Kama bunge likishindwa njia mbadala ni hii hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama bunge likishindwa njia mbadala ni hii hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SJUMAA26, Apr 20, 2012.

 1. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuendelea kuwatetea Watz kwa maneno matupu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa!. Kwa Watz hata upige makelele kama mtu aliyefiwa hakuna wa kukuelewa na mwisho ukipoteza Ubunge au wadhifa wako hakuna wa kukutetea wala kukumbuka! Hebu fikiria, wako wapi akina Sokoine, Kawawa, Abdul Jumbe, n.k?

  Ama walikufa vifo vya aibu, au wako hai ila ni kama wafu, hata hakuna anayekumbuka Memorial Days zao! Ndio maana wajanja walipogundua Chama si cha Mapinduzi tena bali ni cha kuchukua chako mapema wakazika Azimio la Arusha na, taratibu lakini kwa uhakika, wakakigeuza chama chao kuwa cha Majambazi, Mafisadi na Matapeli!

  Hata hawa wanaopiga makelele ni either wako nje ya system au hawako kwenye mtandao na ndio maana njaa zinapowapiga wanaanza kupiga kelele! Madaraka matamu jamani, hata hao wenye makelele wakipewa nchi utawaona tu, wao na Magamba itakuwa like father like son! Ukitaka ku-test hii Hypothesis, waambie wote wenye makelele nao waachie nyadhifa zote walizo nazo kama ishara ya kupinga mfumo uliopo...Weee, nani utampata??

  Hivi hamkumbuki suala la Posho lilivyokuwa? Je, ni kweli hao wapiga kelele wote hawazichukui hadi leo? Dr. Slaa wa watu alipiga makelele kuhusu UFISADI hadi akataja orodha ya vinara lakini mambo yalibaki vile vile, naona huyu Mzee wa watu atakuja kufa pasipo kuona Watz wakistuka, na badala yake nchi yao bado wanaendelea kuwakabidhi manyang'au wale wale waliotajwa! Tungekuwa serious, kwanza tungewaadhibu kwa kutowarudisha madarakani, lakini hata kama wangepita kwa wizi na ghiliba zao, basi serikali yao tungeikataa kwa migomo, maandamano na fujo, na ikibidi hata vita!

  Tatizo Watz wengi wanadhani makelele yao tu ndio yatawafanya Magamba wang'oke, thubutu...muulizeni Nape ameshawang'oa wangapi licha ya makelele yake nchi nzima hadi akaamua ku-cease na kubaki na propaganda tu! Ukombozi wa kweli kwa miaka ya hivi sasa hautaletwa kwa maneno matupu kama enzi za Nyerere, La Hasha! Chukulieni mifano kule Misri, Guinea Bissau, Libya, Mali, Tunisia na kwingineko! Tatizo la Watz, they are good at talking but null in action.

  Kwa mfano, wapo watu kupitia JF walijitapa mwanzoni mwa mwezi huu kuwa wangemfungulia mashtaka Lusinde, tena wengine wakadai wana ushahidi na pia wange-support gharama za kesi. Swali ni je, umeshasikia kesi yoyote dhidi ya baradhuli yule? Au kusikia MwanaJF yeyote akiulizia status ili kama kuna sehemu tumekwama tuone tunasongaje mbele ili kutimiza azma yetu?

  Sasa iwapo ktk jambo dogo kama hilo tunaishia kubwabwaja tu, sembuse kuwang'oa Magamba? Is this not like cooking an empty pot expecting to get a nice soup?

  Sasa mimi natafuta saini za wananchi milioni 1 tuanze Movement for Change, ikibidi tuanze kwa migomo na maandamano mpaka kieleweke! Kama uko tayari ni-pm kwa usajili na kupanga mikakati kabambe. Misri walianza hivi hivi, kwanini sisi tusiweze?

  Kama kweli wanaJF mnakerwa na mwenendo wa serikali hii kama mimi basi tuunganishe maneno yetu yaoane na vitendo, otherwise we better stop here and leave Magamba wajigambe!
   
 2. M

  MVENGEVENGE Senior Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo umenene tena neno kubwa kinachotakiwa action weka utaratibu saini zteu utazipata.


   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Nimeku Pm mkuu
   
 4. c

  collezione JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Pamoja. Am on the list
   
 5. D

  Dewiny Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakika umenena hatuwezi kuikomboa nchi kwa maneno tunaitaji utaratibu mi nipo nawe!
   
 6. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hapo unakosea mambo ya PM haufiki mbali, sema kituo cha kukutana tuweke sahihi. Jf haitoshi kupata 1m vote, go public man hata polisi sasa ni wenzetu njaa zinawauma hawapigi tena bomu;uliza Tandahimba
   
 7. D

  Deo JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Onyesha njia ya vitendo basi basi!

  Au wewe stop kabla kwa sababu hawa wachangiaji hapa JF wanapandisha munkari kwanza mpaka pale mori ya vitendo ipande, hivyo usizuie huu mchakato
   
 8. M

  Mabelana JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Nyie acheni ujuha hayo mnayoyasema mtaumizwa nyinyi!? wenyewe hao mnaowaita wakombozi wako na maprado yao mbali sana.
   
 9. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  kunausemi umezagaa kwamba "Watanzania ni weng wa maneno kulko vtendo". Kauli hii ni ya muda mref sana na kwa kwel inatudhalilisha, inatufedhehesha na kuzd kuturudisha nyuma..tunapiga kelele "amkeni, amkeni." sasa sijui tunao waamsha wataamka lini, wakati wengi wa Tunaojarbu kuamsha tumejfunika kwa blanket huku tumelala ktandan tukikoroma! Au tunataka nani amfunge paka kengele? Wengi tunaogopa vta,fujo na kuvunja amani yetu, ni kweli (hata mi mwenyewe naogopa). Ila tujiulze, amani ipi tunailinda? Je ni hii ya mama wenye mimba kufa kwa kushndwa kununua mkasi? Ni hii ya kununua sukar klo 2500? Au ni hii ya kutimuliwa kwenye ardh yetu wenyewe? Au ni hii ya vjana kugeuka ombaomba ndani ya nchi yao kutokana na kukosa ajira? TAFAKARI ZAIDI YA HAPO..CHUKUA HATUA
   
 10. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160

  [​IMG]


  We zunguka wee! -hakuna njia nyingine! - Hii ndio njia mbadala pekee ambayo serikali na mafisadi wanasikia!
   
 11. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii picha imenitia moyo sana, na kunipandisha hasira. Hakika hii njia mbadala (Nguvu ya UMMA)
  Mtoa mada tunaomba uiunganishe hapo juu.
   
 12. M

  Mawinyi Yeye Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsimg ni kwamba maisha tunayo yaishi hivi sasa yametuchosha hasa ukizingatia tofautiya maisha tulio kuwanayo katiya waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho! na wakati huohuo unakuta kwamba mnae tofautiana nae kwakiasi kikubwa namna hiyo mnalingana/una mzidi katika ujuzi ila tofauti ni kwamba mwenzako anamtu anaemfahaku kwenye system! Kamahiyo haitoshi huduma za kijamii zinazo tolewa na serikali ya CCM ni duni kiasi cha kutisha ilihali viongozi wenyewe wana ishi maisha ya anasa! waTZ tuamke tusi kubali kuona upuuzi huu ukifanyika mbele ya macho yetu.
   
 13. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kina nani tena, wakati wakombozi ndio sisi? hii nchi ni yetu sote,. sio ya magamba wala watu gani, ni ya watanzania, na tunaamua kama watanzania!!!period
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Njia mbadala ni Raia!
   
 15. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Me too!
  Leta AK 47 hapa
   
Loading...