Kalamu ya Mwigamba: Salamu za CHADEMA kwa watanzania

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
CHADEMA imewatumia salamu Watanzania. Ni baada ya kushinda mtihani waliopewa ama kwa bahati mbaya ama kwa kutegeshewa na wapinzani wao.
Watanzania walikuwa wakisubiri kwa hamu kuona CHADEMA itafanya nini katika mazingira yale iliyokuwemo. Kama ni wapinzani wao kwa maana ya chama tawala ndio waliowategeshea ili washindwe na kuangushwa kisiasa mbele ya wananchi, basi wapinzani wao wamechemsha. Kule Arusha tunasema imekula kwao! Wamewaongezea CHADEMA sifa ya kuchukua dola.
Juni 20 mwaka huu madiwani kupitia CHADEMA katika Manispaa ya Arusha waliingia muafaka na wenzao wa CCM na TLP bila kukihusisha chama.
Hilo lisingekuwa shida sana ikiwa baada ya kufanya hivyo wangewasilisha makubaliano yao na wenzao kwenye ngazi husika za chama ili chama kiridhie. Tatizo liko hivi:
Asubuhi saa tatu madiwani wa CHADEMA walikaa kama party caucus wakaridhia muafaka, saa nne wakaingia kwenye kikao cha kamati ya madiwani wote wakaridhia kwa pamoja.
Baada ya kuridhiana kamati ikabadilika na kuwa Baraza la Madiwani (Full Council) ikiwa chini ya meya yule yule aliyekuwa akibishaniwa. Baraza pia likaridhia na hatimaye muafaka ukaingia kwenye kumbukumbu za halmashauri.
Baada ya hapo CHADEMA wakaombwa kuwasilishwa kwa jina la mgombea wao nao wakaandika kikaratasi chenye jina la Estomih Mallah. Akapita mbele akaomba kura na kuchaguliwa kwa kura 21 kati ya 24 kuwa naibu meya.
Mchana ule ule wakatoka kwenye vyombo vya habari kuutangaza muafaka na jioni saa 1 wakaenda club kwenye tafrija kwa ajili ya kusherehekea muafaka. Katika hatua zote hizo chama hakikuwa na taarifa kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.
Si hivyo tu bali hata wabunge wote watatu katika manispaa ya Arusha ambao pia ni madiwani hawakuhusishwa katika mchakato wote huo. Lakini pia nyaraka yenyewe inayoitwa muafaka ilisainiwa na diwani wa TLP na mkuu wa wilaya. Hakuna kiongozi wa chama hata kimoja kati ya vile vilivyokuwa katika mgogoro yaani CCM na CHADEMA aliyesaini nyaraka hiyo.
Suala hilo lilipofikishwa kwenye kamati kuu ya chama hicho, kamati kuu iliukataa muafaka na kuwataka madiwani wote kuomba msamaha kwa kuingia katika muafaka huo batili bila kuhusisha chama na wale wote waliopata vyeo kutokana na muafaka huo wajivue vyeo vyao. Madiwani baadhi wakakaidi agizo la kamati kuu, chombo kikuu cha utendaji wa chama taifa. Ilikuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu.
Julai 17 wakati kamati kuu ikifanya kikao cha kwanza kilichojadili pia agenda hiyo, viongozi wa madiwani kwa maana ya mwenyekiti na mnadhimu waliitwa na ofisi ya katibu mkuu wa chama kuhudhuria kikao cha kamati kuu na kueleza yale waliyodhani yalihitajika kwa ajili ya kamati kuu kufanya uamuzi wa busara. Walikaidi kwa jeuri kuhudhuria kikao hicho.
Kamati kuu ilipokuwa inakwenda kuketi Agosti 6 mjini Dodoma, Katibu Mkuu akatumia busara ya kuwaita tena madiwani wote waliokaidi agizo la kamati kuu. Safari hii wakaja wote. Habari za uhakika ni kwamba walipewa wote fursa ya kuongea na kamati kuu kwa muda wa kutosha na kupewa nafasi ya mwisho ya rehema kuomba radhi na kujiuzulu vyeo vyao kwa wale ambao walipata vyeo kutokana na muafaka.
Inasemekana wengine walijibu kwa jeuri kwamba "mimi nimekuja kufukuzwa naomba mnifukuze". Katika hali ya namna hiyo na baada ya kubembelezwa sana kamati kuu haikuwa na namna zaidi ya kuwafuta uanachama kwa utovu mkubwa wa nidhamu.
Mengi yamesemwa na wengi wameunga mkono uamuzi wa chama ila wachache wameuponda. Lakini taarifa zinaonyesha waliouponda ni viongozi wa chama tawala. Na hapa kuna sababu kwa nini wameuponda.
Kwanza kama nilivyosema hapo awali imekula kwao. Walilenga kuutumia mgogoro huo kama chambo cha kuiingiza CHADEMA kwenye mpasuko lakini imeshindikana. Chama kimechukua hatua madhubuti na kimebaki imara. Lakini pili viongozi wa chama tawala wameumbuka. CHADEMA imewaonyesha kwamba chama hakitakiwi kuogopa kuchukua maamuzi magumu.
CHADEMA imeonyesha kwamba ukihubiri kwamba unapiga vita ufisadi anzia kwenye chama na kuwatoa wale wote wanaonekana kwenda kinyume na misingi ya chama na si kuhubiri kwamba chama si cha kifisadi ila wanachama ndio mafisadi.
CHADEMA imewaonyesha watawala kwamba watu wanaokaidi misingi ya chama wanapewa siku tatu na si siku 90. CHADEMA imewaonyesha CCM kwamba watuhumiwa wakikaidi amri ya kamati kuu hawaongezewi siku 90 nyingine bali wanachukuliwa hatua moja kwa moja.
Yote haya yamekiaibisha chama tawala na sasa kinawaya waya. Tumesikia kauli za Waziri Mkuu bungeni pale alipoamua kuwa ‘bush lawyer' wa madiwani hao waliofukuzwa uanachama na CHADEMA na kuwashauri waende mahakamani.
Tukasikia Naibu spika naye ‘akichombeza' kwa kudai eti mambo hayo ya madiwani kuchaguliwa kwa nguvu ya umma na kufukuzwa kwa nguvu ya kamati za siasa. Maneno yote hayo ni kuweweseka.
Baada ya NEC ya CCM kuwataka Lowassa, Chenge na Rostam kuondoka kwenye nafasi zao ndani ya chama vinginevyo watatimliwa, sikusikia Waziri mkuu akiwashauri waende mahakamani. Wala sikusikia Ndugai akihoji kwa nini chama kiwachukulie hatua watu waliochaguliwa kwa nguvu ya umma wa wana CCM kuingia kwenye NEC na kwenye ubunge.
Hata Rostam alipojiuzulu nafasi zake ikiwemo ya ubunge, kamati kuu ya CCM ilishangilia na kumpongeza. Pinda alikuwemo kwenye kamati kuu hiyo. Hakumwambia bungeni aende mahakamani.
Ninachosema mimi ni kwamba hizi ni salamu kwa Watanzania kutoka CHADEMA. Wengi walisubiri kuona CHADEMA itafanya nini. Uamuzi wa kuwagwaya madiwani wale kwa namna yoyote ungeonyesha kwa watanzania kwamba hawajawa tayari kuchukua dola ama kwamba hata wao wakiingia watakuwa vile vile kama CCM. Lakini CHADEMA wakawaonyesha Watanzania kwamba wako tayari kuchukua dola na yale wanayoyahubiri ndiyo wanayoyatekeleza.
Ushahidi wa ninayoyasema ni pongezi zilizotolewa na Watanzania kutoka kila kona ya nchi wakipongeza hatua hiyo. Ushahidi mwingine ni umati uliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC kule Arusha.
Jumatano Agosti 10 viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini na Mkoa wa Arusha waliambatana na wabunge kadhaa wa chama hicho pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kuzunguka mjini Arusha wakifungua matawi na kuutangaza mkutano mkubwa ambao ungefanyika kwenye viwanja vya NMC kesho yake.
Watu wengi walifurika kwenye mikutano hiyo ya ufunguzi wa matawi na baadaye kwenye mikutano ya kata ambayo ilifanyika kwenye vituo vitatu jioni yake kikiwamo kituo cha Tindigani anakotoka aliyekuwa Naibu Meya kupitia CHADEMA, Estomih Mallah.
atika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi waliofurika walianzisha pale pale kaulimbiu ya "hatuvui nyoka gamba tunakata kichwa". Muda mfupi baadaye wakatangaza matawi yale yote yaliyofunguliwa yataitwa "kata mti panda mti".
Kesho yake mkutano wa NMC ulifurika. Binafsi naufananisha ukubwa wa mkutano ule na ule wa ibada ya mazishi ya watu waliopoteza maisha kwenye maandamano ya kudai uchaguzi huru na wa haki wa umeya mjini Arusha. Lakini kuna waliosema huu wa Alhamisi Agosti 11 ulizidi.

