Kama Barua yenu kwa Spika Ndugai imeitwa 'Kipeperushi' mkienda kukutana na Rais Samia angalieni tu asiwaite 'Wapuuzi' pia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,480
2,000
Ni kweli Spika Ndugai ana 'Mapungufu' yake, ila na Mimi GENTAMYCINE sasa taratibu naanza kuona pia kuna Matatizo ya 'Kimsingi' kwa upande wa Wapinzani ( hasa CHADEMA ) juu ya madai yao ama kwa Serikali au kwa Chama Tawala ( CCM )

Ushauri wangu tu Kwenu Marafiki zangu wa 'Kidemokrasia' nchini Tanzania CHADEMA kama Spika Ndugai kasema 'andiko' mlilompelekea ni 'Kipeperushi' basi nawaombeni mno anzeni Kujipanga hasa 'Kihoja' mnapojiandaa kwenda kukutana na Rais Samia katika Siku mtakayopangiwa ili baada ya kuonana nae asije kuwaita 'Wapuuzi' kwa yale mtakayoyawasilisha Kwake ambayo mmeyapania kweli kweli.

Kwa aina ya Uzungumzaji ule wa Spika Ndugai na ukiiangalia na 'body language' yake ( tena huku akijiamini kabisa ) tusifichane hapa ni lazima tu kutakuwa na Shida Kubwa ya 'Kiutendaji' kwa CHADEMA ila 'inafichwa' ama 'inafunikwa' tu kwa Mgongo wa Mapungufu ya Serikali na Chama Tawala chake cha CCM.

Ni wakati sasa wa Watu Makini ( Waelewa ) kuacha sana Kumshutumu Spika Ndugai 'Kimazoea' au kwa 'Kumkariri' na sasa tugeuke 'Kuwakosoa' hawa CHADEMA ili mwisho wa Siku tutende Haki kwa wote na tusijiingize katika 'Dhambi' ya kuja Kuitwa Wanafiki, Waongo na Wazushi tu wa Masuala.

CHADEMA anzeni 'Kujitathmini' haraka.
 
Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
15,322
2,000
Ndugai arudi Mirembe. File lake lipo kule.

Hivi kuandika barua kwake ni lazima uweke attachments zote hizo?

Yeye kama speaker anaesimamia wabunge wa vyama vyote ndio mwenye kutakiwa kuwa na katiba za vyama vyote ili ikija barua aweze kupekua na kuona je hao walioandika barua wako sawa au la.

Suala la kusema CHADEMA waambatanishe mambo kibao kwenye barua ni ujinga na haijawahi kutokea duniani.

Hiyo sio "report" ni barua. Mwambieni ajifunze kutofautisha.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,480
2,000
Umeona wapi uongozi huohuo umeseal deal wabunge waingie bungeni, then kesho wanawageuka ndio maana spika kamweleza nnauye kua haya mambo ni makubwa kuliko anavyofikiria
Taratibu naanza sasa Kumuelewa Spika.
 
Kichuchunge

Member
Dec 2, 2020
33
125
Ndugai arudi Mirembe. File lake lipo kule.

Hivi kuandika barua kwake ni lazima uweke attachments zote hizo?

Yeye kama speaker anaesimamia wabunge wa vyama vyote ndio mwenye kutakiwa kuwa na katiba za vyama vyote ili ikija barua aweze kupekua na kuona je hao walioandika barua wako sawa au la.

Suala la kusema CHADEMA waambatanishe mambo kibao kwenyw barua ni ujinga na haijawahi kutokea duniani.

Hiyo sio "report" ni barua. Mwambieni akifunze kutofautisha.
Hata mimi sijawahi kuona duniani, ina maana hamuamini Katibu Mkuu wa Chadema? Haamini kama walikaa vikao? Ya nini kuomba viambatanisho vyoote hivyo wakati kinachotakiwa ni barua tu! Au na barua nyingine za kiofisi ni lazima kila kitu kiwe na viambatanisho kama ripoti?
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,088
2,000
naunga mkono hoja yako...

CDM na upinzani Tanzania kuna shida kubwa ya kiuongozi ambayo inapaswa kufanyiwa kazi ili imani kwenye hivi vyama irudi... vyama vimejikita sana kulalamika hadharani kuliko kuja solution na kuweka hadharani the way forward yawanacholalamikia..

Hili suala la Covid 19 wanalalamika tu, hatua gani wanachukua kupata haki yao kama kweli ni uonevu unakuta hakuna...mwisho wa siku ukifikilia kwa kina unakuta wanawafanyia usanii tu wafuasi wao maana wanakua behind the scene...
 
Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
15,322
2,000
Hata mimi sijawahi kuona duniani, ina maana hamuamini Katibu Mkuu wa Chadema? Haamini kama walikaa vikao? Ya nini kuomba viambatanisho vyoote hivyo wakati kinachotakiwa ni barua tu! Au na barua nyingine za kiofisi ni lazima kila kitu kiwe na viambatanisho kama ripoti?
Ni uhayawahi wa mchana kweupe. Na wapumbavu wanaunga mkono hilo jambo bila kutumia akili.
 
Jerry Ekky

JF-Expert Member
May 6, 2018
1,133
2,000
Kwa hali ilivyo/inavyokwenda sioni km kweli CDM wanamaanisha juu ya madai yao, zaid naona wanatengeneza drama tuu japo sijajua ni kwa nini! haiwezekani upeleke majina ya wateule wako then uje useme tena huwatambui na umewavua uanachama kwa maneno makavu bila viambatanishi/vielelezo sababu umekwisha onesha una shida sehemu flani

Nadhani hili ni jambo la wakati tuu na litafikia mwisho hivi karibuni
 
Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,353
2,000
Ndugai arudi Mirembe. File lake lipo kule.

Hivi kuandika barua kwake ni lazima uweke attachments zote hizo?

Yeye kama speaker anaesimamia wabunge wa vyama vyote ndio mwenye kutakiwa kuwa na katiba za vyama vyote ili ikija barua aweze kupekua na kuona je hao walioandika barua wako sawa au la.

Suala la kusema CHADEMA waambatanishe mambo kibao kwenyw barua ni ujinga na haijawahi kutokea duniani.

Hiyo sio "report" ni barua. Mwambieni akifunze kutofautisha.
Huyu JOB hili pira kaachiwa mwenyewe maana nahodha wa mchezo sir god kamchukua. Polepole hana lake, Kakurwa ndio hajulikani yupo wapi. Huu mchezo wa hawa wabunge 19 ni aibu ya bunge. Wabunge wenyewe wamekiri kufukuzwa na wamekata rufaa sasa JOB anataka nini. Huyu mzee ni uchuro kabisa.
 
Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,353
2,000
Hata mimi sijawahi kuona duniani, ina maana hamuamini Katibu Mkuu wa Chadema? Haamini kama walikaa vikao? Ya nini kuomba viambatanisho vyoote hivyo wakati kinachotakiwa ni barua tu! Au na barua nyingine za kiofisi ni lazima kila kitu kiwe na viambatanisho kama ripoti?
Halafu mle ndani kuna wasomi wabunge wakati haya yakisemwa na JOB meza zikagongwa.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,382
2,000
Ndugai yupo kwenye mstari unaotenganisha wazima na wenye matatizo ya afya ya ubongo.

Fuatilia matukio mbalimbali ambayo yanahusisha baadhi ya wanachama waliokuwa wabunge walipofukuzwa na vyama vyao, na namna spika alivyotenda, kisha linganisha na alichotenda pale vyama vya upinzani vinapowafukuza uwanachama watu ambao ni wabunge. Bila shaka yoypte utajua kuwa Ndugai ni mwongo, mnafiki, mjinga, akili ndogo, na mlevi wa madaraka.

Angekuwa mkweli, hapo awali asingekana kuwa CHADEMA haikupelekea barua ya kuwafukiza COVID 19.

Kama asingekuwa mnafiki, angenena wazi kuwa alikuwa hana ubavu wa kushindana na marehemu, hivyo alilazimika atende kama mwendawazimu wa sheria ili aendelee kuwa kuishi.

Kama angekuwa mwerevu, angejua kuwa hapo awali alikwishakana kupokea barua ya kuwafukuza COVID19.

Kama angekuwa na akili kubwa asingetengeneza uwongo huu unaoyafanya maelezo yake mwenyewe yakinzane.

Angekuwa ni mtu anayetambua kuwa cheo ni dhamana, asingekuwa akitenda kazi zake kwa kuishia kingo za jengo la Bunge. Angefikiria zaidi kuijenga kesho kuliko kufurahia uovu wa leo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom