Kalemani/ Byabato anzeni na Meneja wa TANESCO mkoa wa Dar es Salaam

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,892
22,649
Mh.waziri nilimsikia juzi Mh. Rais akikutaja wakati akikuapisha kwamba unakimbia maamuzi na kuyakwepakwepa lakini nikutie moyo kuwa bado wizarani kwa maksudi naomba usome hapa.

Sisi wakazi wa jiji la Dar hususani tunaohudumiwa na kituo cha Kibamba kama sub-zone ya mkoa tumechoka tena tumechoka kukatiwa umeme kila siku kama vile kuna mgao, tumeunguziwa vitu maana anayekata ni kama anachezea switch vile kila siku kama jana.

Maeneo ya Mbezi Louis, Makabe, Kibamba, Msingwa, Temboni hadi Kimara ni kero tupu kila siku. Tumesema sana tumetoa sana taarifa tumepiga sana simu makao lakini mchezo ni ule ule tu hakuna anayejali.

Tunaomba kuwa pamoja na kuchelewa kutoa maaamuzi ila hili jitahidini maana tangu Oktoba umeme umekuwa kitu cha anasa.

USSR
 
Akimalizana na huyo amgeukie Manager wa TANESCO wilaya ya Ukerewe. Tangu juzi usiku wilaya nzima ipo gizani ndo wamemaliza kuuleta saa moja hii ya jioni.

Yaani siku mbili mfululizo wilaya haikuwa na umeme Kiasi kwamba shughuli zote zinazotegemea nishati ya umeme zilikwama na kufanya watu washindwe kuzalisha na kujiingizia kipato.

Kinachosikitisha ni hili tatizo kujirudia mara kwa mara bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. Hii ni ishara ya uzembe fulani inabidi wahusika wawajibishwe.
 
Kabla hajaondoka DSM, Mh Waziri KALEMANI tunaomba amalizane na Manager wa kituo cha TABATA - LIWITI.

WANANCHI wa mtaa wa BONYOKWA- MACEDONIA tulipeleka kero tangu mwezi August 2020 kabla hata JPM hajaanza kampeni, lakini wanatuona 'mazwazwa' tu. Almost kila baada ya two wks tunawakumbushia kwa simu na kwenda ofisini kwao but wanajishebedua tu na kutoa majibu hewa.

Mh Kalemani, mkuu JPM amesema anaoreserve wengi sana, so kabla hawajakuharibia, fuatilia uondoe uozo wa TANESCO TABATA- LIWITI.

Malalamiko ya tangu Aug hadi leo Nov 2020. So shameful kwao..
 
Nzega napo, wakati nasoma huu uzi wamekata nao nasikia ni kawaida yao kila siku ni lazima wakate,ila Tanesco mmezidi kukata Umeme sijui shida ni nini?
 
Duuh Nashukuru Mungu tatizo la Umeme hapa nilipo limegeuka historia tangu awamu hii ianze hata hapo kabla hawakuwa wanakata Sana.

Ila kwa kiasi kikubwa majenereta hayangurumi Sana kama hapo awali. Hali ilitisha Sana.
 
Duuh Nashukuru Mungu tatizo la Umeme hapa nilipo limegeuka historia tangu awamu hii ianze hata hapo kabla hawakuwa wanakata Sana.


Ila kwa kiasi kikubwa majenereta hayangurumi Sana kama hapo awali. Hali ilitisha Sana.
Hongera sana
 
Back
Top Bottom