Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,858
Kwema Wakuu!

Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.

Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?

Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.

Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.

Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.

Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;

1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.

a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.

Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.

Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.

Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.

2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.

Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.

Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.

3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.

Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.

Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.

Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.

4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.

Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?

Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.

Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?

Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.

Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.

5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.

Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.

Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.

6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.

Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.

7. Mtiririko na visa na matukio ya Kihistoria.
Biblia ni kitabu ambacho kimeandikwa Kwa kufuata mtiririko wa visa na matukio unaoleweka. Kuanzia kisa cha Adamu mpaka Yusufu anachosimulia Musa, Kisha tawala za dunia kama Tawala la Nimrodi, kisha tawala la mafarao, kisha tawala la Waashuru na Wakaldayo, kisha wakafuata Waajemi na Wamedi, kisha wakafuata Wayunani/wagiriki, kisha wakafuata Warumi ndipo alipozaliwa Yesu.
Lakini Quran haina mtiririko wa visa na matukio, kumaanisha haiwezi kutumika hata shuleni Kama rejea za kihistoria kuhusu tawala, au mambo ya kuitawala au Kisiasa kwani Quran haijui wapi dunia imetoka ilipo na wapi inapoenda. Wakati Biblia inaeleza wapi Dunia ilipotoka na wapi ilipo na inapokwenda.

Quran inaweza kuulizwa swali, Yesu alizaliwa wakati WA utawala gani na wanani na ukashindwa kujibu?
Kimahakama Quran kama haijui baadhi ya taarifa muhimu kama Zama na Maeneo husika ya tukio lilipotukia haiwezi kutumika kama Rejea au ushahidi muhimu katika mambo ya Kidini.

Kwa mfano; Issa kazaliwa kwenye mtende Kwa mujibu wa Quran lakini haielezi ni eneo gani au nchi gani Issa alizaliwa, hata Hapa Tanzania ipo mitende, hii ni tofauti na Biblia inataja na kuelezea visa katika mtiririko uliokamilika.

8. KUjitosheleza, kujitegemea na kutoa taarifa zote muhimu.
Biblia inajitosheleza na kujitegemea Biblia kuhusisha kitabu kingine. Msomaji yeyote wa Biblia akimaliza kuisoma hatahitaji rejea za kitabu kingine.
Mfano msomaji akisoma kisa cha Yakobo, atajua Yakobo alizaliwa wapi, ndugu yake ni Nani, Routes zake zote, wake zake, watoto wake na umri wake mpaka anakufa. Kwa nini aliitwa Yakobo, ikawaje akabadilishwa jina n.k
Lakini Quran haijitoshelezi haina hizo taarifa muhimu. Hivyo kuifanya Quran kuwa tegemezi Kwa vitabu vingine.

Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Majaji mjadili kwa hoja.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Unaandika meengii halafu ni uharo tu, hata Musa kaandika kitabu kwa mkono wake(kwa mujibu wako, sababu kwenye bible haionekani hivyo). Yesu kaandika kitabu gani kwa mkono wake!?

Zaidi ya vitabu vingi vya Imani ya kikristo kuandika na Paulo ambaye hakuwa na time na Yesu alipokua hai!?

Hujui chochote kuhusu Qur'an. Unasema vitabu vyote kwenye Qur'an kashushiwa Muhammad peka yake, Qur'an ni kitabu kimoja hivyo vingi umevitoa wapi!?

Ibrahim alikua dini gani!? Maana najua alikua muhamiaji pale Yerusalem, alikua mwarabu wa Iraq!?

Neno eloi Kama mtamkavyo kwa lugha ya Yesu ni ilahi ina maana ya mungu wangu ambapo kwa kiarabu ni illahiy
 
Unaandika meengii halafu ni uharo tu,hata Musa kaandika kitabu kwa mkono wake(kwa mujibu wako,sababu kwenye bible haionekani hivyo)..yesu kaandika kitabu gani kwa mkono wake!?..zaidi ya vitabu vingi vya Imani ya kikristo kuandika na Paulo ambaye hakuwa na time na yesu alipokua hai!?...hujui chochote kuhusu Qur'an...unasema vitabu vyote kwenye Qur'an kashushiwa Muhammad peka yake, Qur'an ni kitabu kimoja hivyo vingi umevitoa wapi!?..Ibrahim alikua dini gani!?..maana najua alikua muhamiaji pale yerusalem,alikua mwarabu wa iraq!?..neno eloi Kama mtamkavyo kwa lugha ya yesu ni ilahi Ina maana ya mungu wangu ambapo kwa kiarabu ni illahiy
Naona alshabab mmefika kwa uzi, karibu ustaadhi.
 
Mtume Muhammad alikuwa ni mtu mwerevu sana.

Mwenye kumbukumbu nzuri na uwezo wa kusimulia hadithi alizozijua kutokana na kusafiri safiri kwake miji tofauti kibiashara.

Akiwa safarini Alisikia hadithi nyingi za dini zilizokuwepo kipindi hiko kutoka kwa Mayahudi (walioishi Arabuni wakati huo) na za Kikristo (kutoka kwa safari zake za kwenda Syria ki biashara) na akaunganisha hadithi alizozisikia kutoka kwenye dini tofauti hadi kwenye dini mpya aliyoianzisha ya kiislamu yenye hoja ya Mungu mmoja na yeye mwenyewe kama Mtume.

(Ni kama story za utani za kumsema nyerere enzi zile akiona kitu kwenye tv anakuja kusema ameoteshwa kwamba Marekani kimetokea hiki.. sababu watu wengine hawana tv wanaamini kaoteshwa kweli)

Alifanikiwa kuitumia dini hii mpya kufikia malengo mawili, moja la muda mfupi na moja la muda mrefu.

Malengo yake ya muda mfupi yalikuwa ni ya kumfanya yeye kuwa Chief Man in Arabia jambo ambalo alifanikiwa kulipata hadi wakati wa kifo chake na, baada ya kifo chake, warithi wake walifanikiwa kufikia lengo lake la muda mrefu la kuwafanya waarabu waitawale dunia kwa kutumia advantage waliyonayo ya uislam na lugha ya kiarabu isambae dunia nzima na waarabu wawe watu muhimu kwenye jukwaa la kimataifa

Ukisoma vizuri quran story zilizopo kwenye quran zinazungumzia mazingira ambayo Mohammad aliyajua tu (kwa kufika ama kusikia story zake). Mazingira ya mbali hayapo kwenye quran Maana alikuwa hajawai kufika na hakuwai sikia story zake. Maana ni mbali na uarabuni

Mfano matunda yaliyotajwa , wanyama waliotajwa kwenye quran, ndege waliotajwa kwenye quran, vyakula na mengineyo ni vya mazingira ya middle east tu ambayo Mohammad aliyaona ama aliyasikia kwa watu jirani zake ( Mungu angeandika Quran asingefanya hili kosa maana anayajua mazingira ya dunia nzima na angeyaweka kwenye quran)

The Qur’an really speaks only of the animals found in the Arabian lands (midle east) , and only the plants and fruits that grow in that geography.”

Also Foods known in the ( midle east) Arabian lands such as figs, grapes, pomegranates, dates, olives, honey, onions, garlic, gherkin, etc. have also been used in various Qur’anic verses and examples for various topics…

Jiulize Why do animal, and fruit names not belonging to the arab land doesn’t indicated in the Qur’an?

Utapata jibu Prophet wrote these names which he saw in places he went and he heard story from other merchants .

Inshort prophet Mohammad had a dream

Nothing was going to stop him from making that dream come true…

He came up with Islam to gain political power and to unite his people under the rule of one goverment

Ukijiuliza swali hili

Why does the Quran not mention prophets in America, Australia, Asia, Northern Europe, China, Japan, or South Africa?

Jibu litakalokujia kichwani haraka haraka ni hili

Because the writers of the Qur'an would not have been aware if these lands. Islamic religion is invented in one small area of the world (arabs land) which is why quran, hadith, & sunnah text only mentions things happen in that area only
 
Kwema Wakuu!

Kutokana na mjadala Fulani uliokuwa unaendelea katika jukwaa la intelligence nimeona nianzishe Uzi huu Kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia Kupima katika mizania ya kimahakama/ kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.

Nani Mkweli na Nani muongo Kati ya Biblia na Quran?

Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au myahudi Bali nipo kujadili Nani mkweli Kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama.
Majaji mtakuwa ninyi wasomaji;

Mahakamani sio kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa Sheria, Hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani Kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.
Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema Kwa vile mambo haya yanagusa Imani za watu Jambo hilo linaweza kuwa gumu.

Zifuatazo ni hoja Kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa Rejea kuu zaidi ya Quran. Kwa sababu;

1. Biblia Kwa sehemu kubwa haina maneno ya Hearsay wakati Quran Kwa 90% maneno yake ni Hearsay.
Kimahakama maneno ya hearsay hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa Kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu.
Hoja hii ndio hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.
i. Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, yona n.k.

Wakati Msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo.
Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita.
Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.

Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali Kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, mathayo na yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu walioshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya
Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka Kwa sababu yeye alisimuliwa. Hata hivyo ulikuwa ni wakati uleule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka.

Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.


2. Waandishi WA Biblia walikuwepo Maeneo tajwa kwenye Biblia.
Lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika Maeneo anayoyasimulia.
Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na waisrael ambapo hajawahi kupafika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.
Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman alafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman.
Wakati suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.
Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea Kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia.
Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.


3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa Kwa manabii tofauti tofauti Kwa nyakati tofauti tofauti wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshishiwa Muhammad.
Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu, kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha yakobo na yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu.
Na visa vyote hakuwepo😀😀.

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha yona kaandika Yoña mwenyewe, Kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu(wanafunzi waliomshuhudia)
Kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.
Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi Kwa sababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni Kama vile kitabu cha Mzee wetu mwinyi au Mzee wetu MENGI.

Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay) kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa Fact na ikachukuliwa Kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.

4. Biblia imeandikwa na Wayahudi Kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu Kwa lugha ya kiarabu lakini inasimulia habari za wasiowaarabu. Inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.
Yaani Mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo.
Hivi ninyi mtanisikiliza Mimi mpare ninayesimulia habari za kale za wasukuma au mtasikiliza wasukuma wenyewe?

Muhammad muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo alafu yeye anakuambia alizaliwa kwenye mtende alafu kuna mtu myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye Hori la ng'ombe. Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza Nani?

Haya Quran na hadithi za kiyahudi Kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga Majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji WA Daudi na mwanaye Suleiman, hajui kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.
Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini.
Lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu Kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo Majini.
Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika Vitabu vyake vilivyopo katika Biblia?
Jibu utabaki nalo.


5 Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah mungu wa waarabu wa kabila la wakurdi wa zamani lakini chaajabu huyo Allah ati huyo Allah kunasehemu anamuagiza kina Musa (myahudi na Dini yake uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.
Hata hivi leo Mungu WA Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu WA waarabu hajabadilika ni yuleyule Allah.
Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa muarabu

Wahusika kuanzia Kwa Yakobo mpaka Kwa Yesu ni Wayahudi na Dini Yao ni uyahudi na Mungu wao ni Yahweh.
Lakini Quran imepuyanga katika eneo H
Shida yako wewe ni ujuaji mwingiiii halafu empty mind jinga we! Haujui kitu utawapata wapumbavu wenzio tu
 
Una hoja tena nzito

Halafu Biblia ni kitabu chenye historia hata ya Ulimwengu wote

Mtu Kama Sir Isack Newton alichambua kitabu Cha Daniel vizuri Sana

Kupitia Biblia unakutana na Unabii wa Tawala za Alexander mkuu, vitu Kama hivi huwezi kukuta kwenye Quran

Kitu kingine ambacho nakipenda kwenye Biblia ,mfano kitabu Cha ufunuo kimetabiri kabisa Super power atakuwa U.S.A,

Miaka ya 80-90 ,watu walikuwa hawaamini Biblia inapotabiri mnyama wa 2 ambaye Ni U.S.A kuwa atakuwa Super power ,wakiangalia USOVIET USSR ilivyokuwa na nguvu .

Lakini Leo Nani atabisha U.S.A Sio Super power?

USSR ilisambaratishwa

Biblia ni kitabu kitamu Sana , Nimesoma Quran Sana tu ni kitabu hakieleweki, kinajichanganya, hakina Tumain lolote kwa mwanadamu

Nina shuhuda Zaidi ya 10000 za Biblia Ni kitabu Cha Mungu wakweli.

Aisee iacheni Biblia tu, Ni vile matapeli Kama mwamposa ,n.k wanaitumia vibaya kutapelia,

Lakini Biblia ina maajabu mengi sana
 
Kafanye kazi huu muda unaopoteza na kujiona muandishi uchwara utaujutia uzeeni!!!!
Screenshot_20221011-103927_Gallery.jpg
 
Vijana wa Tz hamnaga Jambo lolote la maana la kujadili zaidi ya Udini na Fikra Mfu. Tu na huu ndo mtaji wa Ccm kuhakikisha watu wanakuwa mazuzu
Jukwaa la elimu lipo, wewe kuna kufaa huko.

Jukwaa la siasa lipo.
Jukwaa la chitchat lipo
Jukwaa la vyakula lipo
Jukwaa la kilimo na mifugo lipo
Jukwaa la entertainment lipo
Jukwaa la michezo lipo
Jukwaa la teknolojia lipo
Nk.
Majukwaa yote yapo.

Wewe baki tu kwenye jukwaa lako.
 
Back
Top Bottom