Kakobe Ni mwanasiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe Ni mwanasiasa?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mdau, Jan 5, 2010.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Nimekua nikifuatila kwa karibu sana mienendo na kauli za 'Askofu' zakaria Kakobe wa Full Gospel Fellowship, Mwenge, Dar Es Salaam...naanza kuamini sasa kwamba mtu huyu ni Mwanasiasa zaidi kuliko mchungaji wa kondoo wa Bwana kama navyotaka wengi tuamini...kuanzia sakata lake la kumuunga mkono Mrema, majibizano yake na viongozi wenzake wa kiroho,na sasa hili sakata la TANESCO, vimenifanya nielekee kwenye kumtazama kisiasa na kifedha zaidi kuliko kichungaji..sijaona mantiki ya yeye kuruhusu ama ku-support Tshirts zenye maandishi ya uchochezi na kutoa maneno yenye mwelekeo wa chuki na migongano kwa jamii..TANESCO kupitisha nguzo mbele ya kanisa lake kunahusiana vipi na RICHMOND??? kama alikuwa na la kusema kuhusu RICHMOND, aliwahi kuongea nini kuhusu RICHMOND? Kakobe anaongoza maelfu ya waumini,ambao ana uwezo mkubwa sana wa KU-CONTROL & MANIPULATE their mindsets, sasa anataka kutuambia nini hapa?? jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,na vyombvo vingine vya usalama mnasubiri nini kumkamata mtu anayeweka amani rehani naman hii? mbona mara kadhaa tumeshuhudia mkipita palepale kwa kakobe kwenda kukabiliana na vijana wasomi wa ARDHI UNIVERSITY or UDSM ambao huwa wanadai madai halali na ya msingi?? sidhani kama ni haki kuacha kumpatia haki yake mtu anayevunja haki!!! mkamateni kakobe,liwe funzo kwa wengine..... kwa sasa simtofautishi sana na PROPHET AKABA, yule mchungaji wa kwenye Novel ya Danny Safo His Excellency the Head of State,kwa waliobahatika kuisoma novel hii..........
   
 2. M

  Mndamba Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Sikutegemea mtu kama Kakobe mwenye upeo wa hata kuweza kubadilisha midset za waumini wake angeweza kuwa mtu ambaye hapendi maendeleo. Kwa mujibu wa Tanesco mradi huu wa usambazaji wa umeme umefadhiliwa na serikali ya Japan hivyo sidhani kama ni sahihi kwa Kakobe kupinga zoezi hili lisifanyike. Hata hivyo mimi sioni uhusiano wowote kati ya hili na Ufisadi wa Richmond. Nashauri Tanesco wamuelimishe na napinga kwa nguvu zote matumizi ya nguvu katika kutatua kadhia hili.
   
 3. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  KAKOBE ,anaweza kuwa na hoja kama akisikilizwa, kwani anasema kuwa umeme huo ni mkubwa sana na ukipita kanisani kwake utaingiliana na mitambo yake ya kurusha matangazo, na pili anasema kuwa anataka kuanzisha kituo cha Television hapo hapo kanisani kwake.

  Anadai kwanini mradi usingepita ndani ya hifadhi ya barabara wakati kuna nafasi?
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  Aende zake alipokuwa akijenga hilo kanisa hakujua kuwa kuna barabara? na kwa nini asitoe hati kama ameonewa? anajenga barabarani halafu anataka kutumia ushawishi wa dini kukwamisha maendeleo! piga nyundo kanisa lile!
   
 5. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kakobe m-binafsi na muoga yupo tayari kufanya lolote kujilinda, anaposema "hakuna cha ulokole katika hili" ana maanisha nini? na hizo t-shirt ni kutafuta sapoti, RICHMOND na MISIKITI vimetoka wapi? huyu anataka kulifanya swala lake lionekane la kidini zaidi werevu walisha msoma, anasema atapiga kambi masaa 24 mpaka uchaguzi, mtumzima atishiwi nyau, aache blabla asimame kwenye pointi yake ya msingi (kama anayo) lakini sio mpaka likukute la kumkuta ndio utuandalie WARAKA
   
 6. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Si alisema waraka wa makanisa ni uhaini? Sasa ngoja awe muhaini ndio atajua maana ya neno hilo?

  Au alishasikia kuwa TANESCO wanakuja, ndio maana akaanza kujipendekeza kwa serikali? Maana aliwahi kufanya hivyo hivyo alipohisi Mrema angeshinda mwaka 1995. Bahati mbaya kwake ndoto na sala zake hazikufanikiwa. Sijui kama zitafanikiwa this time around.

