake iliwasilisha kwa CAG risiti zote za kielectronic kama alivyoagiza na siyo kweli kwamba kuna utata katika malipo waliyolipwa na wizara ya maliasili na utalii.

Ndiposa natafakari kama meneja huyo wa fedha bwana Masoud anasema ukweli basi kuna tatizo kubwa kwenye hiyo taarifa ya CAG ihusuyo ukaguzi.

Ni vema CAG mheshimiwa Kichere akalitolea ufafanuzi hili jambo.

Ukinizingua Nitakuzingua!
kusema tu haitoshi. watu wanataka evidence.
blah blah blah hata ww unaweza ukatunga zako
 
Masoud amesema malipo yaliyofanyika ni halali kwa mujibu wa nyaraka na sheria.

Aliyelipwa amekubali kuwa ni kweli amelipwa na risiti za kielektroniki alitoa

Na kama CAG nguvu yake inaishia kwenye kukagua upande mmoja tu bila kujiridhisha upande wa pili basi anatumia mbinu za kizamani sana.
sheria zilizotungwa si yeye. yeye hawajibiki na private institutions.
kama walifanya payment kwa goverment institutions, upande wa gov ndio wa ku confirm kwa mba kweli payment imefanyika.
not otherwise.
na wasiliete maneno kwenye hili.. watu wanatala evidence
 
Anayepaswa kuonesha risiti ni wizara ya maliasili na utalii sio clouds.
CAG anakagua Wizara na si Clouds,labda huyo angesema tuliwapa Wizara risiti zote halali.
 
Back
Top Bottom