Kama bei ya kununulia ndege inatamkwa katika vitabu vya Bajeti,ugumu wa kuweka wazi mikataba unatoka wapi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Binafsi nilitarajia usiri wa bei katika kununua
hizo ndege baada ya kukubaliana bei ndio iwe chanzo cha usiri wa mikataba ya manunuzi kwa malengo ya kibiashara(mteja mwingine nae aje ani-gotiate bei na terms za manunuzi kivyake).

Sasa kama gharama ya kununua hizi ndege imetajwa,nini tena msingi wa usiri huu?

Je,inawezekana bei iliyoko katika mikataba ni tofauti na iliyoko katika vitabu vya Bajeti?

Na je,kuna logic ya kujadili vitu vilivyoko katika mikataba ya siri?

Tusaidieni katika hili.
 
Mikataba ya biashara ni siri popote duniani haiwezi kuwekwa wazi kwa maslahi ya kampuni husika vinginevyo utakuwa umekiuka masharti ya mkataba.
 
Binafsi nilitarajia usiri wa bei katika kununua
hizo ndege baada ya kukubaliana bei ndio iwe chanzo cha usiri wa mikataba ya manunuzi kwa malengo ya kibiashara(mteja mwingine nae aje ani-gotiate bei kivyake).

Sasa kama gharama ya kununua hizi ndege imetajwa,mini tena msingi wa usiri huu?

Je,inawezekana bei iliyoko katika mikataba ni tofauti na iliyoko katika vitabu vya Bajeti?

Tusaidieni katika hili.

Hahaha sasa hivi mmeamia kwenye mikataba?
 
Mikataba ya biashara ni siri popote duniani haiwezi kuwekwa wazi kwa maslahi ya kampuni husika vinginevyo utakuwa umekiuka masharti ya mkataba.
Kama hiyo ndio hoja,kwanini mnashindwa kuitetea kama ni hoja halali?
 
Ipo siku mtaomba hadi mikataba ya kununulia ndege vita,maana mnaushabiki wa kishamba.

Nini maana ya kuwa na bunge? Bunge ndio wananchi wa Tanzania wao ndio wanatuwakilisha,muwe mnatumia akili.
Kama kuna wanaopitishwa na TUME wananchi tunawakilishwa na nani tuliyemtuma sisi?
 
Mkataba ni jambo la sili baina ya wahusika wawili iwe kampunia ,mtu binafsi nk ,lkn kama kuna umuhimu wa kuwekwa hadharani na ifanywe hivyo ,mkataba nia makubaliano ya jambo Fulani ambalo lina mwisho, mfano naingia mkataba wa kujenga ktk eneo lakobaada ya muda mkataba ukiisha mwenye eneo anachukua eneo lake, ununuzi hauwendani na mkataba huwezi andika mkataba wa kuuzinana kiwanja hapo utakuwa umekosea sana, sasa zile ndege zimenunuliwa hazipo ktk mkataba kwaana cc ndio wamiliki halali maana ktk ununuzi kunaweza kukuwa na mkataba ikiwa mnalipa kwa awamu awamu

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nilitarajia usiri wa bei katika kununua
hizo ndege baada ya kukubaliana bei ndio iwe chanzo cha usiri wa mikataba ya manunuzi kwa malengo ya kibiashara(mteja mwingine nae aje ani-gotiate bei na terms za manunuzi kivyake).

Sasa kama gharama ya kununua hizi ndege imetajwa,nini tena msingi wa usiri huu?

Je,inawezekana bei iliyoko katika mikataba ni tofauti na iliyoko katika vitabu vya Bajeti?

Na je,kuna logic ya kujadili vitu vilivyoko katika mikataba ya siri?

Tusaidieni katika hili.
Mbona hata airbus walionyesha bei za ndege hizo. Au tatizo ni kutokusoma vitu vya maana ila unasoma sana udaku au ukiambiwa na Lissu.
 
Mbona hata airbus walionyesha bei za ndege hizo. Au tatizo ni kutokusoma vitu vya maana ila unasoma sana udaku au ukiambiwa na Lissu.
Kuonyesha sio hoja kwani mkini-gotiate bei inaweza kubadilika na ikawa ni siri ya muuzaji na mnunizi kwenye mkataba /makubaliano ya mauziano.
 
Back
Top Bottom