Kalamu ya Askofu Bagonza: Tuhuma za Ugaidi ni silaha ya mtawala dhidi ya mtawaliwa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,090
Askofu Benson Lwakalinda Bagonza (PhD) Ameandika

KABLA YA KATIBA MPYA...

1. Kabla ya Katiba Mpya ya Afrika ya Kusini, Nelson Mandela aliitwa gaidi.

2. Kabla ya "Katiba Mpya" iliyoandikiwa Lancaster, Julius Nyerere alikuwa ni Mchochezi aliyekuwa nje ya gereza kwa kulipa faini.

3. Kabla ya Agano Jipya (Katiba Mpya), Musa alikuwa ni gaidi machoni pa Farao (Firauni).

4. Kabla ya ufufuko (Katiba Mpya) Bwana Yesu Kristo alikuwa na tuhuma za ugaidi na uhaini mbele ya utawala wa Kiyahudi.

5. Kabla ya Muswada ulioleta "Tamko la Haki kwa wote" (Katiba Mpya) huko Marekani, Mwanamke na mtu mweusi kudai kupiga kura ilikuwa ni kitendo cha ugaidi.

6. Kabla ya SUK huko Zanzibar, hayati Maalim Seif alikuwa gaidi, kibaraka wa Usultani na mtuhumiwa wa uhaini.

7. Kabla ya CCM Mpya ("Katiba Mpya"), Waitara, Prof Mkumbo, Mollel, Gekul, Katambi, Silinde, Kafulila, hayati Mgwira nk walikuwa vibaraka wa ubeberu na sasa ni wazalendo.

8.Kabla ya msiba wa kitaifa (Katiba Mpya), Mama SSH alikuwa ni Mshauri wa Rais (Asiyelazimisha ushauri wake), Sasa ni Mshauriwa (Asiyelazimishwa na washauri).

Tunajifunza Nini?

A. Ugaidi ni dhana na silaha ya mtawala dhidi ya mtawaliwa.

B. Muda ndio mwamuzi wa kweli na WA haki.

C. Watawaliwa huteseka; watawala hujuta.

D. Bora mateso kuliko majuto.

E. Katika harakati za kupata madaraka, kila aliyewahi kutawala aliwahi kuonekana ni gaidi mbele ya anaoshindana nao. Hata ndani ya CCM "Magaidi" ni wengi dhidi ya SSH.

Wanaomtuhumu Mbowe kuwa gaidi leo, watakuwa Magaidi wa mfumo wakati ujao.
 
Hata Sabaya aliambiwa na Mbowe safari hii ataozea jela.

Lakini sasa wote watakutana Kisongo
 
Ni gharama kubwa kwa Samia kuzuia mjadala wa katiba mpya kuliko kuwaacha wabishane kwenye bunge la katiba na washindwe kuelewana.
 
Hata Sabaya aliambiwa na Mbowe safari hii ataozea jela.

Lakini sasa wote watakutana Kisongo
Sabaya jambazi wakati Mbowe anaedai haki za kisheria wote wanakutanishwa jela moja chini ya utawala dhalimu.
 
Hata Sabaya aliambiwa na Mbowe safari hii ataozea jela.

Lakini sasa wote watakutana Kisongo

Hata ucopy na kupaste huu utoto kila post humu ndani, uzuri Sasa hivi watanzania ni waelewa wanawachora tu. Hiyo mbinu ilifanikiwa karne iliyopita enzi za Mahita, sio kwa karne hii.
 
Back
Top Bottom