Kama anayevumbua anavumbua kitu chema, kizuri kwanini anayetumia anatumia vibaya: Kuna nini hapa?

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Ukiangalia vumbuzi zote Duniani ni njema, nzuri kwa ajili ya kufanya maisha si tu kuwa mepesi bali bora zaidi. Hakuna uvumbuzi ambao umefanyika duniani ambao ni mbaya.

Kinachokuwa kibaya ni matumizi ya vumbuzi. Vumbuzi hizi tunaona katika historia kuwa zinafanywa na binadamu. Kuna vumbuzi nyingi katika nyanja mbalimbali na zote binadamu ndiye amekuwa akivumbua. Kuanzia kwenye sayansi asili mpaka kwenye sayansi ya jamii, kote binadamu amevumbua mambo mbalimbali na kufanya maisha ya mtu kuwa bora zaidi toka kizazi kimoja hadi kingine.

Uvumbuzi wa mashine, kwa mfano umesababisha hatua kubwa ya maendeleo katika viwanda na kilimo kupigwa pakubwa.

Sasa uvumbuzi wa teknolojia. Kizazi cha karne ya 21 kinashudia si tu uvumbuzi wenyewe lakini pia maendeleo makubwa ya teknolojia ya mawasiliano na habari, usafirishaji na utabibu.

Uvumbuzi huu ambao binadamu amekuwa akivumbua umemwezesha mtu kujibu na kufafanua maswali magumu ambayo karne na karne yamekuwa mjadala usiofika mwisho.

Kwa mfano, swali kuhusu mwanzo wa vitu na nini maana ya maisha kupitia maarifa na uvumbuzi wa kisayansi ufafanuzi na ushahidi wa maswali hayo msingi umeelezwa wazi, hatua kubwa imefikiwa japo si kwa ukamilifu wote.

Hakuna anayeweza kuainisha kuwa vumbuzi hizi zilizofanyika ni mbaya au ovu. Kwa asili vumbuzi zote zimekuwa na zinaendelea kuwa njema na nzuri.

Hatahivyo matumizi ya hizi vumbuzi au haya maarifa ndio yamekuwa na yanaendelea kuwa mabaya na ovu.

Hapa ndipo najiuliza:

Kama mvumbuzi ni mmoja yaani binadamu na anavumbua kitu chema kwa nini huyo huyo binadamu anatumia vibaya?

Inawezekanaje binadamu yule yule akavumbua kitu chema na huyo huyo akatumia hicho kitu chema alichokivumbua vibaya? Au uvumbuzi na binadamu ni vitu viwili tofauti?

Akili inatuwezesha kuvumbua, kugundua na kupata maarifa ya mambo na vitu mbalimbali. Katika hili tunaona kuwa akili inafanya mambo mema na mazuri.

Fikiri kwa mfano, mambo ya ujenzi wa nyumba, utengenezaji wa magari, uvumbuzi wa dawa na matibabu, elimu na maarifa ya vitu mbalimbali. Haya yote mtu ameyapata kwa akili. Ni akili tu ndio inafanya haya na mengine mengi mazuri, mema.

Sasa kama akili ndio inatupatia hayo yote mema, mazuri ndio hiyo hiyo unatufanya tutumie hayo mema iliofanya vibaya?

Inawezekanaje akili inayofanya mema ifanye pia mabaya? Hapa nataka tuangalie uvumbuzi. Je, kuna uvumbuzi au maarifa mabaya?

Ndipo hapa najiuliza hivi:

Kuna akili ya juu inayovumbua ambayo hiyo ni tofauti na huyu mtu inamotumia kufanyia uvumbuzi wake?

Kwa heshima kubwa nikaribisha wenye ufahamu zaidi mnielimishe. Karibuni!
 
Ukiwa unapitia vitabu vya dini zetu mbili kuu utaona vinaeleza kuhusu tunda la mti wa mema na mabaya na Adam na Mkewe Hawa walipokula wakapata kujua mema na mabaya . kabla ya kula tunda walijua mema tuu, utaona kusudi la mungu ni Binadamu azungukwe na wema tu lakini kutokana na kwenda kinyume na agizo la Mungu Binadamu anakabiliwa na mabaya pia ambayo tunaamini yanatoka kwa bwana Shetani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom