MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,752
- 5,497
1: Alipoandika Amri Kumi kwa mara ya kwanza.
2: Musa alipozivunja zile mbao, Mungu Alizirudia tena na kwa mara ya pili.
3: Alipoandika ukutani "Mene mene tekel na pelesi" mbele ya mfalme Belshaza
4: Kwa wanaoamini yesu ni Mungu: Alipoandika chini pale mafarisayo walipotaka kumponda mawe mwanamke mzinzi.
Ukitoa sehemu hizo nne, maandishi yote yaliyobaki yaliandikwa kwa wawakilishi aliowaongoza.
Tanzania hii ili tujue, Umekosea lazima iangaliwe ni sheria au amri gani uliyoivunja vinginevyo hakuna maana ya Mahakama. Tunaambiwa hata kwa Mungu siku ya Mwisho Kutakuwa na Hukumu.
1: Ziliwekwa ndani ya sanduku la agano waliloagizwa na Mungu kuliunda:Kutoka 40:20
2: Ziliandikwa na MUNGU mwenyewe kwa KIDOLE: Kutoka 31:18
3: Zinaitwa sheria za kifalme:Yakobo2:8
4: Tusingeijua dhambi bila hizi:Warumi 7:7,3:20
5: Sio nzito wala mzigo kama wengi wanavyoambiana 1Yohana 5:3
6: Zitawahukumu wanadamu wote:Yakobo 2:10-12
7: Ni safi na hazina pungufu lolote: Zaburi 19:7
1:Zilitengwa kabisa na amri kumi, na kuwekwa nje ya sanduku:Torati 31:26
2:Ziliandikwa na Musa katika Vitabu:2mambo ya nyakati 35:12
KAMA HAITOSHI MBAO HIZI MBILI HAIZKUWAHI KUUNGANISHWA NA MASHERIA MENGINE MENGI WALIOPEWA WAISRAEL. SANDUKU ZILIMWOTUNZWA HIZO SHERIA NYINGINE ZA MAAGIZO ZILIWEKWA KANDO (SHERIA ZA MUSA -Torat Moshe)
Kama hizi zikikubalika kuwa hazifai, na wengine wanakwenda mbali wanasema Yesu alizifuta, Kwao nini maana ya KOSA au DHambi?
REFERENCE: AMRI KUMI ZA MUNGU KWA MUJIBU WA BIBILIA
1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.KUTOKA 20:3
2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini duniani,wala kilich majini chini ya dunia.usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa mimi ,BWANA Mungu wako ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne chawanichukiao,name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.KUTOKA 20:4-6
3. Usilitaje bure jina la BWANA,Mungu wako maana BWANA hata mhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure.KUTOKA 20:7
4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.KUTUKA 20:8-11.
5. Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa BWANA Mungu wako.KUTOKA 20:12
6. Usiue. KUTOKA 20:13
7. Usizini. KUTOKA 20:14
8. Usiibe. KUTOKA 20:15
9. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako. KUTOKA 20:16
10. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake wala cho chote kile alicho nacho jirani yako.