Uchaguzi 2020 Kama Amiri Jeshi Mkuu, tuambie hawa "wasiojulikana" ni akina nani tutakupa kura, mengine tutakusamehe

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Wakuu leo nimekuja na kibwagizo kipya. Kwanza tunaweza kukiri kuwa katika mambo ambayo ni makosa na ambayo hayawezi kuvumilika hata mbele za mwenyewezi Mungu ni kitendo cha mwanadamu kutoa uhai wa mwanadamu mwingine kwa sababu yoyote ile.

Kisa cha Kaini kumuua Abel ni mfano tosha kwa sisi Wakristo kujifunza jinsi ilivyo laana kubwa kama utafanya kitendo hicho. Kwa mujibu wa Neno la Mungu mwenyewe mtu aliyeua mwanadamu mwenzake hulaaniwa pia yeye na uzao wake hadi kizazi cha nne, pili hata ardhi humlaani na kila anapotia mguu muuaji ardhi inamkimbia. Mtu muuaji hubaki kuishi kama hayawani, digidigi.

Rais Magufuli ndiye alikuwa Amir Jeshi Mkuu wa Tanzania kuanzia 2015 hadi 2020. Ktk kipindi hiki nchi ineingia hofu kutokana na vikosi vinayoonekana kuratibu na kutekeleza mauwaji ya wananchi mbali mbali kwa mtindo unaoonekana ni wa kiufundi na utaalam wa hali ya juu.

Kwa mamlaka aliyo nayo Rais kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Taifa yeye Dr John Pombe Magufuli anawajibu wa kutwambia hiki Kikundi kilichoshindikana ni watu gani? Na je, kama kimemshinda kwa muda woote wa miaka mitano kukiteketeza je bado anasifa ya kuwa rais wetu?

Mtu aliyepewa kwa mamlaka ya kikatiba nyenzo zote za vyombo vya ulinzi kwa uchache tu JWTZ, Polisi, TISS n.k na bado ameshindwa ku-organize na kuleta tija kwenye usalama huyu mtu ni mdhaifu sana.

Na kama atatwambia ni akina nani basi tutampa kura. Huu ndio mtihani wetu kwake na sasa ni kipindi cha kampeni ambapo anakutana na raia moja kwa moja. Tunaomba atwambie.

Wapambe wake msaidieni kutufu ulia nani huyu Mtu/ Watu wasiojulikana?
 
Watanzania mwaka huu hawana hamu na mtu asiye na uwezo wa kulinda usalama wa nchi
Halafu alivyo na ujeuri ambao haukuwahi kushuhudiwa na Watanzania, hivi sasa anapita kwa Watanzania hao hao akiwataka wampe tena awamu nyingine bila hata kuwaomba msamaha kuhusu vitendo vya wasiojulikana. Aliapa kuwalinda Watanzania lakini akashindwa na badala yake kwa miaka mitano Watanzania wametekwa, wameteswa na kupotezwa na kikosi hicho cha wasiojulikana! Hakika huyu hana kabisa DNA ya Kitanzania.
 
Halafu alivyo na ujeuri ambao haukuwahi kushuhudiwa na Watanzania, hivi sasa anapita kwa Watanzania hao hao akiwataka wampe tena awamu nyingine bila hata kuwaomba msamaha kuhusu vitendo vya wasiojulikana. Aliapa kuwalinda Watanzania lakini akashindwa na badala yake kwa miaka mitano Watanzania wametekwa, wameteswa na kupotezwa na kikosi hicho cha wasiojulikana! Hakika huyu hana kabisa DNA ya Kitanzania.
Wale waliomsukumiza wanamtesa sana hana jeuri yoyote ya kuwapinga.
 
Yaani vikosi vya jeshi/polisi/usalama vilivyojaa snipers wa kutumia risasi mmoja tu kutawanya ubongo wake waje kutumia risasi 30? Acha dharau kwa majeshi yetu, hata mgambo wa nchi hii hahitaji zaidi ya risasi moja kama wangetaka kumua huyo yuda iskariote.
Hivyo hivyo vikosi unavyosema vineshawakamata wasiojulikana? Ni akina nani?
 
Kuna kauli aliitoa Mama Samia Kwenye mmoja ya mikutano ya Kampeni, Kwa kauli ile utafahamu nani yuko nyuma ya shambulizi lile la aibu.
Shambulizi la uoga. CCM haikwepi lawama.
 
Hili swala upinzani hawajalieleza vizuri kwa umma kwenye kampeni, wawaeleze watanzania kwa undani na jinsi serikali ilivyoshindwa kulinda usalama wa RAIA na Mali zao
 
Yaani vikosi vya jeshi/polisi/usalama vilivyojaa snipers wa kutumia risasi mmoja tu kutawanya ubongo wake waje kutumia risasi 30? Acha dharau kwa majeshi yetu,hata mgambo wa nchi hii hahitaji zaidi ya risasi moja kama wangetaka kumua huyo yuda iskariote.
Acha uwongo wewe Mungu pekee ndo anaeamua Nani aishi Nani asiishi ila syo nyie mlimshindwa Basi Yule Mungu ndo alisema aendelee kuishi ili tujue ujinga wenu mnatumia mabavu na huyo mhutu wenu
 
Acha uwongo wewe Mungu pekee ndo anaeamua Nani aishi Nani asiishi ila syo nyie mlimshindwa Basi Yule Mungu ndo alisema aendelee kuishi ili tujue ujinga wenu mnatumia mabavu na huyo mhutu wenu
Mkuu waliomshambulia Lissu hawawezi kuwa kikosi kilichotumwa na Mkulu,ingekuwa hivyo sidhani Kama kungekuwa na ugumu wowote.
Waliomshambulia Lissu Ni migambo wa Chadema.
 
Back
Top Bottom