Kama anatafuta dowans nyingine ajaribu-mmiliki wa palm beach amwambia tibaijuka

Mama T,usikonde wakikuzuia kuchukua hatua sasa wanajenga mazingira ya wananchi kutumia nguvu hapo baadae. Everything and everybody have their limit of elasticity.
 
Wahindi haooo mama umecheza na wahindi? umechezea serikali ya dunia. Be careful maana hata Kikwete hatakuwa upande wako. Take my words.
 
Nadhani sasa Profesa, itaijua vizuri CCM- hawa wamiliki ndio watoa michango kwa CCM. Huyu mama afahamu kuwa viwanja vya wazi vyote ni vya mafisadi. Je, ana ubavu na kushidana na CCM - ya mafisadi. Je, mashamba, rachi - atasema nini. Nchi imekwisha.

Ama, wewe hujui kuwa hata Mbowe anakiwanja kala kilikuwa cha wazi? Sasa na yeye ni mfadhili wa CCM?
 
Mama T, nivizuri ujaribu kuonyesha sikitiko lako la namna nchi ilivyo uzwa. Jitahidi hivyo na uwe ngangari hata kama utapoteza uwaziri wako; mimi nina imani mawaziri wakibadilishwa utatolewa hapo na kupewa wizara nyingine lakini bora iwe hivyo kuliko kuona uozo. Tumia uzoefu wako ulionao kurekebisha hii hali. Tuko pamoja.
 
mmh yaani ukiangalia mkwala ambao umepigwa hapo unabaki unafikiri ubavu kama huo anautoa wapi......nakumbuka enzi zile za baba wa taifa ambapo kuna mzungu alisema kuwa serikali yote ya TZ ameiweka mfukoni, hamna haja ya kukumbusha kilichomtokea.....natumaini huyu jamaa pia ataonyeshwa nani yupo juu......

Nchi inatakiwa iongozwe kwa mujibu wa sheria wala sio kutumia madaraka vibaya au vinginevyo, huyu jamaa ana haki ya kusema aliyoyasema na Waziri pia na haki na mamlaka kama alivyoagiza, lakini ikitokea kuto kukubaliana kuna taratibu za kufuata, sio tukusanyike tukabomoe ukuta, Pia kila jambo na wakati wake, Wakati wa MWL Nyerere sio wakati huu, nadhani mengi tunayoyazungumza kuhusu viongozi na Rais usingethubutu wakati wa Mwalimu hata kama lingekuwa na ukweli.TUTUMIE BUSARA
Pia huyo waziri angeanza maofisi ua ccm yaliyojengwa viwanja vya wazi,,, toa banzi lako kwanza
 
Back
Top Bottom