Kuna kituko kingine kilitokea pale wakati mbunge wa Arusha mjini akihutubia. Alimwonya rais Kikwete kwa kujiangalia anavyoongoza nchi hii kwani kwa umati ule kama CHADEMA wangeamua kuwaambia waandamane mpaka Kikwete ang'oke angeng'oka.

Baada ya kusema hivyo yeye mwenyewe na waandishi waliokuwa jukwaani walishangaa wananchi waliokuwa wamekaa karibu na jukwaa wakiwa wamesimama wote na kugeuka nyuma. Lema alipouliza kuna nini alijibiwa na umati "tunakwenda barabarani sasa hiviiiii!". Ikabidi awaambie "hapana jamani naomba mkae tu tutakapohitaji kuingia barabarani tutawatangazia"
Hiyo ndiyo CHADEMA chama ambacho huko nyuma niliwahi kutabiri kwamba ni chaguo la Mungu la kuwakomboa Watanzania. Wapo walionibeza na kunifananisha na wale wale waliomuita JK chaguo la Mungu. Wakasema sikusitahili kusema hivyo.

Lakini kwa kweli moyo wangu, dhamiri yangu inanituma kuendelea kusisitiza kwamba kuna mkono wa Mungu katika yale yanayofanywa na chama hiki. Na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Aikael Mbowe, amekuja kuniunga mkono katika mojawapo ya mikutano yake kule Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pale alipotamka kwamba yanayofanywa na chama chake si yao bali ni Mungu anawawezesha.
Alikuwa akirejea nguvu kubwa inayofanywa na chama tawala kwa kushirikiana na vyombo vya dola kutaka kuikwamisha CHADEMA lakini kadiri wanavyokazana ndivyo hujikuta wakifanya makosa zaidi yanayowakasirisha wananchi na CHADEMA kuzidi kupendwa na wananchi.
Mfano kuna taarifa za nguvu kubwa ya ushawishi, fedha na vitisho vilivyotumika kuwazuia wananchi wasijitokeze kwenye maandamano ya CHADEMA mikoa ya kusini. Lakini mahudhurio ya wananchi yalivunja rekodi wakati watawala wakiendeleza kufanya makosa ya kuwakosanisha na wananchi kama vile kuiba maiti hospitali na kuzitelekeza barabarani.
Jaribu kuangalia historia ya vyama vikubwa vya upinzan, ni CHADEMA peke yake ambayo haikuwahi kukumbwa na mpasuko wa ndani ama mgogoro wa ndani mithili ya ule wa CUF uliomng'oa James Mapalala kwenye uenyekiti wa taifa au wa NCCR uliomfanya Mrema akimbilie TLP ama ule wa UDP uliopelekea mapinduzi ya kumng'oa mzee Cheyo kwenye uenyekiti taifa na yeye baadaye akawafukuza uanachama wabunge wake wawili.
Ni chama pekee kilichoongozwa na wenyeviti taifa watatu walioachiana madaraka bila mgogoro. Hakuna mgogoro uliowahi kukitikisa chama kwa ndani kiasi cha kushindwa kuukabili na chama kusambaratika.
Salamu za CHADEMA kwa Watanzania ziwawezeshe Watanzania sasa kuamua kukikabidhi madaraka chama hiki na kuondokana na ukiritimba wa chama tawala uliodumaza maendeleo ya nchi hii kwa nusu karne sasa. Kazi ni kwenu Watanzania!

My take: ninapata kuamini sasa kuwa ukombozi wa nchi hii utaanzia Arusha, kama ambavyo wa libya ulianzia Benghazi
 
Uchambuzi mzuri sana, nimeusoma kila mstari, umeenda shule - siku zote nafurahia makala zake. Nitafurahi kusikia mwigamba akiungana na akina Tundu Lissu, Mnyika, Mdee,Lema na vijana wengineo bungeni mwaka 2015 au kabla ya mwaka 2015 kama Kikwete atashindwa kutufikisha huko.
 
