Kaliua, Tabora: Suala la Mwalimu Johari Jumanne aliyedaiwa kupigwa na Mwalimu Mkuu kwa kuchelewa Shule lachukua sura Mpya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
IMG-20210213-WA0023.jpg

Mwalimu Johari Jumanne wa Shule ya Msingi Lufukutwa Iliyopo Kaliua Tabora, amelalamika kupigwa na Mwalimu wake Mkuu anayefahamika kwa jina la Africa Kitinya. Johari amedai alipigwa sababu ya kuchelewa na inaonekana Mwalimu Mkuu huyo alipewa maelekezo na Afisa Elimu amnyanyase kwani wamekuwa hawana Maelewano. Amedai yeye kosa kidogo anaadhibiwa lakini Walimu wenzake hawafanyiwi hivyo.

"Ilikuwa Tarehe 28 Januari, nlichelewa kufika Shuleni kwani nlifika saa moja na dakika hamsini na tano Asubuhi, Walimu tunatakiwa kufika saa moja na nusu hadi saa moja dakika 45 Asubuhi. Kilichosababisha nichelewe ni Mgonjwa wa Nyumbani ambaye namhudumia kabla ya kuondoka. Lakini kabla ya kuingia darasani nikaitwa kwa Mwalimu Mkuu na akaanza kunitukana huku ananifokea Kwanini nimechelewa. Nikamuuliza wewe una Mamlaka gani ya kunitukana sababu nimechelewa na nimeshakwambia nauguza? Na kila siku unaniambia kwamba nilishawahi kuwa kiongozi ni mfano gani natoa.

Nikamwambia nilikuwa Kiongozi niliongoza kwa muda wangu na wewe unaongoza kwa muda wako. Mimi kuwa Kiongozi inahusiana nini na mimi kuchelewa? Ndipo nikaanza kupigwa kama mtoto mdogo ikabidi nitoke nje. Walimu wakaja kuamulia na watoto wakajaa nje, ilikuwa ni aibu kupigwa mbele ya Watoto” Mwalimu Johari anaeleza

Baada ya tukio hilo kwakuwa alikuwa kaumizwa, alienda Polisi kutoa Taarifa na akapewa PF3 aende Hospitali.

Mwalimu Mkuu akana kumpiga
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lufukutwa, Ndugu Africa Kitinya, amekana kumpiga Johari. Amesema siku hiyo alimuita kumuuliza kwanini amechelewa na kumpa majukumu ya Siku, lakini Johari akwa Mkali na kuanza kumtukana. Mwalimu Kitinya Kasema imekuwa tabia yake kuchelewa na ukimuuliza anajibu kwa jeuri.

"Niliona kawa mkali, nikatoka nje na kusimama chini ya mti, lakini yeye akaendelea kuongea kwa sauti hadi akazua taharuki kwa Waalimu na Wanafunzi kwani alikuwa anatukana. Ikabidi niende kumtoa Ofisini kwangu nikamsukuma nje. Baada ya hapo akaenda kutoa taarifa Polisi.”

Mwalimu Kitinya ameongeza Kwamba aliona pale Shule halii, lakini alipokaribia Polisi akaanza kulia kwa sauti.

“Polisi walinikamata na kuniweka ndani bila kunisikiliza, Walisikiliza Upande mmoja. Nimekaa Mahabusu kuanzia saa tano hadi Saa kumi na moja, nilikasirika sana” ameongeza Mwalimu Africa Kitinya.

Mwalimu Johari anena tena
Mwalimu Johari akaulizwa: Kwanini Umedai Afisa Elimu wa Wilaya ndo kasababisha Upigwe? Akajibu kwamba ana Ugomvi na Martin Mahinda(Afisa Elimu Wilaya) hata kumpeleka kwenye hiyo Shule alifanya hivyo ili kumukomoa.

"Ndugu Mwandishi Mimi nilishakuwa Mwalimu Mkuu kwenye hii Shule, baada ya kufanya vizuri wakani-promote kupelekwa Halmashauri ya Kaliua kuwa Afisa Elimu wa Vifaa na Takwimu. Nimekaimu kwa Miaka Mitatu. Nilipokuwa Mwalimu Mkuu, niliitoa shule kwenye ufaulu wa 57% nikaipeleka kwenye ufaulu wa 90% ndipo Viongozi wakaniona. Kipindi hicho wakati nafanya kazi nilikuwa chini ya Mkurugenzi Dk. Athumani Kihamia ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo, pia nikafanya kazi na Mkurugenzi John Pima (sasa ni Mkurugenzi Arusha Jiji). Na Afisa Elimu Wakati huo alikuwa Fravian Nchimbi ambaye Kastaafu na kumleta huyu hapa Martin Mahinda. Lakini huyu DEO (Afisa Elimu wa Wilaya) Mpya alipokuja akinirudisha huku nilipokuwa Mwalimu Mkuu kuwa Mwalimu wa kawaida" alisema Mwalimu Johari.

Rushwa ya ngono yahusishwa
Anaongeza: “Sababu kubwa ya kunifanyia hivi, ni kwa sababu nilimkataa Kimapenzi. DEO mpya alipokuja akanitaka kimahusiano ili aweze kumuandikia barua Katibu Mkuu TAMISEMI ili promotion yangu ikubalike ila sikuwa na ridhaa ya kufanya naye Mapenzi. Akanitishia kuniondoa na akasema nikiwa chini ya Utawala wake nitanyooka. Mwisho wa siku kweli akaniondoa kwasababu aliyoitoa kwamba sina barua ya Utambulisho kutoka kwa Katibu Mkuu TAMISEMI." alidai Johari.

Johari amedai aliwenda Kutoa taarifa TAKUKURU kuhusu kuombwa rushwa ngono akaambiwa apeleke Ushahidi, vinginevyo hamna jinsi ya kumsaidia ndio akakwama.

Johari alidai alimuomba DEO ampangie Shule nyingine tofauti na hii aliyokuwepo awali, akaambiwa aandike barua.

"Nikaandika barua, akakataa kunibadilishia Kituo kwa sababu sikusaini hiyo barua, hakutaka niende kusaini hiyo barua wala niandike nyingine ndiyo maana hadi leo nipo hapa.”

Afisa Elimu wa Wilaya akana
Afisa Elimu wa Wilaya(DEO) amekana kuhusika kwa namna yoyote iwe kumuandikia barua ya kupromote au kimshusha cheo.

Amesema hajui lolote kuhusu kumtaka kingono kwani hajawahi kuitwa wala kuhojiwa na TAKUKURU na kuwa ndo kwanza anasikia leo hayo masuala ya rushwa ya ngono.

Amehoji kwanini mwathirika akimbilie TAKUKURU na asiende kwa Mwaajiri wake?

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI aahidi haki kutendeka
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu, Ndugu Gerald Geofrey amesema hilo suala halijafika kwake, akasema analifuatilia kwa haraka sana na atahakikisha Mwalimu Johari anapata haki zake sitahili.

====



Huyo Afisa Elimu pia hata mimi kwa mwaka Ulioisha baada ya kutoka masomoni alimlazimisha Mwalimu mkuu Kupitia kwa Afisa Elimu Kata tuombe kuhamishwa kituo ili tupewe Uwalimu mkuu kinyume na Taratibu za kazi pale unapoamua Kumpa mtumishi PROMOTION yake.

Kwa kifupi Mahinda hafai kuongoza Walimu ni mnyonyaji wa haki za Walimu wilaya ya kaliua na Usahidi wa huo ujinga pia Upo.



Huo ndio ukweli ndugu kama shida ni barua toka Wizarani mbona kuna Jamaa Aliachwa pale Wilayani na % kubwa walioondolewa ni wanawake akiwemo huyo Johari na Mdada mmoja Alikuwa Afisa elimu Taaluma no 2 akiitwa Magreth.....

Ni wazi huyo Afisa ana huo ujinga.

Pia soma;

 
Kwa akili ya kawaida tu huyo mama kama alipandishwa cheo akakaimu kwa muda, kumrudisha kwenye shule aliyoondoka akiwa mkuu halafu anarudi kama mwalimu wa kawaida ni ukosefu wa busara, labda kama angekua ameharibu.

Ndio maana wakuu wa taasisi ama idara wakiondolewa wanahamishwa kwani eneo walipokua wakuu wana loyal fans wao, itamletea mkuu mpya kazi ngumu iwapo atafanya kazi pamoja na mkuu wa zamani.

Huyo afisa elimu hana akili.
 
Unapigwa na mtu anaitwa Africa, just itamke 'Africa' unathubutu vipi kumuanzishia mtiti mtu ana jina kama hili?

Hawa watu wenye majina ya kipekee hua hawapendi kushindwa battle atakushtakia hata kwa Mungu au mungu.

Waandishi wameshindwa hata kuuliza kama kweli alikua mkuu na amerudishwa kama mwalimu wa kawaida kwa vigezo gani.

Mchunguzi anaenda kuchunguza huku anaahidi "Johari atapata haki yake"

Hebu picha ya Johari.
 
Inasikitisha, rushwa ya ngono ipo sana, Johari atakuwa mkweli. Hivi TAKUKURU walitaka abakwe? Hivi hawawezi kutumia njia zao za kiitelijensia kubaini badala ya kusubiri ushahidi?

Rais Magufuli kazi ipo, Mh. Kafo wizara yako ina kasoro. Katibu mkuu enzi zile Sagin alikula rushwa kupandisha watu vyeo, leo rushwa ya ngono bado ipo. So sad
 
Back
Top Bottom