Kama Babu wa Loliondo aliweza kuchota akili za watu, iweje wenye mamlaka washindwe?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Nafikiri wabongo tuna tatizo kubwa sana la kufanya reasoning juu ya mambo tunayoyasikia na kuyaona hasa mambo haya yanapofanywa na watu wenye mamlaka makubwa.

Hali hii imenifanya nisione ajabu kwanini hata Babu wa Loliondo aliweze kuteka akili za watu wakiwemo wasomi na viongozi mbalimbali.

Sisi tukiambiwa jambo na wakubwa hatujipi muda wa kutafakari na kujiuliza kama kuna kipya katika kauli na matendo yao.

Mtu anaweza kusimama akataja figure fulani fulani na watu wakawa impressed wakati hizo figure hawajui kama ni za kweli au laa!

Mtu anaweza akasimama akaongea mambo yale yale ila akayakuza kidogo tu baadhi ya watu wakawa impressed!

Mtu anaweza kufanya mambo yasiyoofaa leo alafu baada ya muda akaja na .maneno matamu wata wale wale wakaanza kumshangilia!

Mtu anaweza kuwa anaongea mambo mazuri jukwaani lakini sera na matendo yake haviendani kabisa na maneno yake na bado wafu watamshangilia.Hawana muda wa kupima wala kutafakari!

Mtu anaweza kuongea mambo ya kutafuta huruma majukwaani kuwa anafanya kazi ngumu lakini mtu huyo hawezi kuacha hiyo kazi hata kwa mtutu na bado watu watakuwa impressed na maneno yake!!

Mtu anaweza kuwaletea vitu vya kufurahisha fahari ya macho alafu kesho akawafanyia jambo la kuumiza nafsi zao na bado wasijali!!

Sometimes hakuna tofauti na mzazi anaemchapa mtoto alafu baada ya nda anampa mdoli na mtoto anaanza kufurahi!!

Watu hawajipi muda wa kupima na kutafakari kisha wafanye maamuzi. Hawana muda wa kupima mambo kwenye mizani na kuangali mizani inaelemea wapi na kama iliko elekea kuna stahili au hapana.

Yaani mtu una mizani ambayo upande mmoja umeeja maneno mengi mazuri na upande mwingine imejaa vitendo kiduchu ila kwasababu uzito wa maneno umezidi ule wa vitendo, basi na wewe unachukua kipimo cha huo mzani na kuridhika na matokeo. Pathetic

Matokeo yake Inabidi watu wachache wenye akili zao wafanye kazi ya kutafsiri maneno haya matam ili watu wasipotoke mithili ya viongozi wa dini wanaotafsiri maandiko ili watu wayaelewe /wasipotoshwe.

Hakika tuna safari ndefu.
 
Kama Magufuli kasema wazi kabisa kuwa katiba mpya si kitu kwake na akashangiliwa na wasomi unategemea nini mkuu!

Taifa hili linahitaji mapinduzi makubwa sana ya kifkra toka kwa wananchi wenyewe, maana viongozi hawa waliopo wapo kwa ajili ya kudumisha madaraka na siyo kwa manufaa mapana ya umma
 
Wasomi wachumia tumbo hawawezi kutumika kama sample halali ya kufanyia utafiti , wananchi tulio wengi tutashinda na kupata katiba .
 
Nafikiri wabongo tuna tatizo kubwa sana la kufanya reasoning juu ya mambo tunayoyasikia na kuyaona hasa mambo haya yanapofanywa na watu wenye mamlaka makubwa.

Hali hii imenifanya nisione ajabu kwanini hata Babu wa Loliondo aliweze kuteka akili za watu wakiwemo wasomi na viongozi mbalimbali.

Sisi tukiambiwa jambo na wakubwa hatujipi muda wa kutafakari na kujiuliza kama kuna kipya katika kauli na matendo yao.

Mtu anaweza kusimama akataja figure fulani fulani na watu wakawa impressed wakati hizo figure hawajui kama ni za kweli au laa!

Mtu anaweza akasimama akaongea mambo yale yale ila akayakuza kidogo tu baadhi ya watu wakawa impressed!

Mtu anaweza kufanya mambo yasiyoofaa leo alafu baada ya muda akaja na .maneno matamu wata wale wale wakaanza kumshangilia!

Mtu anaweza kuwa anaongea mambo mazuri jukwaani lakini sera na matendo yake haviendani kabisa na maneno yake na bado wafu watamshangilia.Hawana muda wa kupima wala kutafakari!

Mtu anaweza kuongea mambo ya kutafuta huruma majukwaani kuwa anafanya kazi ngumu lakini mtu huyo hawezi kuacha hiyo kazi hata kwa mtutu na bado watu watakuwa impressed na maneno yake!!

Mtu anaweza kuwaletea vitu vya kufurahisha fahari ya macho alafu kesho akawafanyia jambo la kuumiza nafsi zao na bado wasijali!!

Sometimes hakuna tofauti na mzazi anaemchapa mtoto alafu baada ya nda anampa mdoli na mtoto anaanza kufurahi!!

Watu hawajipi muda wa kupima na kutafakari kisha wafanye maamuzi.Hawana muda wa kupima mambo kwenye mizani na kuangali mizani inaelemea wapi.

Yaani mtu una mizani ambayo upande mmoja umeeja maneno mengi mazuri na upande mwingine imejaa vitendo kiduchu ila kwasababu uzito wa maneno umezidi ule wa vitendo, basi na wewe unachukua kipimo cha huo mzani na kuridhika na matokeo

Matokeo yake Inabidi watu wachache wenye akili zao wafanye kazi ya kutafsiri maneno haya matam ili watu wasipotoke mithili ya viongozi wa dini wanaotafsiri maandiko ili watu wayaelewe /wasipotoshwe.

Hakika tuna safari ndefu.
A dreamer be the one  A winner be the one  A fighter be the one.jpg
 
Kama nyumbu walivyotiwa chuki dhidi ya Lowasa halafu wakaja kupewa tena kumsafisha.
KATAA KUWA NYUMBU
 
Back
Top Bottom