We need only 20 people of your caliber.
very good statements with deep clarifications.
Keep it up man.
We are just at the back.
You have the shadow.
 
makala imetulia, yaani kila kukikucha kunazuka kituko kipya, mara jairo, mara mgao wa umeme, mara pinda kadharauliwa, mara sijui nini, yaani ccm sasa hata hawajielewi, kila mtu na lake, tatizo wote wezi hakuna wa kumnyooshea mwenzie kidole, huyu anaiba hapa yule aliwahi kuiba pale, nani alijua kuwa msekwa nae ni mzee wa madili, eti ndo aliwaita mapacha na kuwaambia wajivue gamba, sijui kama alikuwa anawaangalia usoni alipokuwa anawaambia hayo maneno, maana wote wanajuana. ccm bye bye
 
wizi mtupu.!Hivi inawezekanaje madiwani wakafikia muafaka bila hata ya ungozi wa CHADEMA wilaya kujua?Ni yaleyale ya Jairo,luhanjo na Pinda coz hii inaonyesha CDM Hakuna uwajibikaji wa pamoja shame on you CHADEMA.BORA ZIMWI ULIJUALO KULIKO USILOLIJUA.
 
<br />
<br />
Ulilazimishwa kuyasoma,kama hutaki si ufuate shughuli zako?!damn!Big up mchambuzi,well analysed and arranged!nimefunguka macho sasa!

Huyo bwana mdogo ni miongoni mwa wale wafuasi wa Nape wanaopoteza muda wao mwingi kushindana na ukweli ili walipe kwa ujira wa sh 1500 kwa siku.
 
freedom Of Flag
Bwn Mwigamba amefanya uchambuzi makini na sahihi!!!!!Hivyo ni kweli kwa watu ambao wanawatakia ukombozi Watanzania toka mikononi mwa wana magamba (yasiyovuka kirahisi) CHADEMA ndilo chaguo halisi!!!!!!!! Hapo hakuna kuangaliana usoni ukiharibu basi tafuta sehemu nyingine ya kufanyia ufisadi wako lakini CDM hapakufai!!!!!!!! Inatakiwa watu wajipange kuwaelimisha wananchi ukweli kuhusu uongozi wa nchi hii, ili wakati sahihi wafanye uamuzi sahihi kuwaondoa wana maghamba kwenye uongozi!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Maelezo marefu kuelezea vitu visivyoeleweka.

Mwita25 utachoka saana maana Watanzania wamechoka maghamba wanahitaji mabadiliko yaani mageuzi na vehicle ya mageuzi ni CHADEMA!!!!!!! Kwanza wewe sio Mwita umeiba jina Wamwita wameisha choka na uongo wa maghamba's!!!!!!!!
 
Benghazi za Tanzania ziko nyingi ni zaidi ya Libya - Arusha, Mbeya, Mwanza, Musoma, Iringa, Shinyanga, Moshi tunategemea Morogoro nayo itakuwa Benghazi kama wataacha ubitozi wao.
 
wizi mtupu.!Hivi inawezekanaje madiwani wakafikia muafaka bila hata ya ungozi wa CHADEMA wilaya kujua?Ni yaleyale ya Jairo,luhanjo na Pinda coz hii inaonyesha CDM Hakuna uwajibikaji wa pamoja shame on you CHADEMA.BORA ZIMWI ULIJUALO KULIKO USILOLIJUA.
Mtabwabwaja saana kipindi hiki kiama kinawashukia sisi madiwani tumewatoa je, nyinyi vipi kuhusu Jairos mbona mnazidi kumkumbatia??????? Hayo maovu yenu mnayo kumbatia ndio kuamgamia kwenu!!!!!!!CCM kwaheri 2015!!!!!!!!!
 
Nimeipenda sana makala/uchambuzi huu,sana tena sana..nitauprint il niwape na vijana wengne wasioweza kuupata kwa njia ya mtandao..hakika sasa nimejua tatizo la Arusha li wap!!..bora wapganaj wachache na watiifu kuliko weng wanafiki na vigeugeu(ivi yule rasta alyekuwa diwani anaitwa nan?kaiabisha sana din ya rastafarian..)
 
Najisikia furaha sana baada ya kusoma hii makala,CHADEMA MKOMBOZI WANGU.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom