Kalapina awataka wale waliomteka Roma Mkatoliki wakamteke na Yeye ili awaonyeshe Kazi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,073
107,563
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmoja wa Watu wanaoaminika kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe wa kutukuka Kalapina jana wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm aliamua kutema nyongo / kuvunja ukimya juu ya Kitendo cha Msanii mwenzake na mshikaji wake Roma Mkatoliki Kutekwa.

Kalapina ambaye anasifika mno kwa Usela / Uhuni na ukorofi ambao kiuhalisia kweli anauweza alianza kwanza kwa kumpa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.

Ifuatayo ni nukuu Kuntu kabisa kutoka kwa Kalapina ambayo nadhani ni ujumbe tosha kwa Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba Beach ( Watekaji ) “ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo / Kipigo pale pale “ mwisho wa kumnukuu Kalapina.

Haya Watekaji ( Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba beach ) Kalapina huyo anawakaribisheni mkamteke na Yeye ili mkapate Kipondo / Kipigo ambacho inawezekana hata huko Chuoni Kwenu Wakufunzi wenu ama hawakuwafundisha au walisahau kuwafundisha.

Shikamoo Kalapina

Nawasilisha
 
Kuna watu wanaleta utani na manati ya mzungu. 90% ya wabongo wanayaona manati ya mzungu kwenye movies. Unatakiwa ukutane nayo live halafu ifyatuliwe juu karibu na hapo hapo ulipo. Baada ya hapo tuletee hadithi ya ujasiri.
 
Mi kiukweli sijategemea kama angeachia wimbo kama ule kwa PINA nnayemfaham mimi aisee.

Kama kuna mwenye nao huu wimbo tunaomba atuwekee hapa wadau.

Nawasilisha.
 
Anafikiri ni kina chid benzi wale aache kujiona mtemi.

Ila Mkuu wanaomjua Kalapina Vijana wa Mikocheni, Msasani, Mwananyamala, Temeke na Tandika wanasema Jamaa ( Kalapina ) anajua mkono / ngumi sana. Inasemekana Masela / Wahuni wote wa Mjini wanamuogopa mno Kalapina kwani ni Mpenda Fujo / Vagi halafu na hizo Fujo zenyewe nazo zinampenda na zinampa ushirikiano wa Kutukuka pale akiwa anazifanya hivyo yawezekana hao Watekaji wakawa na wakati mgumu sana Kwake kama wakimkabili siku moja.
 
Mi kiukweli sijategemea kama angeachia wimbo kama ule kwa PINA nnayemfaham mimi aisee.

Kama kuna mwenye nao huu wimbo tunaomba atuwekee hapa wadau.

Nawasilisha.

Naomba kuuliza hapa umechangia tu au umeanzisha Uzi mpya ndani ya Uzi wa zamani na uliopo?
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom