Kama ana ubavu, afute Mbio za Mwenge!

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Amefuta sherehe nyingi zikiwemo za uhuru na muungano, ila kama ana ubavu au ni mzalendo kama anavyojinadi, afute mbio za Mwenge walau kwa mwaka mmoja ili bajeti hiyo itumike kujenga zahanati katika maeneo ambayo hazipo.
download-32.jpg


download-31.jpg
 
Hivi unaanzaje kuandika kitu kama hiki, mbona Kuna vitu vya muhimu vingi tu? Swali lenyewe ni rhetoric question unauliza ili hali una majibu. Goodluck with your vision endeavor
 
Huo mwenge ni baadhi ya maagano ya kishirikina yanayoifubaza nchi yetu. Nadhani tutakapopata rais aliyezaliwa baada ya uhuru na asiyeamini ushirikina ndio itakuwa mwisho wa huo mwenye. Lakini kama tutaendelea kupata marais wanaoamini ushirikina mwenge utaendelea kuwepo.
 
Hakuna kitu kma mbio za mwenge, hii siku hizi ni kampeni ya CCM. Yani ni mbio za CCm
 

P
 
ibada ya watu hiyo mkuu, wadanganyika wasipofukizwa na moshi wa hiyo kitu wanaweza kuamka na kuanza kudai utawala bora na uwajibikaji, CCM haina uwezo wakuwapa hivyo viwili.
 
Moja ya sababu kubwa ambayo ilimfanya mzee wangu kuachana na CCM ni mbio za mwenge. Hii ni ibada ya miungu kabisa.
 
Moja ya sababu kubwa ambayo ilimfanya mzee wangu kuachana na CCM ni mbio za mwenge. Hii ni ibada ya miungu kabisa.
Nikikumbuka akili za Polepole, Bashiru, Kitila Mkumbo, Mwita, Kafulila nk kabla ya kuunga mkono juhudi na baada ya hapo, napata wasiwasi na KITU GANI HUWAPUMBAZA?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom