Kama anatafuta dowans nyingine ajaribu-mmiliki wa palm beach amwambia tibaijuka

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,887
21,973
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mmiliki wa kiwanja cha palm beach kinachosemekana ni batili ameamka na kumwambia mh waziri pamoja na kuandika barua na yeye kukataa kukutana nae anamshauri aombe washauri wake mawazo kwani asije juta kuwekeza DOWANS nyingine na kuikuta serikali ikiishia kulipa madeni

Kazi ipo
Mmiliki Palm Beach amvimbia Tibaijuka
Amwonya asisuthubutu kuvunja ukuta
Send to a friend Wednesday, 15 December 2010 20:46 0diggsdigg


prof%20anna%20tibaijuka.jpg
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Nora Damian
MMILIKI wa kiwanja kilicho jirani na hoteli maarufu ya Palm Beach iliyoko jijini Dar es Salaam ambaye Serikali imemtaka abomoe ukuta wake kwa kuwa ni eneo la wazi, ametishia kumshtaki Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akidai kuwa analimiki eneo kihalali.

Mmiliki huyo alikutana jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anakusudia kumshtaki Waziri Tibaijuka kwa kuwa ameidharau Mahakama.
Mmiliki huyo, Taher Muccadam alisema Waziri Tibaijuka amedharau amri ya mahakama kwani alishinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kuendelea na ujenzi katika kiwanja hicho.

Alisema kiwanja hicho namba 1,006 kilichopo Upanga anakimiliki kihalali na kwamba ana uthibitisho na vielelezo vyote vinavyomhalalisha kumiliki eneo hilo.
“Tibaijuka awe makini sana, hasa anapotaka kufanya maamuzi. Anaweza akaisababishia hasara Serikali kwa kulipa fidia,”alisema Muccadam.

Alisema eneo hilo si kiwanja cha wazi bali ilipendekezwa tu lakini, baadaye Manispaa ya Ilala ilitoa hati namba 186164/25 kwa wamiliki wa kwanza ambao ni Shantaben Narottambahi Patel na Nilaben Girishumar Patel mwaka 1975.

Alisema Desemba 6, 1975, Wizara ya Ardhi iliwazuia wamiliki hao kukiendeleza kiwanja hicho kwa sababu kilitakiwa kiwe cha wazi na kwamba waliahidiwa kiwanja mbadala namba 1019 kama fidia.

Muccadam aliendelea kueleza kuwa lakini, kiwanja hicho namba 1019 walichotakiwa kupewa wamiliki hao, kilichukuliwa na kumilikishwa kwa AMREF.

"Baadaye wizara iliamua kuwaruhusu waendeleze kiwanja chao cha zamani kwa kuacha upana wa futi 20 kati ya barabara ya Magore na Upanga.

Katika mkutano huo Muccadam alionyesha vielelezo mbalimbali kuhusu kiwanja hicho, ikiwemo barua ya Kaimu Kamishna wa Ardhi F. Luvanda yenye kumbukumbu namba LD/75708/101/LK ya Mei 25 mwaka 2005.

Katika barua hiyo, Kamishna huyo alipendekeza kuwa ili kumaliza mgogoro huo, kiwanja hicho kigawanywe na wamiliki wapate sehemu ya kuendeleza kwa matumizi ya ofisi na hoteli na eneo lingine libaki wazi.

Kwa mujibu wa Muccadam, tayari amemwandikia barua Waziri Tibaijuka kumjulisha suala hilo lakini hakuijibu barua hiyo wala hataki kukutana naye.

Alisema alinunua kiwanja hicho ili ajenge jengo la ghorofa 22, lakini tangu wakati huo, ameshindwa kuanza ujenzi kutokana na kuwepo kesi mbalimbali mahakamani kubishania kiwanja hicho.

Muccadam alisema mwaka 2000, kiwanja hicho kilifutwa kwa makosa, hivyo suala hilo lilipelekwa Mahakama Kuu na kufunguliwa kesi namba 70/2004 na baadaye Wizara ya Ardhi ilipendekeza mgogoro umalizwe nje ya mahakama.

Alisema aliendelea na malumbano hayo Mahakama Kuu kwa muda wote huo na hatimaye alishinda kesi na kurudishiwa kiwanja hicho na kwamba mahakama ilikubali alipwe fidia ya dola za Marekani 6 milioni kama gharama za ujenzi huo.

