Kama bado tuna ushirikiano thabiti wa kidiplomasia na China na Urusi Basi kuwa mpinzani ni uhaini na upinzani hautakuwa huru kamwe

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Demokrasia ya kupokezana madaraka kwa wajamaa ni kitu kisichoeleweka kabisa. Ingawa kwa shinikizo za kimataifa angalau China mwaka 1980 waliweka ukomo wa urais kuwa vipindi viwili. Na Russia 1992 vilevile. Lakini anayeyapokea lazima atokee chama tawala na mtiifu kwa Rais aliyepita.

Angalau ndio Demokrasia tuliyozoea. Ila miaka ya 2005 kuendelea Mambo yakabadilika Tena. Viongozi wakataka kuwa watawala. Marais hawakutaka tena kuachia ngazi mpaka wafe.

Na ndio wakapandikiza aina hiyo ya utawala dunia ya tatu. Juzi Kiongozi wa kijeshi wa Sudani, Pia mapinduzi ya Mugabe, Kiongozi wa Jeshi Uganda na Mapinduzi Afrika Magharibi yote yameonekana kuwa na mkono wa China na Russia.

Hivyo kwa misingi hiyo muafaka wa Mbowe na Samia hautakuwa na maana yoyote kama tutaendelea kupata ushauri wa kiutawala na China na Russia na kwao upinzani ni Uani au Ugaidi kamili.
 
Matatizo yenu yatatueni nyie wenyewe pasipo kuhusisha mkono wa mataifa mengine, mbona China na Russia hawawahusishi nyie ?.
 
Back
Top Bottom