Kama baba wa taifa angekuwepo angesemaje kuhusu mtandao wa jamii forum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama baba wa taifa angekuwepo angesemaje kuhusu mtandao wa jamii forum

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Jun 23, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  KAMA BABA WA TAIFA ANGEKUWEPO ANGESEMAJE KUHUSU MTANDAO WA JAMII FORUM
  Nafikiri mnakumbuka kauli ya baba wa taifa mwaka 95 juu ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa msitari wa mbele kukosoa maovu na ufisadi wa serikari wakati huo ndio mfumo wa vyama vingi ulikuwa umeanza na vilikuwa bado havijaleta changamoto ya kutosha.

  Baba wa taifa alivisifu vyombo hivyo na kusema vinafanya kazi nzuri kuliko vyama vya upinzani ingawa vyombo hivyo kwa upande mwingine vilionekana kama maadui wa serikali na hiyo ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na waandishi wa wakati ule kuzingatia maadili na taalima yao.

  Natamani leo hii angekuwepo na kushuhudia mtandao wa jamii forum ambao unafanya kazi kubwa ya kufichua maovu wakati vyombo vyetu vingi vimetafunwa na mdudu wa rushwa na wamiliki wao kulinda maslahi yao.

  Ingawa Jamii forum imekuwa ikipingwa na viongozi wengi wa Chama Tawala na hata baadhi wa upinzani naamini yeye angetoka na msimamo tofauti angewasifu na kuwataka viongozi wao kukabilia na changamoto zinazotolewa na mtandao huu na vilevile angeweza hata kuwa mwanachama na kutoa michango mbali mbali ukichukulia alikuwa bingwa wa kujenga hoja.

  Mwisho hayo ni mawazo yangu binafsi ingawa wengine mnaweza kuwa na mtazamo tofauti
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Angeifagilia saaana
   
 3. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni vigumu kumhukumu Nyerere kwa kauli ya kama angelikuwepo! Hukumu sahihi ni iwapo yeye kwenye utawala wake wa miaka takribani 25,yaani robo karne aliruhusu uhuru wa kufikiri tofauti naye na kumpinga hadharani, uhuru wa kumkosoa kwa maamuzi ya kiutawala aliyoyafanya na uhuru wa Vyombo vya HABARI kukosoa, hata kuifurahisha jamii.

  Cha msingi kila mchezaji aliyeko nje ya uwanja huweza kuukosoa sana uchezaji wa walio uwanjani ilhali hata yeye aliboronga akiwa uwanjani pia
  Natoa hoja kwamba UHURU niliotaja hapo juu ulififishwa mno wakati wa UTAWALA wa Nyerere,kuliko wakati mwingine wowote hapa nchini
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa mawazo yangu naona kuwa kama Baba wa Taifa angekuwepo kwa kiasi fulani tusingefika hapa tulipo leo kwani naamini kwa dhati kabisa kuwa asingemruhusu huyu jamaa DHAIFU kuwa mkuu wa hili Taifa akiwa na huo UDHAIFU wake!

  Vile vile, ni wazi kuwa Baba wa Taifa angekuwepo na kuendelea kuwa mwana CCM na hali ikawa kama ilivyo leo, angeiponda jf vibaya sana kwani hakuna mwana CCM yeyote mwenye ubavu wa kuitetea JF.

  Huo ndo mtazamo wangu.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kiongozi yeyote FISADI wa Mali ya Umma, Wake za Watu au kodi zetu hizi za kuungaunga, awe ndani ya upinzani au Chama Tawala, kamwe hawezi kuipenda Jamii Forums katika maisha yake!!!
   
 6. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nyerere alisoma kipindi cha ukoloni wa waingereza, masters akasomea Endiburgh hukohuko Scotland ambako nashindwa kupaita kama ni Uingereza au vipi maana kuna waswahili wengi wakitaja neno "Uingereza" basi maana hiyohiyo wanamaanisha "England" au "UK" wakati ni vitu viwili tofauti na hadi leo sijajua ni kipi hapo ni Uingereza.

  Nyerere alikuwa mmoja wa wataalamu wazuri wa history hapa duniani. Ukiwa mtaalamu wa history maana yake unajua kwamba cartoon kama zile za gazeti la Punch lilianzishwa July 17 1841 yaani miaka 81 kabla hajazaliwa. Alilijua ni gazeti la vichekesho lakini limejaa mafumbo ya ukweli ambao yaliwalenga watawala na wanajamii wajirekebishe maana ujumbe ulikuwa unakwenda moja kwa moja kwenye jamii.

  Kumbuka gazeti hilo liliwahi kuchora picha ya Cecil Rhodes akiwa amekanyanga ncha mbili za Africa yaani Tunisia na Cape Town wakimaanisha kwamba Kampuni yake imetawala Africa yote.

