Kama akili za Maprofesa wetu ndio zipo hivi, Basi tusahau kuhusu maendeleo

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,129
4,712
KWA UFUPI

Ha
pa anasikika John Heche akisema kuwa, kwa mujibu wa Profesa Palamagamba Kabudi, serikali iliingia mkataba na Kampuni hewa toka Kenya (iliingizwa mkenge) wa ununuzi wa korosho kwa kuwa wawekezaji hao kutoka Kenya walionekana kuwa "Serious" kwa kuwa walikuja na Ndege.

Hivi ni Kweli waziri mzima ambaye ni Profesa (Tena fani ya sheria) anaridhika kabisa na mwekezaji kisa tu huyo mwekezaji amekuja na Ndege??? Kweli??? Ndio maana kazi ya Barrick ilikuwa nyepesi Sana kwa akili za namna hii...

Zaidi fungua link hii

ni nadra kuona mwafrika anamiliki ndege binafsi na inawezekana walikuja na ndege yenye jina la kampuni hivyo mpaka kampuni tena ya kiafrika kufikia hatua ya kuwa na ndege yao binafsi bila shaka ni kampuni serious. Mpaka hapo John Heche alishindwa kumuelewa prof kwamba anamaanisha hivyo.

Sio kila kitu cha kushabikia , jaribu kulipa uzito kila neno linalotoka kinywani mwa mtu hasa mtu huyo akiwa profesa
 
Sawa tumelipa uzito neno la Kabudi, je korosho amenunua huyo Mkenya.?
 
kuingia makubaliano, makubaliano kufanyika na makubaliano kutekelezwa ni mambo matatu tofauti. Mimi ninachoshukuru , nchi yetu imeweza kuepuka kutekelezeka kwa makubaliano ya kitapeli. Tusimlaumu profesa kwa sababu kampuni haijanunua korosho, ila tushukuru kuchelewa kutekelezwa kwa makubaliano tumenusurika.
 
wengine tuna digrii za kukariri tu! kila siku mnatusumbua tu kuwaiteni nyie eti Mh Professor!
Ninakubaliana nawe kuhusu "---mwenye akili za juu---"

Lisiloeleweka ni hao mnaowaita "---Mh Professor".

Pamoja na mtindo wa elimu yao waliyopitia enzi zao ya 'kukariri zaidi ili kufauru mitihani", ni hawa hawa akina 'Kabuti' waliotegemewa kuguswa na "Elimu ya Kujitegemea" kama ilivyokuwa imeainishwa kwa wakati ule, ili elimu hiyo iweze kumfanya mtu awe na uwezo wa kufikiri nje ya kukariri.

Nadhani, kama yalivyokuwa mambo mengi yaliyoasisiwa na "mwenye akili" kutoweza kufanikiwa pamoja na uzuri wake uliokuwa umelengwa, hawa 'Waheshimiwa Professor wakiwa ni sehemu ya kukosa mafanikio hayo.

Hili linanikumbusha wale 'Maprofessor' wa Makinikia ya Acacia!.

Nchi yetu ina vichekesho kweli; lakini tunaumia sisi wenyewe.
 
kuingia makubaliano, makubaliano kufanyika na makubaliano kutekelezwa ni mambo matatu tofauti. Mimi ninachoshukuru , nchi yetu imeweza kuepuka kutekelezeka kwa makubaliano ya kitapeli. Tusimlaumu profesa kwa sababu kampuni haijanunua korosho, ila tushukuru kuchelewa kutekelezwa kwa makubaliano tumenusurika.
Unafahamu kuwa imeshaanza kuharibika?
 
ni nadra kuona mwafrika anamiliki ndege binafsi na inawezekana walikuja na ndege yenye jina la kampuni hivyo mpaka kampuni tena ya kiafrika kufikia hatua ya kuwa na ndege yao binafsi bila shaka ni kampuni serious. Mpaka hapo John Heche alishindwa kumuelewa prof kwamba anamaanisha hivyo.

