Kalemani: Wawekezaji wafunge migodi kama hawapati faida

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Naibu waziri wa nishati na madini Medard Kalemani amewataka wawekezaji wafunge migodi yao kama wanaona hawapati faida na kushindwa kulipa kodi
Pia amewataka TRA kupita kwenye migodi yote ya mafuta na madini ili kuhakikisha wawekezaji wote wanalipa kodi

Huyo alikuwa mwanasheria wa wizara hiyo kwa zaidi ya miaka 20,waliowahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo karibu wote wamepata misukosuko na wamehusishwa na ubadhirifu uliofanywa katika sekta ya nishati na madini,yeye hakuna aliyethubutu kuligusa hata pindo la vazi lake.

Kamishna wa madini ametumbuliwa lakini kigogo huyo wa kitengo cha sheria hajawahi kuguswa!Tunapojitoa ufahamu kujiona tunapambana na wahujumu uchumi huku tukichagua yupi wa kumuwajibisha na kuwaacha walio upande wetu ni dalili za wazi kuwa yote tunayoyatamka yanasukumwa na "muwashowasho" wa chuki na hila,siraha ya maangamizi ya mafisadi haipaswi kuwa na macho,ukiona siraha imemtambua mtoto wa nyumbani,tambua mrenga shabaha ni mnafiki na ana muwashowasho.
 
Anajua yeye,mkewe,na watoto wake wanalishwa na serikali,ameshiba sana,hajui kuna watanzania wameajiriwa migodini,hasemi waende wapi

Na yeye mwenywe ndio tatizo,amelala usingizi wizarani wakati almasi inasafirishwa

Amekuwa wizara ya madini kama mwanasheria kwa miaka zaidi ya 20,ni huyu ambaye anajua mikataba ya madini na pengine alihusika

Huyu ni tatizo naye,atoke hapo wizarani,huwezi kukaa kwenye wizara chafu kwa miaka 20,uwe safi
 
Muhongo alifukuzwa uwaziri kwa sababu ya ripoti ya makinikia,kamuachia wizara Medard kalemani,imekamatwa amalsi kalemani akiwa mkuu wa wizara, mbona hafukuzwi?

Hii haki ina angalia sura? Maana lazima vikao vya wizara vikiongozwa na kalemani vilikaa vikajadili suala la mwadui na almasi

Huyu ni mtu wa kutilia shaka sana
 
Atoke aende wapi? Nyumbani kwa mjomba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anawashwawashwa na ndio maana anaongea kama aliyevimbiwa, upo wizarani kwa miaka ishirin halafu unakuja kuongea pumba kweli nchi hii ni vigumu kuielewa
 
Muhongo alifukuzwa uwaziri kwa sababu ya ripoti ya makinikia,kamuachia wizara Medard kalemani,imekamatwa amalsi kalemani akiwa mkuu wa wizara, mbona hafukuzwi?

Hii haki ina angalia sura? Maana lazima vikao vya wizara vikiongozwa na kalemani vilikaa vikajadili suala la mwadui na almasi

Huyu ni mtu wa kutilia shaka sana
Huu ndio ukweli wenyewe na report za kamati zote hazijamtaja kwa ushiriki wake kama mwanasheria wa wizara
 
Nchi inaendeshwa kwa kiki sasa naye anataka sifa za kijinga, anajua kilichoandikwa kwenye hiyo mikataba anataka kutulea makesi mengine ya kulipa fidia, mwaka huu tutakoma mbona
 
Naibu waziri wa nishati na madini Medard Kalemani amewataka wawekezaji wafunge migodi yao kama wanaona hawapati faida na kushindwa kulipa kodi
Pia amewataka TRA kupita kwenye migodi yote ya mafuta na madini ili kuhakikisha wawekezaji wote wanalipa kodi

Wanyumbani ameibuka toka shimoni kweli tutaona mengi,amekua mwanasheria hpo wizarani muda mbna hakutoa ushauri kwenye mikataba leo hii anakuja kubwelabwela kma lusinde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhongo alifukuzwa uwaziri kwa sababu ya ripoti ya makinikia,kamuachia wizara Medard kalemani,imekamatwa amalsi kalemani akiwa mkuu wa wizara, mbona hafukuzwi?

Hii haki ina angalia sura? Maana lazima vikao vya wizara vikiongozwa na kalemani vilikaa vikajadili suala la mwadui na almasi

Huyu ni mtu wa kutilia shaka sana
alipndikizw upande wa maadui...
 
Back
Top Bottom