Ticktock dork
JF-Expert Member
- Dec 23, 2015
- 466
- 305
amri ya upendo sio amri mpya bali sheria ya mungu imeBASE humoKaka MSEZA MKULU tukianza kufanya rejea za Biblia dhambi ni kitu chochote ambacho kinaenda kinyume na kanuni na taratibu za Uumbaji wa Mungu. (Any act of transgression against the divine law of God).
Ukikumbuka vizuri kabisa Dhambi ilikuwepo duniani hata kabla ya Torati ya Musa pale Mlimani Sinai, hivyo sidhani kutokuwepo kwa Amri Kumi za Mungu Torati kunaweza kufanya Dhambi isiwepo duniani.
MTAZAMO WA KIHISTORIA.
Tukiangalia tokea Uumbaji wa Mungu miaka mingi hata kablya MUSA dhambi ya Kwanza kutendwa ilikuwa ni KIBURI na UASI dhidi ya Mungu ambao alifanya Kerubi Lucifer pamoja na genge lake la Malaika Waovu.
Dhambi ya Pili ilikuwa ni Kiburi tena ambayo waliifanya ADAMU na HAWA katika Bustani ya Edeni baada ya Kula Tunda kwenye mti waliokatazwa na Mungu. Hapa ni lazima Ikumbukwe Mungu ametoa AMRI nyingi kwenye BIBLIA hata kabla ya Maandishi kugundulika. (Alikuwa akisema kwa kinywa Chake)
Dhambi ya tatu ni ile ya Uuji. KAINI alimuonea wivu MDOGO wake baada ya kutoa SADAKA BORA mbele za MUNGU. Hivyo hapa utakuja Kujua kwamba hata kabla ya AMRI KUMI kuwepo MUNGU aliikataa DHAMBI ya UUAJI. Alimwambia KAINI kabisa kwamba "DHAMBI INAKUNYEMELEA MLANGONI INABIDI UISHINDE". Kipindi hiki kulikuwa hakuna maandishi wala SANDUKU LA AGANO.
Unakumbuka Gharika ya NUHU na SODOMA na GOMORA ?
Majanga yote yaliwakumba wanadamu Vizazi Vingi hata kabla ya MUSA na AMRI KUMI.
Hivyo hapa tunakuja kujua kwamba hata kama Amri Kumi hazitakuwepo kufanya kitendo chochote kinachoendana na mapenzi ya Mungu ni Dhambi. Zamani kabla ya Maandishi watu walitumia Oral Tradition.
MTAZAMO WA KITHIOLOJIA
Yesu hakuja kuivunja Torati bali Kuitimiza. Hata yeye Mwenyewe alikiri na kusema "Sijaja Kuivunja Torati bali nimekuja Kuitimiza" tena akazielezea zaidi AMRI KUMI katika Mafunuo Mapya. Mfano Mzuri:
1. Usizini- Yesu akaseme "Mtu anayemwangalia mwanamke kwa kumtamani azini moyoni mwake"
2. Usiabudu Sanamu- Mtume Paulo anasema Kupenda kitu kuliko Mungu ni Ibada ya Sanamu.
3. Heshimu Wazazi- Mtume Paulo anasema Mzee Usimkaripie bali Muonye kwa hekima endapo atakosea.
HITIMISHO:
Hata kama AMRI KUMI hazitakuwepo DHAMBI bado itakuwepo kwasababu ilikuwepo kabla ya kuandikwa kwa hizo AMRI KUMI. (Rejea mifano yangu hapo juu). Japo Biblia inasema bado zipo na zinafanya kazi mpaka leo na kesho.
Mkristo yoyote anayeamini anaweza kubaliana na mimi kwamba BIBLIA ndiyo AMRI KUU inayotumiaka kumuonyesha Mwanadamu ni mambo gani ukifanya MUNGU anaweza kughafirika.
Pia ndani ya BIBLIA kuna AMRI KUU mpya ambayo haikuwepo kwenye AMRI KUMI. Inasema Mpende BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO. Akamalizia na kusema hakuna AMRI KUU KULIKO HIZI. ( Marko 12:30-31)
NB: Ngoja Mkuu nitarudi na kuleta vifungu vya Biblia kuhusiana na yote yaliyosemwa hapo.