Kakonko, Kigoma: Eng. Christopher Chiza(CCM) achukua fomu kuwania Jimbo la Buyungu | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakonko, Kigoma: Eng. Christopher Chiza(CCM) achukua fomu kuwania Jimbo la Buyungu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Hivi punde, Jul 4, 2018.

 1. Hivi punde

  Hivi punde JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2018
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 1,536
  Likes Received: 3,486
  Trophy Points: 280
  Waziri wa zamani Christopher Chiza ni miongoni mwa wana CCM, walioonyesha nia ya kuwania jimbo la Buyungu lililoachwa wazi baada ya mbunge wake, Kasuku Bilago kufariki dunia.

  Bilago alifariki dunia Mei mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Abdul Kambanga amesema hadi kufikia Julai 3, jumla ya wana CCM 20 wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao.

  Wana CCM wengine waliochukua fomu ni pamoja Jeremia Ruhele, Maganga Toga Manyama, Brighton Gwamagobe, Mawazo Methusela, Hekima Ngeza, Baraka Mathias, Leopold Muhagaze, Emmanuel Gwegenyeza, Aloys Kamamba na Marco Kumdanko.

  Wengine ni Jiles Damianna, Olaf Kaboboye, Aram Kingo, Liberi Ndabita, Ernest Basaya, Msakila Kabende, Anthon Fumbe, Daudi Kidyamali na Meshack Abednego.

  Kwa mujibu wa katibu huyo, wana CCM wanatarajia kupiga kura Julai 6 ili kumpata mgombea atakayechuana na wagombea wa vyama vingine katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

  chiza%2Bpic.jpg
   
 2. pureView Zeiss

  pureView Zeiss JF-Expert Member

  #21
  Jul 4, 2018
  Joined: Sep 5, 2016
  Messages: 1,217
  Likes Received: 2,902
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee atakuwa ANARUKA usiku
   
 3. lnx

  lnx JF-Expert Member

  #22
  Jul 4, 2018
  Joined: Oct 21, 2016
  Messages: 277
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60
  Hata kama lakini huyo mzee akae pembeni awapishe damu changa ishike uwakilishi,amekuwa mbumge waziri miaka mingi leo unakuja kukomaa kutaka ubunge tena kwenya uchaguzi mdogo NI FEDHEHA KWAKE!
   
 4. Gide MK

  Gide MK JF-Expert Member

  #23
  Jul 4, 2018
  Joined: Oct 21, 2013
  Messages: 5,536
  Likes Received: 4,483
  Trophy Points: 280
  Tangu awamu sijui ya ngapi jamaa yupo
   
 5. kelao

  kelao JF-Expert Member

  #24
  Jul 4, 2018
  Joined: Sep 24, 2012
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,571
  Trophy Points: 280
   
 6. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #25
  Jul 4, 2018
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,532
  Likes Received: 46,606
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti anamtaka nani kwenye ilo jimbo?
   
 7. zipompa

  zipompa JF-Expert Member

  #26
  Jul 4, 2018
  Joined: Aug 19, 2014
  Messages: 3,529
  Likes Received: 5,518
  Trophy Points: 280
  Alafu alivyo mnafiki kwenye mahojiano atakwambia "wazee walinifata wakaniomba nigombee nami nikajitathimini nikaona ngoja nigombee"

  wakati ukweli njaa na tamaa ndo zilizo msukuma,huyu apigwe chini tu
   
 8. 3llyEmma

  3llyEmma JF-Expert Member

  #27
  Jul 4, 2018
  Joined: Oct 23, 2017
  Messages: 975
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 180
  Huyu mzee hana vijana,.. Hv anataka nn hasa.
   
 9. Jumong S

  Jumong S JF-Expert Member

  #28
  Jul 5, 2018
  Joined: Jul 3, 2013
  Messages: 3,024
  Likes Received: 1,993
  Trophy Points: 280
  Kwa imani za wale waha watasema hili Jamaa ndo limemkaanga Bilago!!!
   
 10. prs

  prs JF-Expert Member

  #29
  Jul 5, 2018
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 1,659
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Naona Mnamshambulia sana Huyu Mzee.. ila Pamoja na Kuwa Yupo CCM ni Mcha Mungu kweli na Mimi binafsi nafahamiana nae kwa Zaidi ya Miaka 20 Akiwa Moshi,Pasua na Cheo cha Mzee wa Kanisa "HANA NJAA"..Tatizo amechagua Kuwatumikia Wananchi kupitia CCM ambayo hata Mimi Binafsi siipendi..
  CCM ni genge baya sana Linachafua sana Majina na Heshima za Watu..
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #30
  Jul 5, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 13,300
  Likes Received: 6,065
  Trophy Points: 280
  Huyu Chiza anapingana na Katibu Mkuu wa chama aliwataka wale ambao wameshahudumu bungeni muda mrefu na ambao umri umesogea waachie vijana wenye mawazo mapya?
   
 12. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #31
  Jul 5, 2018
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 1,042
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Kama ameshindwa kufahamu kanuni rahisi ya Muumba wake kwamba kadri umri unavyosogea nguvu ya akili na mwili inapungua pia hata huo uzee wa kanisa hakupaswa kuwa nao..kazi ya ubunge kwa sasa inahitaji vijana, lakini pia hana shukurani hata kwa Muumba wake..wakati alipewa nafasi kuwatumikia wanachi hadi kuwa waziri yeye anaona haikutosha tu? nini ambacho hakufanya wakati huo na anataka afanye sasa..ni vzr sana kuridhika na kufahamu kwamba Mungu hajaumba superman..ajue wapo wenye uwezo kuzidi yeye awape nafasi hao..
   
 13. Mbulu

  Mbulu JF-Expert Member

  #32
  Jul 5, 2018
  Joined: Apr 15, 2015
  Messages: 4,772
  Likes Received: 4,372
  Trophy Points: 280
  Jiwe anamuhitaji sana kwa sasa
   
 14. prs

  prs JF-Expert Member

  #33
  Jul 5, 2018
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 1,659
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Umri sidhani kama umewahi kuwa kikwazo cha Maendeleo Tz..Hata hao Vijana Kama Makonda na Mwenzake Wa Arusha Sijaona utendaji zaidi ya Kujikomba kwa Aliyewateua..Inawezekana Alipata Vikwazo awamu ya nne kutokana na Mfumo..
  Ilkua Lazima Ashindwe awamu ile..
   
 15. KIKAZI

  KIKAZI JF-Expert Member

  #34
  Jul 5, 2018
  Joined: Aug 26, 2014
  Messages: 869
  Likes Received: 671
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa kama mtaji anao kwann asionyeshe mfano kwa kujiajiri kwanza anakimbilia siasa.
   
 16. P

  Papa1 JF-Expert Member

  #35
  Jul 5, 2018
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 1,300
  Likes Received: 757
  Trophy Points: 280
  Huyu CCM ya akina Kinana si waliishasema ni cargo!
   
 17. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #36
  Jul 6, 2018
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 1,042
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Mfumo hauwezi kuwa tatizo kwa mtu mwenye akili..hata kama ni hivyo ilitosha fursa aliyoipata kufanya yale Mungu alimpa kutumikia watu, sasa hivi aachie wengine nao pia watoe kile wanacho kwa manufaa ya watu, na si kweli kwamba kutoa mchango wako ni hadi uwe mbunge..afanye vitu vingine akitumia uzoefu alioupata wakati akiwa kiongozi.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...