  Let's wait and see.
   
 7. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja ni kama jasusi vile. Mbona unafikiri richmond siyo tatizo?Richmond ni kero kwa watanzania wote.Sema kuhusisha dini ni kosa lakini kuhusisha richmond na uonevu ni sawa kwa sababu kila mtu anajua serikali ilitamka wazi kwamba wale RICHMOND HAWAKAMATIKI.KAMA RICHMOND ILIPORA PESA ZA WATANZANIA WOTE IKASABABISHA UMEME KUPAND NA NI WATU WAWILI TU EDWARD LOWASA NA ROSTAM KWA NINI KAKOBE NA KUNDI LAKE KUBWA AMBALO HALIJAPORA WATANZANIA AKAMATWE? HATUWEZI KUSAHAU RICHMOND NA MAJIBU HAYO YA SERIKALI.KAMA TANESKO LINAHITAJI SEHEMU HIYO BASI IWALIPE WAKAJENGE KWINGINE MBONA NDO UTARATIBU
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni vema ungefuatilia kwanininanaprotest kabla yakumtuhumu pamoja na mapungufu yake. Hakuna mfadhili asiyejua madhari mamradi wowote anaoufadhili kwa jamii na namna ya kuushughulikia. Kama mradi unapita maeneo ya makazi ni lazima kuwe na utaratibu wa fidia, sasa tungefahamu nini kimemsibu Kakobe kuprotest huende hajatendewa haki katika hili
   
 9. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  You seem to be so happy to see another man suffering
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Not at all. I just want us all to learn from our deeds. A better world is the one that is fair to all.
   
 11. Kidege

  Kidege Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama muumini wa kakobe vile
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Does it matter in Tanzania ya leo anymore? au kuna something I am missing here?

  Respect.


  FMEs!
   
 13. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Yap,I think your missing something.................or rather, something is missing somewhere...
   
 14. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180

  mkuu Zhule, Jasusi ana rangi gani??? Au unamtambuaje? Kila tatizo lina forum yake, basi kama vipi mlalamikie JK kwa kwenda uwanjani jana badala ya Kigoma ambapo watu wamekula sumu kwenye unga,upo???
   
 15. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  I like your comments.

  Ninachokiona ni kwamba T-shirt za Ask. Kakobe, zimetoa sura ya msimamo wa dhehebu analoliongoza kwamba wanachukizwa na ulaji wa nchi. Kwa lugha nyingine, ni lugha ya fasihi kwamba kanisa linachukizwa na madudu yanayofanywa na serikali kupitia TANESCO.

  Mtoa mada, akapimwe kama yuko sawasawa!
   
 16. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Karibu JF mkuu........unaweza kutueleza JAPO KIDOGO, kati ya TANESCO na SERIKALI/CCM nani anapaswa alaumiwe kwenye sakata la RICHMOND?
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Jan 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Man is by nature a political animal-Aristotle
  unamwonea kakobe mkuu! haujafanya upelelezi wa unachokisema, umewaza umemchukia! Umezusha, kuanzia '95 leo tena ndio unasema mwanasiasa! does this make sense?? kwa hiyo akina Pengo wote wanasiasa!

  You are also politician, so am I.

  Nadhani title yako igekuwa ili sakata la juzi nani mwenye makosa? na siyo kusema vitu kwa kuwaza,
   
 18. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  mkuu Waberoya, nimetumia PLAIN MEANING ya neno mwanasiasa, I agree with you that every human being is a political animal - but in a more philosophical sense I presume........
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Jan 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Umetumia maneno mengi basi plain!

  Kakobe anaongoza maelfu ya waumini,ambao ana uwezo mkubwa sana wa KU-CONTROL & MANIPULATE their mindsets

  Can you actually prove kanisa lenye PhD holders, professors, professionals wa kila aina wamekuwa manipulated na kuwa-controlled na Kakobe!!

  ndiyo sikutaka kubishana na wewe ila next time, peleleza kwanza, what we think and hear is sometime very far away from the truth.

  Sisali kwa kakobe usifikir muumini wake, but i know him
   
 20. T

  Tom JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio ni Mwanasiasa, nawe pia na kila mmoja wetu. Haiwezekani kuishi bila siasa hasa kwa Tanzania ambapo kila mtu ana uhuru wa siasa.
   
Loading...