Katika hatua nyingine mmiliki wa kiwanja namba 1072 kilichoko Upanga Magharibi jijini Dar es Salaam kinachodaiwa kuwa hakina sifa ya kuwa kiwanja, amedai kuwa waziri Tibaijuka amedanganywa na watendaji wake kuhusu umiliki wa kiwanja hicho.

Paul Anthony aliliambia gazeti hili jana kuwa alipewa ‘ofa’ ya kiwanja hicho na wizara ya Ardhi tangu Januari 24, 1989 na kwamba ameendelea kukilipia kodi hadi leo.

Alisema kiwanja hicho kiko katikati ya viwanja viwili vilivyopimwa vya Salender Bridge Club na uwanja wa shule ya Muntazir lakini, kiwanja chake hakijapimwa hadi leo.

“Mkurugenzi wa Makazi ana ajenda ya siri juu ya kiwanja changu na jana (juzi) alimdanganya Waziri,”alieleza Anthony.

Alisema kabla ya kutakiwa kupewa hati, wizara ilimtaka kwanza atoe maelezo ya tathmini ya athari za mazingira kuhusu Mikoko iliyoko nje ya kiwanja hicho na alifanya hivyo.

Mmiliki huyo alionyesha vielelezo mbalimbali zikiwemo barua zilizoandikwa na J. Kombe kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc) na ile ya Mali Asili na Utalii iliyoandikwa na Dk Tango kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Barua hizo zimeeleza kuwa kiwanja hicho kiko nje ya msitu wa mikoko na kwamba mradi unaotaka kutekelezwa hautakuwa na madhara yasiyoweza kudhibitika.

Barua hizo zilielekeza upimaji wa kiwanja hicho usisitishwe kwa kigezo cha kuharibu mikoko kwani kiwanja chenyewe hakina mikoko.

Alisema pia mchoro wa mipango miji namba 1/504/569 Dar es Salaam Area 2 ambako ndiko kiliko kiwanja chake bado haujaidhinishwa hali inayochangia kuchelewa kupimwa kwa kiwanja hicho.
Juzi Waziri Tibaijuka alitoa siku 30 kwa wananchi waliojenga nyumba kwenye maeneo ya fukwe ya Bahari ya Hindi kuzibomoa kabla ya kuanza kuchukua hatua.

Akizungumza katika ziara ya kukagua hali ya makazi na mipango miji katika jijini la Dar es Salaam jana, Waziri Tibaijuka alisema viwanja vya Serikali vilivyokuwa wazi haviruhusiwi kuwa makazi watu kwa kuwa viwanja hivyo ni kwa ajili ya michezo na bustani za kupumzika wananchi wa maeneo husika.

“Nasikitika kusikia kuwa wananchi wanaoishi hapa wamenunua maeneo haya. Hivi viwanja si vya watu ni vya Serikali na kila aliyenunua anapaswa kubomoa na kurudisha kiwanja kwa wahusika,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema miongoni mwa viwanja hivyo ni eneo la wazi lililopo Ocean Road ambalo lilikuwa linamilikiwa na Shree Hindu Mandal, kiwanja namba 59 kitalu 1 kilichokuwa kinatumika kuchomea maiti mwaka 1952 mpaka 1967 na kuhamishiwa Kijitonyama na kutaka eneo hilo lilirudi mikononi mwa serikali.

Alisema katika hali ya udanganyifu Shree Hindu Mandal waliibuka na kudai mabadiliko ya matumizi ya kiwanja hicho na baadaye kupewa kibali na rais cha kutaka matumizi ya awali yafutwe na msajili alikifuta kwa nyaraka namba 131942 ya Septemba 2 mwaka huu kisha kuagiza manispaa ya Ilala ivunje ukuta uliopo.

Katika eneo jingine lililopo Palm Beach kiwanja namba 1006 ambalo lilikuwa la matumizi ya wazi mwaka 1975 kabla ya kubatilishwa kuwa eneo la mtu binafsi mwaka 2002 na mpaka sasa kinamilikiwa na mtu huyo.

“Mtu hawezi akajenga kwenye eneo la serikali kubwa kama hili wakati wananchi wanaoishi katika maeneo haya hawana sehemu ya kupumzikia wala sehemu ya watoto kucheza. Hii ni hujuma na wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua,” alisema Tibaijuka.

