Kalemani huu sio ufisadi kwa kujenga ofisi ya TANESCO ya mabilioni katika Kijiji cha Chato, kubwa kuliko ofisi yoyote Kanda ya Ziwa na Kati?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,959
20,529
Hii ni Ofisi ya Tanesco iliyojengwa kwenye kijiji (wao wanaita wilaya) ya Chato, ni kubwa kuliko ofisi yoyote katika mikoa ya kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati,Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini.

Tanesco ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Dk. Kalemani, wateja wa umeme Chato wakifika elfu tano ni bahati sana, ofisi hiyo ni kubwa kuliko hata ya Tanesco jiji la Mwanza ambako kuna mamilioni ya wateja

Mh. Samia,asante kwa kumuondoa Kalemani, huu ni ufisadi.

IMG-20210917-WA0003.jpg
 
Hii ni Ofisi ya Tanesco iliyojengwa kwenye kijiji (wao wanaita wilaya) ya Chato, ni kubwa kuliko ofisi yoyote katika mikoa ya kanda ya ziwa, kanda ya kati,kaskazini na nyanda za juu kusini. Tanesco ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Dk. Kalemani, wateja was umeme chato wakifika elfu tano ni bahati sana, ofisi hiyo ni kubwa kuliko hata ya Tanesco jiji LA mwanza ambako kuna mamilioni ya wateja

Mh. Samia,asante kwa kumuondoa Kalemani, huu ni ufisadiView attachment 1941428
Kosa moja humuondolea mtu mazuri yake. Tanzania tulikuwa na utaratibu tuliojiwekea wa kujenga maofisi ya Umaa kutokana na hadhi ya mji kimamlaka.
 
Hii ni Ofisi ya Tanesco iliyojengwa kwenye kijiji (wao wanaita wilaya) ya Chato, ni kubwa kuliko ofisi yoyote katika mikoa ya kanda ya ziwa, kanda ya kati,kaskazini na nyanda za juu kusini. Tanesco ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Dk. Kalemani, wateja was umeme chato wakifika elfu tano ni bahati sana, ofisi hiyo ni kubwa kuliko hata ya Tanesco jiji LA mwanza ambako kuna mamilioni ya wateja

Mh. Samia,asante kwa kumuondoa Kalemani, huu ni ufisadiView attachment 1941428
Hawa Sukuma Gang walikuwa na ajenda chafu na mbaya dhidi ya nchi hii.

Yasirudiwe tena makosa yaliyofanyika mpaka nchi kuingizwa mkenge kiasi hiki.

Hawa watu wa Chato wanapaswa kutengwa na plan za maendeleo mpaka tugawe mkate sawa na mikoa ya kusini kwanza at least kwa miaka 10 watu wa Chato watengwe kama Nyerere alivyoitenga mikoa ya Singida na Tabora enzi hizo.
 
Walipata madaraka makubwa wakawa na vipaumbele vya kijinga hivi huko chato mahitaji Yao yalikuwa ofisi kubwa ya Tanesco?
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
Kwa Siasa na vipaumbele vyao vya hovyo vilivyozingatia upendeleo na kumpendezesha Mwendazake wakashindwa kuangalia uhalisia wa mahitaji. Jengo kubwa Kama hilo lilipaswa kujengwa kwenye miji ambayo Tanesco ina wafanyakazi wengi ambao wanaohitaji office space nyingi na kubwa. Na nature ya kazi za Tanesco haiitaji Jengo lenye office nyingi kama hizo na hasa kwenye makao ya wilaya.

Hapo wanaenda kuongeza operational costs tu ndani ya shirika. Hakuna investment yoyote itakayorudisha faida kwa Tanesco toka kwenye Hilo jengo.

Heko Mama Samia kwa kututolea huyu Waziri.
 
Back
Top Bottom