Mtu Mzima
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 394
- 124
Kuna uwezekano mkubwa wa Kalonzo Musyoka kupoteza nafasi yake ya sasa.Hali hii inapata nguvu zaidi kwa vile kwa sasa anaonekana msaliti kwa kambi ya upinzani na iwapo serikali ya sasa itavunjwa kutoa nafasi kwa serikali mpya.Ingawa yeye pia anaweza kupata nafasi katika serikali mpya kutokana na kuwa chama chake kinashika nafasi ya tatu kwa wingi wa wabunge lakini wachambuzi wa mambo wanapata mashaka iwapo atabaki katika nafasi yake ya sasa.
Iwapo atapata 'demotion' kuwa waziri wa kawaida au naibu itamuweka katika wakati mgumu sana kisiasa.Kutokna na kamati ya anani kupewa kila baraka na mataifa makubwa na jamii ya kimataifa.Jambo jingine linalompa wakati mgumu ni uamzi wake wa kujiunga na serikali ya Kibaki,ikimaanisha kwamba chama chake hakina uwakilishi kwenye mazungumzo ya sasa kwa vile yeye pia anawakilishwa na kamati ya PNU na atalazimika kukubali chochote kitakachofikiwa huko kwa kuwa yeye ni sehemu ya serikali.
Kwa vyovyote vile matokeo ya majadiliano ya serikali ya mseto yanaweza kuwa mwiba kwa Kilonzo na kuzima ndoto zake kabisa.
Jambo hili linapata msukumo kwa kuzingatia ukweli kwamba Raila Odinga hawezi kukubali kufanya kazi chini ya Kalonzo.
Tunasubiri kwa shauku matokeo ya mazungumzo yanayoendelea chini ya Anani siku chache zijazo ili tupate sura halisi ya jinamizi linalomnyemelea ndugu Kilonzo.