Alisema kiwanja namba 1072 kilichopo eneo la Upanga ambacho ni cha nyongeza, kilibuniwa pasipo kufuata utaratibu. Alisema kiwanja hicho kiko eneo la mikoko na hakijawai kupimwa rasmi.
 
Mimi ndiyo maana nasema tuanze na hwa hawa wapuuzi waogawa ovyo maeneo ya bustani.
Mnawahamisha hamisha kwa nini??
 
Nadhani sasa Profesa, itaijua vizuri CCM- hawa wamiliki ndio watoa michango kwa CCM. Huyu mama afahamu kuwa viwanja vya wazi vyote ni vya mafisadi. Je, ana ubavu na kushidana na CCM - ya mafisadi. Je, mashamba, rachi - atasema nini. Nchi imekwisha.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mmiliki wa kiwanja cha palm beach kinachosemekana ni batili ameamka na kumwambia mh waziri pamoja na kuandika barua na yeye kukataa kukutana nae anamshauri aombe washauri wake mawazo kwani asije juta kuwekeza DOWANS nyingine na kuikuta serikali ikiishia kulipa madeni

Kazi ipo
Mmiliki Palm Beach amvimbia Tibaijuka
Amwonya asisuthubutu kuvunja ukuta
Send to a friend Wednesday, 15 December 2010 20:46 0diggsdigg


prof%20anna%20tibaijuka.jpg
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Nora Damian
MMILIKI wa kiwanja kilicho jirani na hoteli maarufu ya Palm Beach iliyoko jijini Dar es Salaam ambaye Serikali imemtaka abomoe ukuta wake kwa kuwa ni eneo la wazi, ametishia kumshtaki Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akidai kuwa analimiki eneo kihalali.

Mmiliki huyo alikutana jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anakusudia kumshtaki Waziri Tibaijuka kwa kuwa ameidharau Mahakama.
Mmiliki huyo, Taher Muccadam alisema Waziri Tibaijuka amedharau amri ya mahakama kwani alishinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kuendelea na ujenzi katika kiwanja hicho.

... verbalised phraseology. hivi huyu jamaa si yule mwenye kesi mahakamani kwa kujifanya Wakili au? Unajua, ukishazoea vitu feki unachakachua hadi shahada. Kama ndo yeye, basi ana vyeti fake kabisa vya shahada za elimu ya juu. Likewise, mjanjamjanja tu, but then, kama jamaa wengi wanovaa yale mashati ya kijani.
 
nadhani sasa profesa, itaijua vizuri ccm- hawa wamiliki ndio watoa michango kwa ccm. Huyu mama afahamu kuwa viwanja vya wazi vyote ni vya mafisadi. Je, ana ubavu na kushidana na ccm - ya mafisadi. Je, mashamba, rachi - atasema nini. Nchi imekwisha.

labda niwape kifupi

kulikuwa na watu kazaawanagombania hiko kiwanja yule muhindi akamtumia wazir mmoja kuonana na mh rais uwezi amini na hii nawambia itabaki kuwa hivi waliitwa wahusika wakaambiwa huyo ndio mmiliki halali na hata muende chooni huyo bwana ameweka serikali ya kikwete mkononi ndio maana nikaomba hawa mawaziri wawe makini na semi zao zisiwaumbua siku ya kuomba kura..tumeuzwa siku nyingi sana
 
Naona kama sikuzake zinahesabika namshauri asiige wakina MWAKYEMBE WAMEAGA KWAO HAWA
Dar awakuja kutalii muulize Mgufuli wamerusha vingapi sasa kama anataka kusingizia shinikizo la damu sina cha kumshauri
 
labda niwape kifupi

kulikuwa na watu kazaawanagombania hiko kiwanja yule muhindi akamtumia wazir mmoja kuonana na mh rais uwezi amini na hii nawambia itabaki kuwa hivi waliitwa wahusika wakaambiwa huyo ndio mmiliki halali na hata muende chooni huyo bwana ameweka serikali ya kikwete mkononi ndio maana nikaomba hawa mawaziri wawe makini na semi zao zisiwaumbua siku ya kuomba kura..tumeuzwa siku nyingi sana

Ndg mwacheni Prof afanye kazi yake, visiletwe vitisho hapa, ametoa siku therathini wacha waende tena kwa Rais kuzima tuone mwisho wake!! Nchi hii imezidi watu kuishi kwa ujanja ujanja hapo imefika mahali pake.
 
mwacheni ajenge ghorofa 22 asipewe permit za sewage kwa sababu system haitoshi kila mtu anajenga hayo maghorofa infrastructure ya mwaka 47
 
This country will see a new dawn of economic progress only if pragmatism replaces political dogma.

I advise mama yetu Prof. Anna Tibaijuka to follow the pragmatic approach to problems solving as it is often more successful than an idealistic/political one. La sivyo Mafisadi watakupelekesha mama!!!

labda niwape kifupi

kulikuwa na watu kazaawanagombania hiko kiwanja yule muhindi akamtumia wazir mmoja kuonana na mh rais uwezi amini na hii nawambia itabaki kuwa hivi waliitwa wahusika wakaambiwa huyo ndio mmiliki halali na hata muende chooni huyo bwana ameweka serikali ya kikwete mkononi ndio maana nikaomba hawa mawaziri wawe makini na semi zao zisiwaumbua siku ya kuomba kura..tumeuzwa siku nyingi sana
 
Pole sana tibaijuka. Tatizo kubwa ni mfumo kama anavyosema ndugu yangu Kitila.

Dhamira na uwezo ni kweli unayo, lakini je fursa ya kuonesha uwezo wako na kudhihirisha dhamira yako utaipata???

Usipoangalia utachafuka bure kwa kuingizwa mkenge

Hao unaowatolea mikucha ndio waliopambana wenzako wapate pesa waingie madarakani

Bahati nzuri wewe umeingia kwa bei chee.

Hivyo kabla hujapambana nao ni muhimu kujua kwamba nguvu iliyo nyuma yao ni kubwa kuliko uliyonayo.
 
Viwanja vya kutunishiwa misuri wakubwa wanahusika kwa hiyo wakiguswa itakula kwako kuwa makini wahindi sio watu
 
Tibaijuka ataweza tu kufanikiwa ikiwa tu Kiranja namba mmoja atamuunga mkono ,vinginevyo itakuwa nguvu ya soda,kuna watu wasioguswa nchi hii.Vinginevyo jiuzulu ubakie mbunge wa kawaida.
 
hahahaha


yaan jamaa anatunisha msuli namna hiii

Kweli nchi hii ina watu wazembe kabisa!

Hawa wanaodai viwanja reasoning yao ni dhaifu kabisa. Bahati mbaya kabisa kinga pekee wanayoitumia ni uhusiano wao na Rais, waziri fulani, mkurugenzi fulani,n.k..

Mmoja eti anataka kukutana na waziri. Wafanye nini!
Mwingine eti anakilipia tangu 1989! Rubbish. Tusiwashabikie hawa wahuni eti prof. hawawezi.

Waache waendelee kupewa kinga na viongozi lakini ukweli utabaki kwamba hakuna kiwanja. baadaye kinga zao zikiisha ndo kuambiwa jengo chini.

Tatizo kubwa ni watu kupinda sheria. Ukisha pinda sheria usidhani umefanikiwa. Mwekezaji yeyote awe m-TZ au toka nje ya nchi anatakiwa kufahamu kama chochote anachokifanya kiko chini ya sheria au nje ya sheria. Ikiwa nje ya sheria ukapewa, hata kama utasema unakilipia sijui tangu lini, hiyo inachukuliwa kwamba ni udhaifu wako, kutofanya homework yako.
 
Mambo hayo, sinema inaendelea. Mtu anatuna misuri kana kwamba yeye ni waziri mkuu vile! Utamu wa kuchangisha hela za kuchakachulia kura utakutana nao live Prof, na hapo natumai ni mwanzo tu.
Sisi sote tumetenda dhambi, pale palipopitishwa kale ka mnyama Takrima, na wanasiasa hata kama hawana ujasiri wa kuongoza wakang'ang'ania madarakani kwa kupitia tume zisizo huru; ni hapo tu ndipo tulipotenda dhambi. Lakini, siku zinahesabika, tutamnyoa kuku manyoya live, bila hata kumchinja. Nchi hawezi kuendeshwa kigoigoi kabila hii. Naomba kuwakilisha
 
Back
Top Bottom