Kama Bunge likishindwa njia mbadala ni hii hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Bunge likishindwa njia mbadala ni hii hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SJUMAA26, Apr 20, 2012.

 1. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuendelea kuwatetea Watz kwa maneno matupu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa!. Kwa Watz hata upige makelele kama mtu aliyefiwa hakuna wa kukuelewa na mwisho ukipoteza Ubunge au wadhifa wako hakuna wa kukutetea wala kukumbuka! Hebu fikiria, wako wapi akina Sokoine, Kawawa, Abdul Jumbe, n.k?

  Ama walikufa vifo vya aibu, au wako hai ila ni kama wafu, hata hakuna anayekumbuka Memorial Days zao! Ndio maana wajanja walipogundua Chama si cha Mapinduzi tena bali ni cha kuchukua chako mapema wakazika Azimio la Arusha na, taratibu lakini kwa uhakika, wakakigeuza chama chao kuwa cha Majambazi, Mafisadi na Matapeli!

  Hata hawa wanaopiga makelele ni either wako nje ya system au hawako kwenye mtandao na ndio maana njaa zinapowapiga wanaanza kupiga kelele! Madaraka matamu jamani, hata hao wenye makelele wakipewa nchi utawaona tu, wao na Magamba itakuwa like father like son! Ukitaka ku-test hii Hypothesis, waambie wote wenye makelele nao waachie nyadhifa zote walizo nazo kama ishara ya kupinga mfumo uliopo...Weee, nani utampata??

  Hivi hamkumbuki suala la Posho lilivyokuwa? Je, ni kweli hao wapiga kelele wote hawazichukui hadi leo? Dr. Slaa wa watu alipiga makelele kuhusu UFISADI hadi akataja orodha ya vinara lakini mambo yalibaki vile vile, naona huyu Mzee wa watu atakuja kufa pasipo kuona Watz wakistuka, na badala yake nchi yao bado wanaendelea kuwakabidhi manyang'au wale wale waliotajwa! Tungekuwa serious, kwanza tungewaadhibu kwa kutowarudisha madarakani, lakini hata kama wangepita kwa wizi na ghiliba zao, basi serikali yao tungeikataa kwa migomo, maandamano na fujo, na ikibidi hata vita!

  Tatizo Watz wengi wanadhani makelele yao tu ndio yatawafanya Magamba wang'oke, thubutu...muulizeni Nape ameshawang'oa wangapi licha ya makelele yake nchi nzima hadi akaamua ku-cease na kubaki na propaganda tu! Ukombozi wa kweli kwa miaka ya hivi sasa hautaletwa kwa maneno matupu kama enzi za Nyerere, La Hasha! Chukulieni mifano kule Misri, Guinea Bissau, Libya, Mali, Tunisia na kwingineko! Tatizo la Watz, they are good at talking but null in action.

  Kwa mfano, wapo watu kupitia JF walijitapa mwanzoni mwa mwezi huu kuwa wangemfungulia mashtaka Lusinde, tena wengine wakadai wana ushahidi na pia wange-support gharama za kesi. Swali ni je, umeshasikia kesi yoyote dhidi ya baradhuli yule? Au kusikia MwanaJF yeyote akiulizia status ili kama kuna sehemu tumekwama tuone tunasongaje mbele ili kutimiza azma yetu?

  Sasa iwapo ktk jambo dogo kama hilo tunaishia kubwabwaja tu, sembuse kuwang'oa Magamba? Is this not like cooking an empty pot expecting to get a nice soup?

  Sasa mimi natafuta saini za wananchi milioni 1 tuanze Movement for Change, ikibidi tuanze kwa migomo na maandamano mpaka kieleweke! Kama uko tayari ni-pm kwa usajili na kupanga mikakati kabambe. Misri walianza hivi hivi, kwanini sisi tusiweze?

  Kama kweli wanaJF mnakerwa na mwenendo wa serikali hii kama mimi basi tuunganishe maneno yetu yaoane na vitendo, otherwise we better stop here and leave Magamba wajigambe!
   
Loading...