Kali Ya Karne: Mlinzi wa Getini amuomba rushwa Rais Uhuru Kenyatta ili amruhusu kutembelea bustani ya taifa nchini Kenya

Habari Wana Kijiji,

Leo katika pita pita za kusoma habari mitandaoni, nimekutana na kali ya karne katika bara zima la Africa. Kenya wamevunja rekodi ya Rushwa katika bara la Africa (Kama Sio Duniani Kwa Ujumla).

Nirudi kwenye mada husika,

Siku za hivi karibuni, Rais Uhuru Kenyatta alikwenda kutembelea Bustani ya Uhuru (Uhuru Gardens) bila ya kutoa taarifa kwa mtu yoyote kwamba anakwenda huko. Alitumia gari binafsi ili mtu yoyote asijue kwamba Rais anakwenda na alikua maeneo yale.

Mara baada ya kufika getini, mlinzi aliokuwepo lindoni kwa wakati huo alizuia lile gari lisiingie ndani ya bustani, bila kujua kwamba aliomo ndani ya gari hilo ni Rais Kenyatta mlinzi aliomba rushwa ili aliruhusu lile gari kuingia ndani ya bustani.

Cha kushangaza zaidi, Rais Uhuru Kenyatta hakua na hila wala gubu, alizamisha mkono mfukoni na kutoa kiasi cha fedha na kumpa yule mlinzi. Mara baada ya kupokea zile hela, mlinzi aliliruhusu lile gari la Rais Uhuru kuingia ndani ya bustani na kulielekeza mahala pa kulipaki gari, huku akimuahidi kwamba usalama wa gari utakua vizuri.

Kama ilivyo ripotiwa na chombo cha habari cha The Star, haikujulikana nini kilimpata mlinzi yule mara baada ya kuomba na kupokea rushwa kwa Rais wa Nchi.

rip mlinzi
 
There was mwana biashara in dar slum he had issues with TRA,
Magufuli alidai na kuwamuru tra walipe fidiya mwana biashara huyo.
To date he has not been payed hata centi moja.
Rushwa ya kufa mtu, au sio???
 
Wewe unasema kavunja rekodi umesahau yule mzee mmoja Nshomile kutoka kule Bukoba alimtapeli raisi Nyerere matofali na tena akijua kabisa ni raisi wa nchi.Raisi Nyerere wa watu hakumfanya lolote nani anajua jina lake atuambie.Watu kama hawa ni adimu sana kupatikana wanatakiwa wapewe ulinzi na nishani ya ujasiri
2.Mme msahau yule mwalimu mkuu wa shule flani sijui alikuwa anaitwa Kamuzora mtoto wa Nyerere alifanya kosa shule akamuambia namuhitaji baba yako.Mkuu wa mkoa akatumwa akasuluhishe akakataliwa mwalimu akasema baba yake huyu namfahamu ndio namuhitaji wakaenda wazee mbali mbali aliwakataa hadi mzee Nyerere akaenda mwenyewe na landrover yake.Mwalimu akasema nilikuwa najua wewe ndio baba yake ndio nilikuwa nakuhitaji.Nyerere akachukua kiboko kengele ikapigwa akamchapa mwanaye mbele ya wanafunzi wenzake.Mwalimu Nyerere alivorudi dar baada ya muda akamteua yule mwalimu mkuu kuwa mkurugenzi wa National Milling.
Alikua anaitwa Batenga, alikua tapeli wa kimataifa.
 
Alikua anaitwa Batenga, alikua tapeli wa kimataifa.
kwani nshomile mna shida gani, au kusoma kwingi manake hata ukienda posta watengeneza mihuri feki na wapiga saini za watu feki ni nshomile, na wanavalia suruali kifuani. kiingereza kingiii.
 
Dah! Kwa namna ulivyowasilisha kwa mihemko nikadhani jamaa aliagiza rushwa akijua fika ni rais, kumbe mlinzi alijua zali la kawaida ila ikawa ndio zake za arobaini. Haya ni matukio ya kawaida sana Afrika, nakumbuka hata Tanzania marehemu rais Magufuli aliwahi kuhalalisha kwa kusema wawe wanapewa hela ya rangi ya viatu.

Afrika ni usen.ge wa kijinga sana, yaani maaskari wanaomba rushwa kwenye kila kitu, ukiibiwa mtaani inabidi upambane na hali yako maana ukienda kushtaki, pale eti askari watoke kwa defenda kuja mtaani kukusaidia lazima uchomoe noti kadhaa, wakati Ulaya unapiga 911 magari ya mapolisi yanakusanyka kwako mlangoni zaidi ya balaa.

Tatizo la rushwa limekithiri sana nchi hii, sema ni aibu kwa Mtanzania kuchekelea wakati nawafahamu sana kwenu huko......hamna utofauti wowote hovyo bin hoi.
Watanganyika makajanja wana mini kwa makanjanja ni kazi kama nyingine ila sheria na dola ni uthi.
 
Back
Top Bottom