kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,408
- 7,190
Tukubaliane tusikubaliane Rais Samia kashakubali mradi wa Bagamoyo kwa masharti aliyoyakataa Magufuli na ambayo Kikwete aliyakubali. Kwa hivi sasa ni kiini macho kinafanyika. Watatumwa watu kimbelembele kuendesha mazungumzo.
Nionavyo mimi viongozi wabinafsi wamejaa kwenye ranks za CCM na bungeni kuliko wananchi wanavyofikiri. Kuna wanafikiri Magufuli kuhamishia makao makuu Dodoma na kufuta mpango wa Bandari Bagamoyo na huku kuwekeza maeneo ya ziwa aliafanya upendeleo.
Kila mwananchi amejua masharti ya kuwekeza bandari ya Bagamoyo baada ya Magufuli kuyataja. Vinginevyo yalifanywa siri. Kwanini viongozi wetu wakubali mashari ya kidhalimu namna hiyo kama sio kwa sababu za maslahi binafsi?
Licha ya Rais Samia kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja itakua ulaghai kwa kua anayofanya ni tofauti. Mradi wa bagamoyo wananchi watataka kuona mashari yake sio yale ya kikoloni aliyowaambia Magufuli. Kama bandari lazima ijengwe sio kwa masharti ya kuweka nchi rahani. Ni bora mradi ufe au tuje tujenge wenyewe kwa fedha yetu.
Tulimsikia kikwete akisema wapwani hawangependa mji mkuu uhamie Dodoma. Tumeona samia akirejesha shughuli za rais kila wakati Dar na sasa anataka bandari ya bagamoyo kujengwa kwa vyovyote.