Agrila Farming
Member
- Mar 3, 2018
- 64
- 53
Ni ukweli usiopingika kwamba kupata faida katika kilimo kwa kufanya kilimo biashara kuna hitaji mambo mengi sana lakini katika vitu muhimu zaidi ni timing ya soko kwa zao husika.Wakulima wengi katika nchi yetu wamekuwa wakikata tamaa kuendelea na kilimo kutokana na hasara wanayoipata katika kilimo na kitu kikubwa kinacho changia hili ni ukosefu wa taarifa sahihi,sio tu taarifa sahihi za mbegu zipi ni bora kwa kilimo au ni udongo upi ni bora kwa kilimo cha zao fulani bali ni muda gani muafaka huwa na bei nzuri kwa zao fulani.Kilimo biashara kimejikita zaidi katika utaalamu unaotumika katika shughuli nzima za kilimo lakini masoko mazuri ni jambo la kuzingatia kabla hata hujaanza kilimo.
Kutokana na changamoto inayowakumba wakulima kutofahamu ni muda gani nizalishe nini ili nipate soko zuri la zao husika basi tumekuja na KALENDA YA MASOKO KWA BAADHI YA MAZAO TANZANIA yenye mazao tofauti tofauti.
Kalenda hii inaonesha ni mwezi gani zao fulani hua na bei nzuri hivyo basi mkulima anachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha kipindi hicho ndicho anachopaswa kuvuna zao husika ili aweze kupata faida nzuri kwenye kilimo.kipindi ambacho zao husika huwa na soko zuri kimeoneshwa kwa rangi tofauti tofauti lakini kikubwa ni kwamba kipndi ambacho hakijaoneshwa kwenye kalenda hii basi ni kipindi ambacho zao hilo huwa na bei ndogo inayopelekea mkulima kupata hasara.Kiuhalisa ni kwamba katika vipindi hivi ambavyo masoko huwa mazuri kwa zao husika huwa kunakuwa na changamoto kubwa kuzalisha zao hilo moja wapo ikiwa ukame lakini ni vyema ukatafuta njia mbadala za kupambana na changamoto hizo upate faida nzuri kuliko kusubiria msimu wake na kuishia kuuza mazao kwa hasara.Kwa maswali na maelezo juu ya kalenda hii unaweza ukacomment swali lako na ukajibiwa hapa.Tuache kulima kwa kufata mkumbo kilimo kinalipa.-Agrila Farming