Kama binadamu wote wataenda Peponi au Jehanamu vipi kuhusu wanyama wengine?

chimela

Member
Jul 14, 2016
63
142
Wale wataalamu wa mambo ya kidini awe Muislam au Mkristo au hata Mhindu naomba kueleweshwa kuhusu Peponi na Jehanamu.

Imekua kawaida ya binadamu kujizungumzia yeye mwenyewe kwamba ndio ataenda peponi au Jehanamu lakini tukirudi katika vitabu vya dini tunaambiwa Mungu alituumba sisi pamoja na wanyama wengine kama Ng'ombe,Kuku, Mbwa nk.

Sasa swali langu ni je baada ya hao wanyama kufa either kwa kuliwa na sisi binadamu au kwa namna nyingine nao wataenda Mbinguni ?
 
majini na wanaadam ndio watawala wadunia na maamrisho na makatazo yanawahusu wao hakuna amri ya kufunga kusali kuhiji kutoa zaka kwa mnyama hivyo hukumu ya siku ya kiama na kwenda peponi ama motoni hayamuhusu mnyama
 
Holy Quaran aka KItabu chenye majibu ya maswali yote imesema kuwa watafufuliwa viumbe wote, watu wakiwa uchi,wanyama na manyoya yao , wanyama watageuzwa mavumbi mara baada ya kusikilizwa .binadamu tutaendelea na utaratibu wa kulipwa matendo yetu.
qur'aan haijasema hayo maneno,usimzulie mwenyezi mungu uongo,hapendi,hukumu ni kwa binaadam na majini tu
 
majini na wanaadam ndio watawala wadunia na maamrisho na makatazo yanawahusu wao hakuna amri ya kufunga kusali kuhiji kutoa zaka kwa mnyama hivyo hukumu ya siku ya kiama na kwenda peponi ama motoni hayamuhusu mnyama
vizuri
 
hakuna pepo wa jihanamu hizo ni habari za kutungwa tu.
wewe una akili ya kujenga nyumba ujikinge na mvua,ukiumwa unatengeneza dawa,unapona,wakat hayo nguruwe na nyani hawawez,hyo tofaut imekujaje?!..unataka kuishi kwenye nyumba(dunia) ya mtu bila sheria,we unaweza,fanya dhambi zako,jidanganye,ila mauti yakikufika utakutana nae
 
Habari za wanyama na ndege na viumbe vingine habari yao ni hapa hapa duniani ndio mwisho wao..
Wanyama na ndege na mimea wameandaliwa kwa ajili ya kutuwesha sisi tuishi katika hii dunia ,mfano mimea tunapata chakula na mavazi,wanyama tunapata chakula ,mavazi na usafiri,,
 
Hilo nalo swali maana tunajijali wenyewe kuliko wanyama ambao tulipewa kuwatawala. Wakati wa Nuhu wawili wawili waliingizwa kwenye safina kuhifadhi kizazi chao kwa matumizi ya baadaye. La kujiuliza kama huko nako wanagitajika basi watakuweko kama la wanachuo waseme. wengi wanasema katika hukumu watasimama Wanadamu
 
Back
Top Bottom