  Hivyo alilijua hilo gazeti la PUNCH. University of D'Salaam ilipoanzishwa wanafuzni wa pale wakaliiga gazeti hilo kwa kuwa wanachora katuni wakisema hizo cartoon ni version ya ya gazeti hilo {PUNCH}. Sanasana UDSM wakaliongezea jina badala ya kuliita tu ggg wakaliita MZEE PUNCH

  Nyerere mwenyewe alikuwa anachorwa kila leo na wenzake kina Kaunda, Obbote na wengi tu. Lakini hata siku moja hakukemea MZEE PUNCH hadi anatoka kwenye utawala wake.

  Lakini mwaka 1990 MZEE PUNCH alipomchora Rais Ali Hassan Mwinyi ikatangazwa nchi nzima kana kwamba hilo lilikuwa jambo geni wakati wale wanafunzi wamefanya vile tangu chuo kilipoanzishwa.

  HUo ni mfano mdogo tu wa uelewa wa Nyerere na kutabiri ambacho angefanya sasa.

  Hivyo, haya mambo Nyerere aliyajua hata kabla hajaanza kupigania uhuru. Hivyo, kitu kama hiki Jamii Forum angeona ni version nyingine tu ya maendeleo ya watu kujieleza.

  Na kama wangetokea viongozi wakakemea JF kama asingekaa kimya basi angewaumbua kama mleta mada alivyosema na ninavyokumbuka alipomsifia Stanslaus Katabalo wa MFANYAKAZI na wenzake walivyoenda kumuuliza Msasani kama ukosoaji wao ni sahihi au la.

  Hivyo, asingekuwa na tatizo kabisa na michango ya JF hata kama angeonana na Moderatprs wa JF. Sanasana angewaambia wajihadhari na watu wanaotaka kuifanya JF ionekane kama genge la wahuni kwa kutoa matusi au kupindisha mada kwa sababu tu wameguswa.
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Angeiunga mkono na Angekua member wa jf
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sidhani kama angeweza kusema lolote kwa kuwa amekufa huku akiwa hajui kutumia kompyuta....
   
 9. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hii thread sidhani kama utatupeleka tunapohitaji, leteni hoja tujadili acheni mambo ya ",kama angekuwepo" huku hayupo na hatakuwepo. Ni bora tumjadili lionchawene aliefumaniwa
   
 10. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Angejiunga lazima na jf kwa sababu he was great thinker
   
 11. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  imejaa uchagauchaga?
   
 12. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  (sidhani kama angeweza kusema lolote kwa kuwa amekufa huku akiwa hajui kutumia kompyuta....) Ndio maana nimesema kama angekuwapo kwa nimeona viongozi wengi wanaposemwa humu jamii forum wanashindwa kujibu hoja badala yake wanaamua kuushambulia mtandao wa jamii forumimejaa uchagauchaga? (imejaa uchagauchaga?)
  Mimi sio mchaga nasielewi kwanini unajenga hoja kwa kutumia ukabila
  hayo niliyowasilisha ni mtazamo wangu sio lazima uwe sahihi na silazimishi kila mtu akubaliane na mimi nitaheshimu michango yenu yote bila kujali kama inanikosoa au la
   
 13. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  nyerere was very unpredictable...angeweza kuunga mkono hii kitu ila angeweza kupinga vile vile...
   
 14. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Philip Ochieng mkenya aliyewahi kufanya kazi Daily News kipindi cha utawala wa Nyerere alibainisha hivi karibuni kuwa enzi hizo gazeti hilo la serikali lilikuwa likimkosoa hadi kumkashifu rais Nyerere na hakuwahi kuwazuia.
  Mwalimu was an advocate of free speech
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Ange ipa big up!
   
 16. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Angesema wazo la kuanzisha JF ni zuri ila inahitajika forum nyingine ambayo moderator wake hawata fungamana na mawazo ya ushabiki wa chama cha siasa!
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuna hii hoja kuna mawili; nyerere akiwa rais au akiwa amestaafu urais

  a. Katika kipindi cha Urais JF na waanzilishi wake wangepotea moja bila kujua wameenda wapi..chezea dikteta wewe???

  b. Katika kipindi alipostaafu angewasifu maana na yeye alikuwa/alibaki mlalamika kama sisi japo tulimpa/alijipa miaka 24 bila maendeleo yeyote zaidi ya maendeleo ya dini yake na kanisa lake (st. nyerere mungu akurehemu)
   
 18. Malunkwi

  Malunkwi JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  asingemind chochote zaidi ya kuwaambia ccm wackilize na kutekeleza maoni ya wanajamvi
   
Loading...