Sio kila kitu cha kushabikia , jaribu kulipa uzito kila neno linalotoka kinywani mwa mtu hasa mtu huyo akiwa profesa
Wewe ndiye unashabikia upumbavu.
 
kuingia makubaliano, makubaliano kufanyika na makubaliano kutekelezwa ni mambo matatu tofauti. Mimi ninachoshukuru , nchi yetu imeweza kuepuka kutekelezeka kwa makubaliano ya kitapeli. Tusimlaumu profesa kwa sababu kampuni haijanunua korosho, ila tushukuru kuchelewa kutekelezwa kwa makubaliano tumenusurika.
Sasa bila kupindisha maneno, huo ni uzembe wa Hali ya juu kwa kipindi hiki tunachoaminishwa kuwa Kuna "kasi ya Magufuli"
 
KWA UFUPI
Ha
pa anasikika John Heche akisema kuwa, kwa mujibu wa Profesa Palamagamba Kabudi, serikali iliingia mkataba na Kampuni hewa toka Kenya (iliingizwa mkenge) wa ununuzi wa korosho kwa kuwa wawekezaji hao kutoka Kenya walionekana kuwa "Serious" kwa kuwa walikuja na Ndege.
Hivi ni Kweli waziri mzima ambaye ni Profesa (Tena fani ya sheria) anaridhika kabisa na mwekezaji kisa tu huyo mwekezaji amekuja na Ndege??? Kweli??? Ndio maana kazi ya Barrick ilikuwa nyepesi Sana kwa akili za namna hii...
Zaidi fungua link hii

Tanzania ya leo ndege ni kitu kikubwa sana ndiyo sababu tunasimama uwanjani kusubiri kuipokea! Wenzetu wananunua hamsini na hawasimami uwanjani.
 
ni nadra kuona mwafrika anamiliki ndege binafsi na inawezekana walikuja na ndege yenye jina la kampuni hivyo mpaka kampuni tena ya kiafrika kufikia hatua ya kuwa na ndege yao binafsi bila shaka ni kampuni serious. Mpaka hapo John Heche alishindwa kumuelewa prof kwamba anamaanisha hivyo.

Sio kila kitu cha kushabikia , jaribu kulipa uzito kila neno linalotoka kinywani mwa mtu hasa mtu huyo akiwa profesa
Kuja na ndege yenye jina hakumaanishi ni ya kwao. Wale ni matapeli walijipanga vilivyo. Unapoenda kuitapeli serikali nzima yenye maphd na maprofesa kibao lazima ujipange. Hata Everton walipokuja basi la Sabbiby ndio lilibandikwa stika lote likawa na rangi na maandishi ya Everton kiasi kwamba ungedhani limetoka London

Ndege za kukodi zipo mkodishaji ukielewana naye unaweza weka chata yako kwa muda.ukimaliza anabandua kama ilivyokuwa kwa Everton. Hiyo kesi ya akina Kabudi haina tofauti sana na Richmond.

Lakini tukubaliane kitu kimoja kuwa udokta au uprofesa siyo kujua kila kitu. Wao nao ni washamba wakubwa kwenye mambo ambayo hawajabobea. Si kuna phd mmoja alisema Gadaf wa Iraq na Sadam Hussein wa Kuweit!!
 
KWA UFUPI

Ha
pa anasikika John Heche akisema kuwa, kwa mujibu wa Profesa Palamagamba Kabudi, serikali iliingia mkataba na Kampuni hewa toka Kenya (iliingizwa mkenge) wa ununuzi wa korosho kwa kuwa wawekezaji hao kutoka Kenya walionekana kuwa "Serious" kwa kuwa walikuja na Ndege.

Hivi ni Kweli waziri mzima ambaye ni Profesa (Tena fani ya sheria) anaridhika kabisa na mwekezaji kisa tu huyo mwekezaji aja na Ndege??? Kweli??? Ndio maana kazi ya Barrick ilikuwa nyepesi Sana kwa akili za namna hii...

Zaidi fungua link hii

Huyo profesa mkodozi wa macho anachojua ni kumsifia Jiwe tu!
 
Back
Top Bottom