Kalemani: Zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,337
TANZANIA :- MAJI YA KUFUA UMEME JNHPP KUJAZWA NOVEMBA 2021

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 21 Februari, 2021 katika ziara yake kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere megawati 2115, amesema zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021.

Dkt. Kalemani amewaomba wadau mbalimbali hususani viongozi kuhakisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuweza kupata maji ya kutosha.

Akitoa wito kwa wananchi wote wanao lima maeneo ambapo kunavyanzo vya maji, Dkt. Kalemani amewaomba walime kilimo ambacho hakitaleta athari ya upatikanaji wa maji katika bwawa la Julius Nyerere, yatakayo tumika kuzalisha Megawati 2115.

Aidha, katika ziara hiyo ameagiza ufanisi wa kusimamia Mkandarasi usiku na mchana ili kuhakikisha anamaliza mradi kwa wakati.

"Mkandarasi ni lazima aongeze wafanyakazi na vifaa vyote vilivyo bandarini hakikisheni vinafika kwenye mradi na kufungwa kwa wakati".
 
Dkt. Kalemani amewaomba wadau mbalimbali hususani viongozi kuhakisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuweza kupata maji ya kutosha.

Akitoa wito kwa wananchi wote wanao lima maeneo ambapo kunavyanzo vya maji, Dkt. Kalemani amewaomba walime kilimo ambacho hakitaleta athari ya upatikanaji wa maji katika bwawa la Julius Nyerere, yatakayo tumika kuzalisha Megawati 2115.
Naafikiana na Kalemani, serikali inatakiwa kuweka mikakati ya uhakika katika kulinda vyanzo vya maji na hususani kule nyanda za juu kusini mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa ambako ukataji bila upandaji wa miti umeanza kutamalaki, ujenzi wa makazi unakwenda mpaka kwenye vyanzo vya maji na hakuna hatua zinachukuliwa dhidi ya wahusika.

Nashauri ingeanzishwa project maalumu huko nyanda za juu maalumu kwa kutunza mazingira ya vyanzo vya maji kama ilivyokuwa HIMA miaka ya 1990s, na ikibidi maeneo hayo wapelekewe bomba la gas watumie gas ili waachane na matumizi ya kuni na mkaa
 
Kalemani tumemzoea kuwa ni Waziri anayependa kuongea kama wasanii wa bongo movie. Yeye alimradi apigwe picha na atokee kwenye TV.

Siamini kuwa STIGLERS gorge power project itakuwa imefikia hapo. Sioni tukipata umeme huo hata 2025, na hili Meko analijuwa na ndiyo maana kauli za kutaka kuongeza muda wa utawala zinapoanzia.
Maneno haya mliyatoa hata kwenye standard gauge mlikuwa hamuamini kama mataruma mngeyaona Leo yameweka mnaanza kuhamisha magoli,kukubali mazuri yafanywayo na serikali hii hakukuondolei utu wako wala uwezo wa kufikiri,na ukiwa kijana wa ufipa haikufanyi ubongo agande upoteze uwezo wa kuona na kuchanganua mambo.
 
Unaanzaje kujaza maji kabla mahandaki hayajakamilika?
 
Maneno haya mliyatoa hata kwenye standard gauge mlikuwa hamuamini kama mataruma mngeyaona Leo yameweka mnaanza kuhamisha magoli,kukubali mazuri yafanywayo na serikali hii hakukuondolei utu wako wala uwezo wa kufikiri,na ukiwa kijana wa ufipa haikufanyi ubongo agande upoteze uwezo wa kuona na kuchanganua mambo.
Kumbe SGR ishaanza kazi? Ngoja nikawahi tiketi nisogee zangu hapo Moro fasta. Viva Magu viva...
 
Back
Top Bottom