Kama aliyeharibu Uchaguzi Mkuu 2020 nae aliimiliki hii ' laana ' kwanini Wabunge aliowapitisha ' Kimabavu ' laana hii isiwaandame tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza bungeni alipokuwa akiwaonya wabunge kutoleta taarifa za kutambulishwa bungeni waume au wake za watu wakidai ni waume au wake zao, alipokuwa akiongoza kikao cha bunge la bajeti, jijini Dodoma leo. Ndugai amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai waume zao wametambulishwa bungeni kuwa ni waume wa wabunge.

Chanzo: mwananchi_official

Na Wabunge hawa ( wa Kike na wa Kiume ) hawaishii tu Kutenda ( Kufanya ) dhambi hii bali kwa sasa wanalicheza vizuri mno Gitaa la Solo la ' Dally Kimoko ' na hao hao Wake / Waume za Watu ambalo Wanafunzi wa UDOM na CBE walishalizoea tokea Siku nyingi tu.
 
Mkuu unamaanisha wabunge Walianza na wanafunzi na sasa wameamia kwa waume na wake za watu? Lakini pia hili la wanafunzi limezoeleka kiasi cha kutopigiwa kelele?
 
Niliwahi kusema bunge LA 2000-2025 sio tu litakua halina meno Bali litakua halina KICHWA!!! Wajinga hawakunielewa!! Sasa bunge limekuwa na reception!!? Au picnic !!? Kila MTU anaenda hapo!? Bora sababu ya maana
 
Haya ndio madhara ya bunge la chama kimoja.

Katika bunge hili la chama kimoja, wabunge wamekuwa wavivu, yaani wame-relax kias kwamba hawajibidiishi kushughulika na mambo ya jimboni + nchi, hivyo wamekuwa bize kufanya ngono na wake za watu au waume za watu.

Wabunge hawa wangekuwa sirias endapo kungekuwepo wapinzani bungeni kwa ajili ya kukosoana. Tunajua fika, wapinzani walikuwa wanajibidiisha kufuatilia mambo mfano, kusoma nyaraka nyingi, hivyo kuleta ushindani bungeni. Wabunge walikuwa hawapati au wanapata muda kidogo wa kustarehe. Lakini kwa sasa wabunge wame-relax, hivyo kujiingiza kwenye vitendo vya aibu.
 
Back
Top Bottom