Kama atafanikiwa kwenye hili basi atakuwa ndio Rais bora katika historia ya Tanzania na huenda akakumbukwa kwa vizazi hata vizazi

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,983
4,080
UTANGULIZI:

Nimiaka zaidi ya arobaini (40) sasa tangu kugunduliwa kwa uwepo wa gesi Asilia huko Likong'o-Mchinga Lindi Pembezoni mwa bahari ya Hindi yenye futi za ujazo trilioni 57.7,

Gesi hii baada ya kuchimbwa na kupoozwa kwa nyuzi Joto -260`F au -162'C nakuwa gasi miminika ndio inaitwa kitaalamu Liquefied Natural Gas (LNG) au inaweza kugandamizwa kwa Pressure kali ya 3'600 na kuitwa compressed Natural Gas (CNG) na hii ni baada ya kuondoa H20,CO2,SO2 na O2 hivyo kubaki gesi Safi ambayo inatumika kutoa Joto,kupoza vyakula,kuendesha magari, et El,

Tangu mwishoni mwa awamu ya nne Makampuni makubwa ya BG (Shell)ya Uingereza na Uholanzi, ExxonMobil ya Marekani,Ophir ya Uingereza, Pavilion ya Singapore,Medco Energi ya Indonesia; na StatOil (Equinox) ya Norway wanaendelea sitaki nataka ili kuwekeza karibu Tshs 70trilioni au $30bl huko Likong'o Mchinga -Lindi,

Mradi huu utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu 15 na ajira ya muda elfu 5 na kuzalisha jumla ya tani 10M za LNG kwa mwaka, utaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa nne Africa wa Gesi asilia na kuingizia nchi fedha za kigeni zaidi ya $5.5BL au Tshs 13trilion kwa mwaka kwa kuuza hiyo tani 10 kwa bei ya $11 kwa mmbtu, Pesa hii ni sawa na 100% ya bajeti nzima ya "Maendeleo" ya nchi kwa mwaka mmoja wa Fedha.

Kwa msiofahamu,Mradi huu wa Likong'o-Mchinga Lindi ni miongoni mwamiradi mikubwa mitano Africa ikiwemo ule wa Rovuma-Mozambique wa $30BL wenye 85tct utakaomalizika 2025,Mozambique LNG wa $20BL wenye 75tct utakaomalizika 2024,Ogidigiben wa $20BL wa Serikali ya Nigeria wenye 18tct na Zabazaba wenye 93.8tct mali ya Shell Nigeria,

Hapa unaweza kuona ushindani ulivyomkubwa na wenzetu wanazo deposit kubwa kuliko sisi na baadhi yao wamekubali kuwa na Visima ndani ya maji (floating plant) ambavyo vinapunguza gharama kwa 35% ndio maana Mozambique LNG inajengwa kwa $20BL,

Pamoja na kwamba mfumo huu kuibiwa ni lazima,Sisi tutajenga mashine km 120 toka baharini ili kuilinda hii mali tuliyopewa na Mungu Serikali yenu ni makini sana "Kawia ufike "

Kama Rais Samia Suluhu Hassan atafanikiwa kuwashawishi hawa matajiri na kwa hulka yake tunaamini atafanikiwa na tunamwombea,Lakini pia bei ya LNG imepanda duniani na inatarajiwa kupanda zaidi na kufikia $40/mmbtu hapo baadae toka $2/mmbtu (Nchi kama Marekani peke yake inahitaji 3.6tct kwa mwaka) lakini pia kwa kuzingatia Amani na Umoja uliopo Tanzania,

Kwaviwango vidogo vya kodi pamoja na Sera zinazotabirika za Fedha na Uchumi awamu hii lazima HGA ifikie mwisho ili tuendelee na Pre-FEED ili ifikapo mwaka 2028 kabla Rais Samia hajaondoka Madarakani atukabidhi zawadi hii ya kihistoria tangu nchi hii kuumbwa huku Watangulizi wake wote wakiambulia patupu,

Uzoefu unaonesha maeneo mengi PSAs zilipitishwa kwa Serikali kupewa 20% ya shares zote kama hili litafanyika kwetu pia basi Tanzania itapokea wastani wa Tshs 3T kama mrabaha kwa kila mwaka kwa miaka yote ya mradi,Pesa hii inaweza kujenga SGR toka Isaka -Mwanza Km 341,

Lakini pia kama 10% tu ya gasi yote ikibakishwa nchi kwaajili ya matumizi ya ndani kama maombi ya Serikali yalivyo hapa tutakuwa na ziada ya karibu tani 800K za gesi kwa mwaka kwani mahitaji yetu ya gesi bado ni chini ya Tani 200K hapa tujiandae kununua Kg 30 za gesi kwa buku ten tu na ndio maana nasema hapa Rais Samia atakumbukwa vizazi na vizazi tuendeleze dua na maombi ili kumtia nguvu,"mwenye masikio na asikie sasa ule mfupa uliowashinda wengine unatafunwa kama muhogo "
photo_2021-10-26_01-27-37.jpg
VIVA SAMIA VIVA || VIVA MAKAMBA VIVA
 
Mabeberu yanazingatia mambo makubwa matatu,

1. Utawala wa Sheria jambo ambalo Rais Samia kaliweka vizuri,

2.Political Stability hili dunia inajua Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ndio maana kule Konde ACT ikashinda mabeberu wanataka hayo,

3. Wanataka kuweko na Sera tabirika za Uchumi Rais Samia amefanya hili,

4. Wanataka Usalama wakutosha kwa wao na mali zao hili halina Shaka Tanzania,

#Awamu hii mama anamaliza mchezo,
 
Kwangu mimi Rais nitakayemkumbuka ni yule atakayewapatia watanzania urithi wa vizazi na vizazi yaani Katiba mpya ya nchi itakayotokana na mawazo yao wenyewe ambayo itakidhi mazingira ya sasa ya kimaisha.

Haya mengine mnayoyaandika kwa sasa naona ni muendelezo ya yale yale, kinachotakiwa ni kutibu chanzo cha yote haya, kutibu matawi ni kujichosha tu ndugu zangu.
 
Uko sahihi mkuu

Namuona Rais Samia akitikisa ndani na nje ya Tanzania

Ipo siku tutanunua gesi kwa buku ten tu Kg 30.

Kazi iendelee
 
Kwangu mimi Rais nitakayemkumbuka ni yule atakayewapatia watanzania urithi wa vizazi na vizazi yaani Katiba mpya ya nchi itakayotokana na mawazo yao wenyewe ambayo itakidhi mazingira ya sasa ya kimaisha.

Haya mengine mnayoyaandika kwa sasa naona ni muendelezo ya yale yale, kinachotakiwa ni kutibu chanzo cha yote haya, kutibu matawi ni kujichosha tu ndugu zangu.
Huu mradi sio urithi mkuu Wangu?

Katiba majibu Rais alishayatoa najua unakumbuka chief
 
Back
Top Bottom