ZILLAHENDER MPEMA
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 2,055
- 4,243
Maelezo ya Makonda juu ya njia zitumiwazo na wauza madawa ya kulevya kuyaingiza nchini ukiyatafakari kwa kina yanatupa taswira hasi dhidi ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kukabiliana na uhalifu unaofanyika katika mwambao wa pwani yetu.
Nchi iliyo madhubuti katika masuala ya ulinzi na usalama isingegeuzwa uchochoro,haiwezekani meli ziingie nchini zikiwa na shehena za mapipa yaliyojaa dawa za kulevya,kisha ziyashushe mapipa hayo katika kina kirefu cha mwambao wa pwani yetu,zije zitie nanga na kushusha mizigo nchini na kuondoka,kisha baadae kwa kutumia vyombo vingine,wauza madawa kwa msaada wa GPRS waanze kuzunguka katika pwani yetu,wazamie na kuyaopoa mapipa hayo yenye shehena za madawa,wapakue madawa yao na kuyasafirisha hadi katika himaya zao bila kugundulika na mtu yeyote.
Hekaya hii yenye kuacha mashaka makubwa kwa wasikilizaji,haiwezi kufanyika katika nchi yenye vyombo makini vya ulinzi bila wahusika kukamatwa,vinginevyo tukubaliane tu kwamba biashara hii inahusisha mtandao mpana sana wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kauli ya Makonda inanifanya niamini kuwa kuna udhaifu mkubwa sana katika kusimamia usalama wa nchi,kama maharamia hawa wa madawa ya kulevya wanaweza kujipenyeza nchini,wakaingiza mizigo yao na kuishusha katika kina kirefu cha bahari bila kujulikana,kisha baadae wakaenda kuiopoa mizigo yao bila kujulikana na wakaisafirisha na kuiingiza kwenye ngome zao,je maharamia hao hawawezi kutumia njia hizo hizo wazitumiazo katika kuingiza madawa,wakaingiza silaha na kuzitumia katika mitandao ya kihalifu?
Viko wapi vikosi vyetu vya majini vyenye jukumu la kuzilinda fukwe za pwani yetu dhidi ya wenye nia ovu na Taifa letu?Intelijensia ya vyombo vyetu ipo wapi kiasi cha kushindwa kuzibaini hila hizi na kuweka mitego itakayowezesha kukamatwa kwa meli hizo zinazoingiza shehena ya madawa ya kulevya nchini?Ni meli ngapi zilishawahi kukamatwa zikishusha mapipa hayo yenye shehena ya madawa katika pwani yetu?Doria zetu katika mwambao wa pwani zimekamata mapipa mangapi yaliyotoswa baharini yakiwa na shehena za madawa?
Kama haya yalikuwa yakifanyika katika pwani yetu,na hakuna yeyote aliyewahi kukamatwa zaidi ya kusikiliza simulizi za Makonda,tuna kila sababu ya kuamini kuwa wauzaji wa biashara hii hushirikiana na dola na ndiyo maana majina ya wahusika yapo ikulu na hayajawahi kuchukuliwa hatua yoyote zaidi harakati za sasa za Makonda kukamata na kuita watu wakaripoti polisi kwa mahojiano.
Ikiwa wafanyabiashara hawa hawana mafungamano yoyote na vyombo vyetu,bali kwa weledi wao wameweza kuingiza madawa bila kufahamika,basi Taifa letu lipo shakani,hatupo salama,muda wowote tunaweza kushambuliwa na maadui zetu ikiwa watatumia mbinu za wauza madawa na kujipenyeza nchini.Hivi sarakasi zile za vyombo vya ulinzi zilizokuwa zikifanyika nchi nzima ili kukabiliana na UKUTA,zimeshindwa walau kukamata meli moja yenye shehena ya madawa ikiyashusha baharini?Magari ya maji ya kuwasha,mabomu ya machozi na "kifaru Kipya" cha jeshi kiitwacho MV Dar es Salaam vimeshindwa kutumika kudhibiti waingizaji wa madawa badala yake vipo kwa ajili ya kudhibiti wapinzani wa serikali tu?
Kuwaruhusu viongozi jamii ya Makonda kusimama mbele ya vyombo vya habari na kuieleza dunia mbinu zitumikazo kuingiza madawa nchini ni fedheha kwa nchi yetu,ni kuivua nguo nchi yetu kwa kuuanika udhaifu wetu katika masuala ya ulinzi.Kama kweli alichokisema Makonda ndiyo mbinu zitumikazo kuyaingiza madawa nchini,na vyombo vyetu vimeshindwa kukamatwa walau pipa moja,basi Taifa letu laweza kuwa hatarini zaidi kiusalama kuliko hatari ya madawa ya kulevya,usalama wa nchi yetu umeyumba,muda wowote tunaweza kujikuta tunashambuliwa na maadui zetu toka katikati ya nchi.Hii ni Hatari.