Kakonko, Kigoma: Eng. Christopher Chiza(CCM) achukua fomu kuwania Jimbo la Buyungu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Waziri wa zamani Christopher Chiza ni miongoni mwa wana CCM, walioonyesha nia ya kuwania jimbo la Buyungu lililoachwa wazi baada ya mbunge wake, Kasuku Bilago kufariki dunia.

Bilago alifariki dunia Mei mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Abdul Kambanga amesema hadi kufikia Julai 3, jumla ya wana CCM 20 wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao.

Wana CCM wengine waliochukua fomu ni pamoja Jeremia Ruhele, Maganga Toga Manyama, Brighton Gwamagobe, Mawazo Methusela, Hekima Ngeza, Baraka Mathias, Leopold Muhagaze, Emmanuel Gwegenyeza, Aloys Kamamba na Marco Kumdanko.

Wengine ni Jiles Damianna, Olaf Kaboboye, Aram Kingo, Liberi Ndabita, Ernest Basaya, Msakila Kabende, Anthon Fumbe, Daudi Kidyamali na Meshack Abednego.

Kwa mujibu wa katibu huyo, wana CCM wanatarajia kupiga kura Julai 6 ili kumpata mgombea atakayechuana na wagombea wa vyama vingine katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

chiza%2Bpic.jpg
 
alafu wanawaambia vijana wasitegemee ajira wakajiajiri huku injinia mzima ameshindwa kujiajiri anakimbialia siasa vice versa kabisa na wanayoyasema.
na itakuwa ni moja ya sera yake, pumbavu sana mtu alisha kuwa waziri, ni injinia ana connection kibao kamw mtaji anao ila kujiajili hawezi anatutaka vijana ndo tujiajili
 
Hawa wanasiasa wa aina hii ifikie hatua wananchi wasiende kwenye mikutano yao ajikute yuko peke yake tu sema vijijini mwamko bado mdogo ila mdogomdogo wata amka tu.
 
Ni haki yake, lakini CCM Mpya haiangalii majina wagombea wote hadhi sawa na yoyote atakaeteuliwa kupeperusha bendera wampokee
 
Waziri wa zamani Christopher Chiza ni miongoni mwa wana CCM, walioonyesha nia ya kuwania jimbo la Buyungu lililoachwa wazi baada ya mbunge wake, Kasuku Bilago kufariki dunia.

Bilago alifariki dunia Mei mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Abdul Kambanga amesema hadi kufikia Julai 3, jumla ya wana CCM 20 wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao.

Wana CCM wengine waliochukua fomu ni pamoja Jeremia Ruhele, Maganga Toga Manyama, Brighton Gwamagobe, Mawazo Methusela, Hekima Ngeza, Baraka Mathias, Leopold Muhagaze, Emmanuel Gwegenyeza, Aloys Kamamba na Marco Kumdanko.

Wengine ni Jiles Damianna, Olaf Kaboboye, Aram Kingo, Liberi Ndabita, Ernest Basaya, Msakila Kabende, Anthon Fumbe, Daudi Kidyamali na Meshack Abednego.

Kwa mujibu wa katibu huyo, wana CCM wanatarajia kupiga kura Julai 6 ili kumpata mgombea atakayechuana na wagombea wa vyama vingine katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

View attachment 802545
Njaa tayari ishamkumba yaani umri wote huo bado anataka uongozi?
 
alafu wanawaambia vijana wasitegemee ajira wakajiajiri huku injinia mzima ameshindwa kujiajiri anakimbialia siasa vice versa kabisa na wanayoyasema.
Atakwambia kashindwa kuwakatalia Wanyonge waliomuomba agombee
 
Hawa ndiyo wazee tusiowataka anang'ang'ana tu badala ya kuachia vijana,,,
My take huyo mzee wampige chini wapewe vijana tena fresh toka vyuoni aambao wengi wao wako mitaani na hawana ajira.
Ccm wanawaogopa vijana maana wanajua wengi wao wamejitambua na hawapo tayari kuwa mbunge ndiyo ndiyo
 
Back
Top Bottom