Kalapina awataka wale waliomteka Roma Mkatoliki wakamteke na Yeye ili awaonyeshe Kazi

Anafananisha tukio la roma kama lile walilolifanya kikosi cha mizinga kumteka solo thang eeh? huku watekaji walikuja na bunduki na hadi leo hakuna anaetafutwa kuhusiana na tukio lile
 
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmoja wa Watu wanaoaminika kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe wa kutukuka Kalapina jana wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm aliamua kutema nyongo / kuvunja ukimya juu ya Kitendo cha Msanii mwenzake na mshikaji wake Roma Mkatoliki Kutekwa.

Kalapina ambaye anasifika mno kwa Usela / Uhuni na ukorofi ambao kiuhalisia kweli anauweza alianza kwanza kwa kumpa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.

Ifuatayo ni nukuu Kuntu kabisa kutoka kwa Kalapina ambayo nadhani ni ujumbe tosha kwa Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba Beach ( Watekaji ) “ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo / Kipigo pale pale “ mwisho wa kumnukuu Kalapina.

Haya Watekaji ( Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba beach ) Kalapina huyo anawakaribisheni mkamteke na Yeye ili mkapate Kipondo / Kipigo ambacho inawezekana hata huko Chuoni Kwenu Wakufunzi wenu ama hawakuwafundisha au walisahau kuwafundisha.

Shikamoo Kalapina

Nawasilisha

Habari za rwanda mkuu
 
Atakuwa ametoka kuangalia movie ya War Bus au No Retreat No Surender.
Jamaa anajichukulia kama Bolo Yeung. Hajui shotokan inaweza kummwaga mchuzi.
 
Kuna kipindi nilisomaga kitabu cha willy gamba,

Basi nikatoka hom ili nipambane na migambo waliokua wanatoza kodi mtaani maana walikua wanaboa kinyama

Namshukuru Mungu walinivunja meno mawili tu
.......wengine tunalalia chaga tupu mbavu zetu zipo hatarini sasa na vichekesho kama hivi mtatumalizaaaaa
 
Kuna kipindi nilisomaga kitabu cha willy gamba,

Basi nikatoka hom ili nipambane na migambo waliokua wanatoza kodi mtaani maana walikua wanaboa kinyama

Namshukuru Mungu walinivunja meno mawili tu
Hah hah hah weekend njema kwangu.
 
Huyu jamaa mwenzake alisema walete defenda walete mijeda.. aka letewa noah anajua nini kili mkumba
kalapina.jpg
 
Ila Mkuu wanaomjua Kalapina Vijana wa Mikocheni, Msasani, Mwananyamala, Temeke na Tandika wanasema Jamaa ( Kalapina ) anajua mkono / ngumi sana. Inasemekana Masela / Wahuni wote wa Mjini wanamuogopa mno Kalapina kwani ni Mpenda Fujo / Vagi halafu na hizo Fujo zenyewe nazo zinampenda na zinampa ushirikiano wa Kutukuka pale akiwa anazifanya hivyo yawezekana hao Watekaji wakawa na wakati mgumu sana Kwake kama wakimkabili siku moja.
Iv kwel una amini kwamba kule hakuna wakorof aiseee pole yako
 
Imekaa viba hii bado haijatulia ila siku hiyo ndio utaona kuwa iko kwenye box halafu inatingishika

We kali p endekea kuwa tukana ili uwachokonoe waje wakutie kifweni
 
Back
Top Bottom