Kakobe: ufisadi hauwezi kuisha chini ya uongozi wa kifisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe: ufisadi hauwezi kuisha chini ya uongozi wa kifisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 1, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (FGBF), Zachary Kakobe

  Elizabeth Ernest
  Mwananchi


  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (FGBF), Zachary Kakobe amesema ufisadi nchini hauwezi kumalizika iwapo nchi itaendelea kuongozwa na mafisadi.

  Akihubiri katika Ibada kwenye kanisa hilo lilliloko Mwenge jijini Dar es Salaam juzi Jumapili, Kakobe aliwataka waumini wake kujiunga katika vyama vya siasa na kugombea nafasi za uongozi ili waiongoze nchi.

  Alisema kwa sasa nchi inatawaliwa na mafisadi na ndio sababu wamejenga dhana ya "chukua chako mapema" kwa kukosa hofu ndani ya mioyo yao kwa uovu wanaowatendea wanyonge.

  "Wote wanaoimba wimbo wa ufisadi ni wanafiki wakubwa, tena ndio mafisadi wenyewe. Mwenyehaki akitawala baraka za Mungu zinakuja na nchi inastawi", alisema Kakobe.


  Kakobe alisema wenyehaki wakijitosa katika siasa kwa nguvu zote wataushinda ufisadi, lakini, wakikaa pembeni, ufisadi hautakwisha na kwamba nchi itaendelea kutawaliwa katika misingi ya kifisadi.

  "Mwenye haki ndiye anapaswa kuongoza, kwa sababu atasimamia haki za wanyonge, tofauti na sasa nchi inavyoongozwa ambapo kuna watu zaidi ya milioni nane hawajui watakula nini, kwa sababu nchi haiongozwi katika misingi ya sheria ya Mungu", alisema.

  Askofu huyo alisema viongozi wanaoongoza nchi hawana hekima kwa sababu hawaongozwi na Neno la Mungu, tofauti na alivyokuwa hayati Julius Nyerere aliyesema alikuwa akitembea na Biblia kila alipokwenda iliyompatia hekima katika utawala wake.

  "Aliye mkamilifu anayo hekima ndani yake, nahitaji watu wenye haki wajiunge na siasa ili ufisadi uondoke kabisa katika nchi hii na wanyonge wapate haki zao", alisema Kakobe.

  Kakobe aliwataka waumini wake kujinga katika vyama mbalimbali vya siasa akieleza kuwa, hata Yesu alikuwa upande wa wapinzani na kwamba msemo wa ‘fikra kwa mwenyekiti zidumu' sasa haupo tena.

  "Jiunge na chama tawala, hata CCJ ingia nitakutia mafuta. Watu wanaosema siasa ni mchezo mchafu, wachafu ni wao wenyewe, tangu sasa dhamiria kuingia kwenye siasa", kiongozi huyo alisema.

  Kakobe alisema yeyote mwenye haki atapata ujasiri kama simba katika kupambana na mafisadi na kwamba hata yeye anao ujasiri aliosema amepata kutoka kwa Mungu.

  Kiongozi huyo alliyewahi kumpigia debe Augustino Mrema wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), katika uchaguzi wa rais mwaka 2005, alisema lazima wenye haki wasimame kutumikia ufalme wa Mungu na kwa kupigana na ufisadi kwa kujitosa kwenye siasa.

  Kakobe aliyewahi kulumbana na serikali katika mambo kadhaa, alisema viongozi wanaoongoza bila kuwa na hofu mioyoni mwao wanatawaliwa na nguvu za giza.

  Alisema kwamba miungu ya viongozi ni tofauti na wenye haki wanaoongoza kwa sheria na misingi ya Mungu.

  "Wanaoongoza bila hofu ya Mungu, miungu yao iko Bagamoyo, Sumbawanga na Pemba, tofauti na wenye haki ambao wataongoza na sheria inayotengenezwa na misingi ya Mungu",alisema.

  Alisema shetani daima anataka watu wanaofanya matambiko na kwenda kwa waganga waongoze nchi, ili waendelee kufanya maisha ya wanyonge yaendelee kuwa magumu na wasijue watakula nini", alisema Kakobe.

  Hata hivyo, alisema kuwa wapo watawala wanaotafsiri vibaya Neno la Mungu wakidhania kwamba mtu mcha Mungu hatakiwi kutawala, bali kutawaliwa na kueleza kuwa dhana hiyo ni uongo na potofu akisema, biblia haitafsiriwi jinsi mtu aonavyo.
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Duuh jamaa kawapa live simchezo safi sana.


  kanimaliza hapa "Wanaoongoza bila hofu ya Mungu, miungu yao iko Bagamoyo, Sumbawanga na Pemba, tofauti na wenye haki ambao wataongoza na sheria inayotengenezwa na misingi ya Mungu",alisema.
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  safi sana kakobe, waambie hao,...na walivyomcharuza kwenye jengo lake na tanesco, ndo kabisaa kura za wakakobe wote tz nzima si za ccm tena...

  wewe unayesema kakobe hawaambii wafuasi wake michango inayopatikana huko...wewe malaria sugu, najua wewe ni muislam, so hauelewi namna michango ya kikristo ambavyo huwa inakuwa...sisi kwenye makanisa yetu si kilabu cha pombe kisichokuwa na utaratibu...katiba zetu zinaongozwa na neno la Mungu...na tunatoa sadaka kwa kufuata Neno la Mungu, sasa wewe ukileta mambo yako ya msikitini kwenye kanisa, hautakuja kuelewa kabisa. kuna wengi hawaelewi, fungu la kumi hauhitaji kuuliza hata siku moja, ni mali ya mchungaji, kasome biblia mambo ya walawi...na kutoka...sadaka zingine ndo zinaongoza vipindi kakobe kwa mwezi analipia si chini ya milioni 30 kwaajili ya vipindi vya tv pake yake, achilia garama zingine....hivyo mambo msiyoelewa msiwe mnaongea tu...

  yaabu TINI TOKA NIANZE KUSOMA POST ZA MALARIA SUGU SIJAWAHI KUONA POINT YA MAANA YOYOTE ALIYOANDIKA, labda ana malaria sugu kwelikweli..
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hajapona yale maumivu ya nyaya za TANESCO. Anataka kumalizia hasira huku.
   
 5. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  actually huyu si mgeni katika mambo ya mabadiliko ya kweli, kuna kipindi alijitahidi sana kuhakikisha watz wanaondokana na unyonyaji chini ya ccm, aliyekuwa anampigia kampeni alishinda, lakini kura zilibadilishwa na mzee wa nchi aliyekuwa zenji kipindi hicho safarini....akabambikizwa mtu mwingine, ndo maana hadi leo wanasema jamaa alidanganya kuwa lyatonga angeshinda, ukweli ni kwamba alishinda kweli lakini matokeo yalibadilishwa....

  tunatakiwa kumsapoti ili tuondoe chama cha ufisadi..wala hatutakiwi kumponda kwasababu ya chuki binafsi za kidini...tusaidiane kuiondoa ccm madarakani ili tuanze ukurasa mpya...nchi chache duniani bado ziko na chama cha kikoloni hadi leo that means kama vile hatutaki mabadiliko vile...kila wakati ccm wakati tunaona kwa macho yetu hela zetu zinavyoliwa na bado tunataka kuwavunja moyo wale wanaopambana na ufisadi...
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mwanzoni kakobe aliwatetea mafisadi sasa baada ya kumuonyesha jinsi walivyo ndo anataharuki. Bado hujachelewa kukemea ufisadi kwani nchi inaangamia.
   
 7. c

  chibhitoke Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shida ya Kakobe ni consistency. Kesho yuko Ikulu na JK kesho jk ni fisadi/ chagua upande mmoja tukuelewe
   
 8. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hivi lini kakobe alikuwa ikulu? kusema ukweli, kakobe ni moja ya watu tangu kipindi cha nyuma, aliyekuwa anaipinga ccm kwa nguvu zote kwasababu anajua kuwa ni chama cha ufisadi...hili halina ubishi kwa mtz yeyote anajua na ameona ccm walivyo. kipindi cha nyuma hadi walitaka walifungie kanisa lake, na watz wengi walipiga kampeni kanisa lake lifungiwe kwasababu alikuwa kinyume na ccm....na kipindi kile upinzani hata haukuwa imara kama sasa hivi...lakini yeye alishaanza mapambano mapemaaa.

  anaweza kuwa na mapungufu yake kama mwanadamu, lakini kusema ukweli, amejitahidi kuonyesha upande mmoja wa shilingi..tangu enzi za mrema...na kwa sasa, kidogo alikuwa hajaeleweka msimamo wake kipindi walipokuwa wanampiga vita vya chinichini kuhusu kile kiwanja cha kanisa lake na tanesco...na yeye kwasababu alikuwa hataki bifu, ndo maana alikuwa kidogo anaonekana kama yuko nyutro...sasa alivoona wanamletea za kuleta, ndo kaamua kuwa upande mmoja.

  kati ya wachungaji wote waliowahi kusema jk ni changuo la Mungu, kakobe hilo amepinga tangi muda mrefu...kama hamumjui yule jamaa, ana akili sana na anajua anachokifanya, na amepitia mapambano mengi ya aina tofautitofauti...hivyo nafikiri anafaa sana kwenye kundi letu la upinzani dhidi ya ccm. tuachane na udini...mimi mwenyewe sisali kwa kakobe, lakini huwa na admire anachokifanya kwakweli...mwamko huu wa kupinga ufisadi yeye alishakuwa nao kipindi kirefu hata wakati wa mkapa na hata kabla ya hapo...mkapa anamfahamu huyu jamaa manake nusura aondoe tonge mdomoni mwake kipindi kile....naomba Mungu hata sasa apige kampeni ya nguvu...na waha huwa habezi kwenye udini wala nini...

  kwa wale walioona speech yake kipindi cha waraka wa katoliki, alikuwa very nyuturo na alisema wazi kuwa, hata kama yeye ni mlokole, hii nchi ni YA WATANZANIA WOTE, ni ya wakristo, waislam,wabudha, wahindu na wapagani...hivyo tunatakiw akuishi kwa kuheshimiana...na alituliza sana lile bifu la waraka kama mnakumbuka mambo yakapotea la sivyo kulikuwa na mabishano kila mtu alikuwa analeta waraka wake na tulikuwa tunaelekea kubaya..
   
 9. B

  Bull JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu mchungaji Kakobe hayumo kwenye lile kanisa la Mashoga? Hana partner? Tafadhali wekeni list ya Mashoga wale wa kanisani ili tuwatambue.
   
 10. R

  Rwechu Member

  #10
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Do Mkuu kama ungechambua kwa umakini alichosema ingesaidia kuliko ulivyofanya. Alichokisema kakobe ni cha msingi, wanasiasa wenye hofu na Mungu wataisadia nchi sana, hivyo kwa kauli ya hii Mashekhe, mapadri, wachungaji wahamasishe watu wenye maadili wagombee ili suala la rushwa na ufisadi liwe historia.
  Pokea msg yoyote yenye kujenga nchi positively hata kama imetoka kwa mtu ambaye humpendi au sio kiongozi wako wa dini.
   
 11. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  yaani kati ya watu wooote wanaozidi kujianika ukilaza na umbumbumbu wao na kuzidi kujiaibisha na kuaibisha dini yao ya kufuga majini, wewe ni mmoja wapo...haujui ulitendalo tatizo, na unasukumwa na chuki za kishetani aliyewajaa mioyoni mwenu, ndo maana tunasema mwende shule mfunguke akili za kihivyo...unaonekana kama una uelewa wa ubongo wa samaki, mwili mkubwaa ubongo kidogoooo...hatuna kanisa la mashoga tz, na ukiona mtu anatajataja mashoga mashoga ujue ushoga umemjaa moyoni mwake so pengine wewe ndio shoga sasa unatafuta kama utapata wenzio.....bwamdogo hapo umekosea njia....kwa kifupi, hatuna kitu kama hicho kwenye makanisa yetu na wewe ni mtu wa kwanza kusikia unaongea kitu kama hicho kwa makanisa ya walokole Tanzania.....endelea kujianika hadi watu waione aibu yako yote....utakapomaliza, utajikuta uko kuzimu unaota moto na mabikira mnaoahidiwa kuwa mtapata toka kwa marehemu kiongozi wenu....pole sana.
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kila mtu yuko huru kuwa na mawazo kulingana na hali anavyoiona kwa ujumla tupinge au tusipinge serikali ya awamu ya nne ni ya nne inayumba sana na inatetemeshwa na mafisadi na mfumo wa siasa wa taifa umebomoka kwani hakuna upinzani au chama tawala wanaoweza kujisifu kuwa wako sahihi kwani wanasiasa wamegeuza siasa kama mitaji yao binafsi huku wakiacha wananchi wakiteseka sijui wanasiasa wanampango gani na nchi hii, nadhani si kitu cha kushangaza ukisikia tanzania imeingia kwenye machafuko au mapinduzi kwani jamii inaendelea kukandamizwa na wafalme wa taifa hili
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wanataka aongee mnafiki ndo watakubali, akiongea mtu ambaye yuko serious wanampinga...kuna kibaya gani kakobe kaongea hapa, badala ya kumsapoti tuiondoe ccm watu wanampinga just because of religion...kaaazi kwelikweli..
   
 14. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni kupitishwa nguzo za umeme kanisani kwake
   
 15. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hata kama, alimradi anaongea ukweli, na mtamkoma mwaka huu.
   
 16. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2014
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ukweli wa neno la Askofu Kakobe kuwa Mafisadi wanatawala nchi,unaendelea kutimia kila siku ;kwa mfano ESCROW GATE etc !
   
 17. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2014
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ni Mungu aweza kufanya badiliko la nchi;wasizidi zaliwa mafisadi papa na kutawala.

  KICHAFU HAKIZAI KISAFI !
  {AYU 14:4}
   
Loading...