Kakobe mtumishi wa mungu au tapeli;waumini kuandikisha malizao ,mishahara, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe mtumishi wa mungu au tapeli;waumini kuandikisha malizao ,mishahara,

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, May 3, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  WAPENDWA BWANA YESU ASIFIWE;
  kutokana na maisha magumu na yaliyojaa na kila aina ya mkanganyiko wanadamu wengi tumexchanganyikiwa na kukuta tunafanya mambo yasiyokuwa sahihi.kibaya zaidi naamini din ambazo leo hii hazikuletwa kwetu ili ziwe chanzo cha kisima cha wajanja wachache kuchota fedha badala yake zilikuja ziwe faraja kwetu ;ASKOFU ZACHARIA KAKOBE ni mmoja watu jamii wanapaswa kumuangalia kwa makini sana na kw amacho mawili,na kumuuliza maswali ya msingi...badala ya kumtazama akifanya mambo ambayo hata YESU KRISTO kristo hakunwahi kufanya..kwa wale wakristo na ambao si wakristo watakubaliana nami kakobe si askofu wala mchungaji ni mmoja wa wajanja wa mjini ambae amefanikiwa kuteka akili za watu wenye akili zao timamu na kuziweka mifukoni mwake...
  KAKOBE huyuhuyu amekuwa akiwanyoshea wenzake vidole ambao kwa kiasi fulanai huduma zao zimeonekana nchini..alipotea siku nyingi kabla ya kuibuka na kuwalaumu wenzake wa deci kwa kuwadanganya na kuwahujumu wananchi...kwa sababu aliamua kuzungumza hadharani nae yamkini atendewe haki kwa sababu watanzania si mizuzu.. swala la DECI limeshafikia tam,ati si vyema kuendelea kulizungumzia..lakini SUALA la KAKOBE ni zaidi ya DECI.....KWA MUJIBU WA BIBLIA SUALA LA MATOLEO NI KATI YA MUUMINI NA MWENEYEZI MUNGU. ANAYEMUABUDU,NA SI SWALA LA ASKOFU WA AINA YA KAKOBE..LAKINI NDANI YA KANISA LAKE LA FULLGOSPEL MAMBO NI TOFAUTI.KAKOBE ANAFANYA BIASHARA CHAFU NA HARAMU NA ANAITAJIKA KUCHUNGUZWA ZAIDI YA DECI......NA HII NI KUTOKANA NA MAMBO YAFUATAYO YALIYOFANYIKA WIKII HII KANISANI MWAKE

  BAADHI YA WAUMINI WAMECHANGANYIKIWA BAADA YA KULAZIMISHWA KUJAZA FOMU ZINAZOONYESHA MALI ZAO.. ZIITWAZO ::
  ""TAARIFA BINAFSI ZA MTOA ZAKA MUHIMU;"
  Kila mshiriki wa kanisa anaitajika kujaza fomu hiyo ikiwa ni pamoja na mume;mke;watoto...yeyote mkubwa.unaitajika kuto ataarifa sahihikuhusu mapato yako ya kila mwezi na ukweli wote,,ukifahamu fika hatuwezi kumficha MUNGU imeandika fomu hiyo....
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  kila kipengele cha swali kinatakiwa kujibiwa pasipo kuachwa wazi na jibu la NDIYO au HAPANA; kutegemeana na jibu sahihi pale ambapo jibu lako ni ndio unaitajika kutoa maelezo ya ziada kama kipengele husika kinavyotaka
  "thamanisha kila aina ya wastani wa mapato yako na fedha halisi..pale inapohusiana na mazo ama mifugo na kadhalika ikiwa pato lako haliko katika shillingi za kitanzania andika ni katika USD ;GBP; na RANDI;kadhalika

  SEHEMU A;IJAZWE NA MTOA ZAKA MWENYEWE
  "JINA LAKO KAMILI;ZONI YAKO;SEKDHENI YAKO;KANISA LA NYUMBANI MWAKO
  je wewe ni mfanyakazi wa kuajiriwa ??ikiwa jibu lako no ndiyo ;unafanya kazi wapi??(shirika gani;kampuni gani;wizara nk),

  SWALI LA PILI
  Nafasi yako kazini ni ipi?taja jumla ya kipato chako cha mwezi mzima yaani mshahara wako pamoja na marupurupu imesema fomu hiyo..kabla ya kufanya makato yote....

  SWALI LA TATU
  Je wewe ni mfanyabiashara??ikiwa jibu lako ni ndiyo taja aina ya biashara; ama aina za biashara unazozifanya pamoja na wastani wa mapayo yakokwa mwezi kwa kila aina ya biashara unayofanya.. tumia chati hapa chini kutoa maelezo yako

  chati ina vipengele vitatu
  1)namba
  II)aina ya mifugo
  III)wastani wa mapato

  je unajihusisha kwa namna yoyote na shuguli za uvuvi..kama ndiyo taja pato lako kwa mwezi
  je unajihusuisha na kilimo??kama jibu "NDIYO" ainisha mazao unayolima pamoja na wastani wa mapato yako kwa mwezi kwa kila aina ya mazao unayolima....tumia chati hapo chini
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  SIO NA SISEMI AMINA.....!
  BISHOP KAKOBE anabaki mtumishi wa MUNGU aliye juu.....! anaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya jambo fulani lakini bado anabaki GOD'S SERVANT.....!
  kuorodhesha mali ni utapeli...? Mbona serikali inahitaji watumishi wake waorodheshe mali zao? je na huo ni utapeli au UTAWALA BORA...?
  Anachofanya mtumishi wa MUNGU aliye hai ni KUWAEPUSHA WAUMINI NA DHAMBI YA ANANIA NA SA****....! au mimi ndo nasoma BIBLIA TOFAUTI NA YA WENGINE....?
  WATU HAWA KATIKA BIBLIA WALIFICHA TAARIFA MUHIMU NA WOTE MAUTI ILIWAKUTA.....!
  HALAFU BIBLIA KATIKA WARAKA WA YAKOBO INATUELEZA TUSIWE WEPESI WA KUNENA BALI TUWE WEPESI WA KUSIKIA.....!
  TUANGALIE TUSIJEINGIA UPOTEVUNI KWA KUWA WASEMAJI.....!

  SASA NASEMA BWANA YESU APEWE SIFAAAA.!
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  BADO NAENDELEA KUSEMA KUWA FOMU HIZO NA NYUMBA NYINGINE ZA IBADA INABIDI IPATE NAKALA ZAKE KWANI ZINAWAEPUSHA PIA WATU HAWA KUWA NA VYANZO VISIVYO HALALI VYA MAPATO YAO , UKWEPAJI KODI N.K
  Pia huenda ni mkakati wa kuleta ELIMU ya FEDHA NA UCHUMI ili watu waboreshe vipato vyao.....!
  PIA ITASAIDIA WATU AMBAO HUWA HATUWEKI KUMBUKUMBU NZURI ZA VIPATO VYETU NA AKIBA KUFANYA HIVYO ILI KUJUA TUNAFANYA KAZI YA HASARA AU YA FAIDA....!
  MUNGU APEWE SIFA...!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  mtumishi wa mungui MAHESABU.ni kweli kabisa unachoongea .na kama nimesoma vizuri kilichoandikwa gazetini ni kwamba watu wanaitaji ufahamu wa mungu kwanza ndipo utakapojua unaitaji kutoa zaka ama lah;mimi binafsi naweza kusema kama mwananchi ama mtu anaeitajika kwenda mbinguni ananafasi ya kuuliza pale ambapo hatawea kuelewa.....na jinsi ya kusaidika ni kwa kupitia wewe na mimi.....
  bado naendelea
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  nini maana yake
  Ukiangalia katika Biblia utaona ya kuwa kuna sababu kubwa zifuatazo:
  (a) Tunatoa ili Mungu ashukuriwe ndani ya Kristo Yesu kwa utoaji huo (2Wakorintho 9:11 -12)
  (b) Tunatoa ili injili ihubiriwe (1 Wakorintho 9:7-14)
  (c) Tunatoa ili waliopungukiwa wapate riziki (2Wakorintho 9:12)
  (d) Tunatoa ili Mungu amkemee shetani au yule anayeharibu matunda yetu ndani ya Kristo (Malaki 3:10-12)
  (e) Tunatoa ili tupate zaidi (Malaki 3:10 - 13; Luka 6:38; 2 Wakorintho 9:6-11)
  Unapotoa kitu chochote kwa Mungu kama sadaka, au zaka au dhabihu, uwe na malengo hayo ndani yako.
  Wakristo wengi kwa mfano huwa wanatoa bila kutegemea kupokea. Mara nyingi huwa nawauliza wasikilizaji ninapofundisha juu ya jambo hili hivi; "Je! Ninyi huwa mnatoa fedha kama sadaka?"
  Wanajibu; "Ndiyo'
  Halafu nauliza tena; "Je! huwa mnawapa watu fedha ili ziwasaidie katika shida zao?"
  Pia wanajibu "Ndiyo"
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  May 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  Mkuu maswali yako ni mazito, ila bado kuna vitu vingi unkown.

  1. Unalazimisha kutaka tumwone Kakobe jinsi wewe ulivyo -conclude
  2. Weka fomnu hizo unazosema ili tupate ya kuchangia/kujadili

  Sijaona ubaya wa kakobe na swala la fomu za kueleza mali zao unless uniambie kuwa tatizo lake ni nini? pengine

  (a) anataka kujua mali za waumini wake ili akamate mafisadi wanaotoa sadaka kubwwa kubwa pasi source za mali ao kutojulikana?

  (b) pengine anataka wale wenye uwezo mdogo wasaidiwe????

  (c) kama wamekubaliana kupitia mikutano halali basi hamna kosa hata kidogo, maana lilikubaliwa na watu Mungu anali-sign!

  Kumbuka Kakobe unayemsema jumapili ijayo utakuta watu wako kibao kanisani, kuanzia maprofessor mpaka wale hawajenda shule hata kidogo!

  Haya yote niameandika ili utupe hasa tatizo la huyu jamaa, ili tuwe upande wako, kuna mambo mengi yanaendelea juu Ya KAKOBE, na moja ni kuwa YULE JAMAA ALIJITENGA KUTOKA EAGT, na hivyo EAGT tangu enzi hizo wamekuwa wakumzulia mambo mengi just kutokana na wivu, ninayeandika hapa ni mu-EAGT, baada ya tuhuma nyingi nimeenda kanisani kwake kwa kuchunguza na niliyoyakuta huko ni tofauti kabisa na stori za mitaani,NA WATANZANIA KWA KUPENDA STORI ZA MITAANI hatujambo! na tunaishi kwazo

  Nitasupport ubaya wote unaousema kuhusu huyu jamaa, pale tu utakapo tupa evidence fulani.

  FYI

  Kanisa la huyu jamaa ni moja ya makanisa stable kuliko unavyodhani! hakuna magomvi wala kuchapana bakora wala kujitenga! haya yanampa kuwa awe katika rank ya kuzuliwa lolote baya kwani anakuwa si wa kaiwada. kumbuka kanisa lake ni kubwa EA!

  Kumbuka huyu jamaa haogopi waumini wake hata kama Lowasa angekuwa anasali pale angebehave na yumkini kama angejua ni Fisadi angeshamtenga mapema! hili nalo lina mpa maadui wengi!

  watu unaotaka wachangie hapa ni hao hao wanaenda kanisani, je hawa watu ni sanamau au wewe una akili kuliko wao??? YALE YALE TUNAPSEMA ROSTAM FISADI ILI HALI AMECHAGULIWA NA WATU WENYE NGOZI NYEUSI TI KAMA YANGU MBON TUNAJIHUKUMU?? UNAPOSEMA HUYU MCHUNGAJI MBAYA AU FISADI WAKATI WIKI IJAYO KUNA MAELFU YA WATU KANISANI MWAKE HUONI UNAPOTEZA MUDA!

  lets put in this way, suppose Kakobe ni tapeli, au RA ni fisadi unafikiri tatizo ni kuwaponda hawa au wale wanaowaweka na kuwatukuza- I-mean raia

  wait a minute......

  WAKATI UNAMSEMA HUYU JAMAA LAZIMA TUANGALIE HAWA WATU WAMETOKA WAPI KWENYE MAKANISA YAPI NA WAMEKOSA NINI KULE MPAKA WAJE KWA HUYU TAPELI??
  TUKIPATA JIBU TUNAWEZA KU-CONCLUDE KUWA MAKANISA YOTE YASIYOFUATA BIBLICAL PRINCIPLES (AKIWEMO KAKOBE KAMA HAFUATI) BASI NI MATAPELI MACHONI PA MUNGU! au unafikiri makanisa ya Katoliki, anglican, lutheran huko kuko safi Ok??

  Utakapofikia wakati wewe kumuhukumu Kakobe nadhani utatumia biblia! then biblia hii haitatulia mpaka ikong'ote mapadri, maaskofu, wachungaji kila kona na kila kanisa! biblia hii haitatulia mpaka itakufuata wewe mwenyewe ndani kabisa ya moyo wako na kusema what about you?? before looking kakobe!

  nimesema hivi kusudi tuamke na kuona kama kuna tatizo basi ni kubwa sana katika makanisa yetu yote, na watu wa kulaumiwa si hawa viongozi ni waumini HAWASOMI BIBLIA , wengine wanataka wasafiri bila passport kwenda ulaya, wengine wanasema Yesu anakuja April 30!

  Ukiamka na kusimamia biblia kikamilifu pasi kufuata siasa za makanisani bila shaka utaona katoliki hamna kitu, so as other many churches,I bet unaweza kurudi kwa Kakobe na kuona afadhali!!!

  in short watanzania ni wanafiki wengi hawana dini japo wana majina ya kikristo na kiislamu, lakini wengi ni zero , wanafuata dini simply kwa sababu wazazi wao walikuwa dini hizo! ukiangalia kwa makini unafiki watabia zetu halisia ndio umepelekea mpaka hata nchi yetu kufikia hapa.

  Keep it real!
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Unapotoa kitu chochote kwa Mungu kama sadaka, au zaka au dhabihu, uwe na malengo hayo ndani yako.

  Nini maana yake sipingani na kakobe ila naitaji tuelimishane kwamba suala la muhimu si kujua mtumishi ana kiasi gani...anachotakiwa ASKOFU KAKOBE ni kumuomba mungu awafungulie watumishi wake ""UFAHAMU""na si kutoa fomu za kujaza mali zako...
  Mtumishi macalculation kama uankwenda kanisani utaona watu wengi wanapotea kwa kukosa maarifa...makanisa mengi yamkuwa yakihubiri juu ya zaka;utoaji;nk .ni kweli lakini ukija katika hekima,maarifa na ufahamu utaona kumbe hata ukipata ufahamu utajua kuna fungu la kumi,sadaka nk.....mimi kama mtumishi ssiitaji kumlazimisha mtu kutoa wakati biblia inasema wazi....

  Ni kweli kwamba mishahara ya watu haitoshi kukidhi mahitaji yao ya kila siku pamoja na familia zao.
  Ukisoma katika 2Wathesalonike 3:6-12; Mtume Paulo anawaeleza Wathesalonike juu ya umuhimu wa kila mtu kufanya kazi. Na hata anaendelea kusema, "ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi , asile chakula. Na katika 1Wathesalonike 4:11 - 15 anazidi kukaza juu ya mtu kufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe.
  Naamini unafahamu ya kuwa ingawa watu walimhudumia Mtume Paulo kwa kumpa vitu vya kumsaida kimaisha; lakini yeye mwenyewe hakuwalemea bali alifanya kazi kwa mikono yake ili aongeze kipato chake.
  Wachungaji na wakristo wengi wanajihusisha na miradi mbalimbali binafsi kwa ajili ya kuongeza kipato. Hili ni jambo zuri; lakini ni muhimu kuwa mwangalifu ili miradi hiyo au kazi unazofanya ili kuongeza kipato, hazitaharibu uhusiano wako na Mungu na kuzorotesha wito wako.
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  kama umesoma hapo juu unapotoa chochote kwa mungu ni lazima uwe na malengo...ujue hii dhabihu namtolea mungu ,,.mungu naitaji kitu fulani kwa akupitia dhabihu hii....bado nalalama hatuitaji kuwalazimisha watu waorodheshe mali zao ili tujue jinsi ya kupata zaka,sadaka ama dhabihu..bado neno la mungu linasimama kwa nafasi yake....natuamaini tuko pamoja mtumishi
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA
  " Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote, ili sasa, kwa njia ya Kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho"(Waefeso 3:8 - 10).

  " Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU,NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)

  Kristo ana utajiri usiopimika. Na wote walio ndani yake ni warithi pamoja naye wa utajiri usiopimika. Kutokana na utajiri huo TUNAJAZWA KILA TUNACHOKIHITAJI. Mahitaji haya ni ya kiroho, kiakili na kimwili. Kwa hiyo hakuna sababu ya mkristo kuishi maisha ya kupungukiwa, ikiwa Kristo yuko ndani ya moyo wake pamoja na utajiri wake usiopimika. Au wewe una maoni tofauti juu ya hili?
  Jambo la kujiuliza ni hili; kwa nini utajiri huu wa Kristo usiopimika hauonekani katika maisha ya wakristo wengi? Wakristo waishije katika ushuhuda wa wokovu ndani ya Kristo, wakati wanaishi katika ulimwengu wenye hali ngumu kiuchumi? Watumishi wa Mungu kwa mfano, wachungaji, wainjilisti na kadhalika, waishije katika kumtumikia Mungu vizuri bila kupoteza ushuhuda wao wakati wanaishi katika mazingira yenye maisha magumu kiuchumi?
  Haya si maswali mepesi kuyajibu, lakini ni muhimu yatafutiwe ufumbuzi. Kabla hatujaanza kuyajibu napenda tusome Waefeso 4:11;

  " Naye (Yesu Kristo) alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na Waalimu."
  Ni kwa kusudi gani Bwana Yesu Kristo aliamua kuwaweka hawa katika kazi yake kanisani? Waefeso 4:12-16 inatupa maelezo:-
  "Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiunganishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo"

  Kwa kuisoma mistari hii tunapata kufahamu ya kuwa hawa waliotajwa ni watumishi wa Mungu katika Kristo. Na wana wajibu maalum waliopewa na Mungu. Pia ni muhimu kukumbuka kuwa si hao peke yao waliotumwa kazini na Kristo, lakini kila mkristo ana wajibu wa kufanya (Yohana 17:18; Warumi 12:4-8).
  Naamini kabisa ya kuwa tukifahamu Mungu aliwatunzaje watumishi wake katika biblia, tutakuwa tumepata mwanga wa jinsi ambavyo anawatunza watumishi na watu wake hivi leo. Ni budi tukumbuke ya kuwa Yeye ni yule aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuja (Ufunuo 4:8) na pia ni "Yeye yule jana na leo na hata milele" (Waebrania 13:8)
  Baada ya kuisoma biblia kwa makini nimeona ya kuwa kuna njia nne ambazo Mungu amekuwa akizitumia kuwahudumia na kuwatunza watumishi wake na watu wake. Na naamini hata hivi leo anatumia njia hizi, kwa namna ambayo yeye mwenyewe amechagua.

  Njia ya kwanza; Mshahara:
  Njia mojawapo anayotumia ni kuwapa watu wake mishahara au ujira - kufuatana na kazi wanazozifanya.
  "Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo? Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe? Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu, kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini; naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake."

  Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni je! Ni Neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?
  ".......... Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio injili wapate riziki kwa hiyo injili" (1 Wakorintho 9:7-14)
  Kwa sababu unafanya kazi ya injili, Bwana ameamuru kwamba upate riziki yako katika injili. Watu wengine kwa kutokuelewa vizuri juu ya mistari hiyo tuliyoisoma, wameigeuza kazi ya kumtumikia Mungu kama mradi wa kupatia fedha za kumsaidia kuishi. Lakini kazi hiyo ni wito. Na kila wito una kusudi lake. Na kwa kuwa Mungu anafahamu kuwa utahitaji kuwa na mahitaji muhimu ya maisha, anakupa mshahara au ujira. Njia anazotumia kutoa mishahara au ujira ni nyingi, na anazitumia kama apendavyo yeye.
  Na kwa wale walio na utaratibu wa kuwapa wachungaji kama mishahara, fedha hizo mara nyingi zinakuwa hazitoshi kukidhi mahitaji yao ya kila siku na familia zao. Na hii ndiyo hali halisi. Lakini jambo muhimu ni kwamba wanapewa mshahara.
  Ukisoma kitabu cha Hesabu 18:8-15, 18 - 20 na Kumbukumbu la Torati 18:1-5 utaona ya kuwa kwa kadri wana wa Israeli walivyomtolea Mungu wao sadaka ndivyo na makuhani walivyoopokea ujira wao. Kwa maneno mengine ina maana ya kuwa, kama wangetoa sadaka kidogo, basi na makuhani wangepata ujira kidogo.
  Na pia watumishi wa Kristo wanatakiwa watunzwe kwa chakula katika nyumba ambazo wanakwenda kuhudumu. " Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Enendeni, angalieni nawatuma kama wana kondoo katika ya mbwa-mwitu ..... Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu ...... Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake ..... Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu"
  (Luka 10:1-8).

  Njia ya Pili: Utoaji:
  Njia nyingine ambayo watumishi wa Kristo na wakristo wanaweza kupokea vitu vya kuwasaidia katika maisha yao ni kwa njia ya utoaji.

  Biblia inasema katika Luka 6:38;" Wapenzi watu vitu, nanyi mtapewa, kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpiamacho ndicho mtakachopimiwa".

  Swali muhimu la kujiuliza ni kama mtu anaweza kutoa kama hana kitu cha kutoa. Ni wazi kwamba hataweza kutoa. Lakini mara nyingi hatakosa kitu cha kumtolea Mungu.
  Na jambo hili Mungu anafahamu. Hata kule jangwani alipowaambia wana wa Israeli watoe kwa ajili ya ujenzi wa Hema ya kukutanikia; alijua kabisa kuwa alikuwa amewapa vitu hivyo kabla hawajatoka Misri. Kwa hiyo walitoa walizokuwa wamepewa na Mungu tayari. Na walipotoa, Bwana aliwabariki zaidi.
  Kwa mkristo je! Anapotakiwa atoe ili apokee, atoe kitu gani alichopewa na Mungu? Wazo la kwanza linalonijia ni atoe fungu la kumi la mshahara wake kila mwezi kama yanenavyo maandiko. Soma Malaki 3:10.
  Mkristo asipokuwa mwaminifu kumtolea Mungu ahadi yake ya fungu la kumi, anategemea kubarikiwa kwa njia gani? Na je! Ni vizuri kwa mchungaji kutokuwa mtoaji, wakati anawafundisha wakristo wawe watoaji?
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  lol, hii kali..
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Asifiwe milele ..Amina
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Toa Kutoka Moyoni

  Katika kitabu cha Malaki, Mungu aliwataka watu waishike torati Aliyoweka miaka 800 awali na Musa. Mungu alinena umuhimu wa dhabihu safi (Malaki 1:7-8), na haja ya makuhani kunena ujumbe wa kweli (Malaki 2:7-8) pia alinenea juu ya kutoa sehemu ya mali yetu-sehemu inayojulikana kama fungu la kumi.

  Malaki 3:8,10
  "Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia Mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu."

  Kanuni ya matoleo ilianza na Kaini na Habili (Mwanzo 4:3-4). Abrahamu baadaye akadhihirisha wazo la fungu la kumi alipompa Melkizedeki "fungu la kumi la vitu vyote"(Mwanzo 14:20) lakini mfumo wa kutoa fungu la kumi haukuanzishwa, mpaka Mungu alipompa Musa torati, (Kumbukumbu la Torati 27:30-33).

  Wakati wa Malaki, Mungu hakutaka tu kurejeshwa nidhamu ya kutoa fungu la kumi, bali alihuzisha fungu la kumi na baraka na akatoa changamoto: "Mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya Mbinguni" (Malaki 3:10). Mungu bila shaka "hatupatii" eti kwa sababu ya chochote tunachofanya; bali Neno Lake lina mwito wa kutii, na utiifu halisi kila mara huleta baraka kamili.

  Yesu alipokufa msalabani, Alitimiza torati kwa wote wanaoamini Na ingawa barua halali ya torati imepita, lengo la torati (ambayo ndiyo moyo wa Mungu) linabaki wakati wote; "mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo" (Wakolosai 2:17).

  Lengo au "Ukweli" wa torati zote ni kwamba Mungu ni Bwana juu ya sehemu zote za maisha yetu. Torati inafundisha ukweli huu na kutuonyesha jinsi tunavyopungukiwa na kiwango chake. Kusudi la torati lilikuwa zaidi ya kutufundisha sisi kukubaliana na mpango wa kanuni zilizoandikwa. Uvuli katika torati iliyoandikwa inasema "Usiue"lakini ukweli katika Kristo unasema kusiwe hata chuki moyoni, (Mathayo 5:21-22). Uvuli katika torati pia inasema "Usizini" lakini ukweli katika Kristo unasema hata usitamani (Mathayo 5:27-28).

  Tunajadili juu ya "Sheria"ya ngapi na wapi kutoa, tutakuwa tunatazamia uvuli na kukosa ukweli wa Kristo - Yeye ni Bwana wa WOTE! Tunapoangazia macho yetu kwa Kristo, tutatoa.

  Tutatoa kwa ukarimu, "Si kwa huzuni, wala si kwa lazima" (2 Wakorintho 9:7). Tutatoa kwa furaha kwa wakati wetu, talanta, na fedha kwa mahitaji yale Anayotuelekeza. Akiwa Bwana kweli kweli, hatutatoa tu kwa "mtindo"unaoshrutishwa na torati, tutaishi katika neema zake na kutoa kulingana na kanuni ya torati. Akiwa Bwana tutaacha kumwibia Mungu na kutoa kwa furaha maisha yetu kama tutoavyo kutoka moyoni.

  Kuwa Na Siku Njema
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  May 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  Supported!

  Kuna maswali mengi kuhusu fungu la kumi, na kwa namna moja au nyingine mimi sikubaliani nayo-NINAKUBALIANA NA WEWE ;KULAZIMISHANA HAPA NDIO inaboa.

  Wakorinto-inasem atutoe kwa moyo
  pia tunaambiwa kuwa ibidi tuongozwe kwa roho! unapotoa zaka unaogozwa kwa Roho?? NA je hii ni sheria?? na kama ni sheria Yesu alizfuta zingine hii akaiacha??
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Toa Kutoka Moyoni

  Katika kitabu cha Malaki, Mungu aliwataka watu waishike torati Aliyoweka miaka 800 awali na Musa. Mungu alinena umuhimu wa dhabihu safi (Malaki 1:7-8), na haja ya makuhani kunena ujumbe wa kweli (Malaki 2:7-8) pia alinenea juu ya kutoa sehemu ya mali yetu-sehemu inayojulikana kama fungu la kumi.

  Malaki 3:8,10
  “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia Mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu.”

  Kanuni ya matoleo ilianza na Kaini na Habili (Mwanzo 4:3-4). Abrahamu baadaye akadhihirisha wazo la fungu la kumi alipompa Melkizedeki “fungu la kumi la vitu vyote”(Mwanzo 14:20) lakini mfumo wa kutoa fungu la kumi haukuanzishwa, mpaka Mungu alipompa Musa torati, (Kumbukumbu la Torati 27:30-33).

  Wakati wa Malaki, Mungu hakutaka tu kurejeshwa nidhamu ya kutoa fungu la kumi, bali alihuzisha fungu la kumi na baraka na akatoa changamoto: “Mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya Mbinguni” (Malaki 3:10). Mungu bila shaka “hatupatii” eti kwa sababu ya chochote tunachofanya; bali Neno Lake lina mwito wa kutii, na utiifu halisi kila mara huleta baraka kamili.

  Yesu alipokufa msalabani, Alitimiza torati kwa wote wanaoamini Na ingawa barua halali ya torati imepita, lengo la torati (ambayo ndiyo moyo wa Mungu) linabaki wakati wote; “mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Wakolosai 2:17).

  Lengo au “Ukweli” wa torati zote ni kwamba Mungu ni Bwana juu ya sehemu zote za maisha yetu. Torati inafundisha ukweli huu na kutuonyesha jinsi tunavyopungukiwa na kiwango chake. Kusudi la torati lilikuwa zaidi ya kutufundisha sisi kukubaliana na mpango wa kanuni zilizoandikwa. Uvuli katika torati iliyoandikwa inasema “Usiue”lakini ukweli katika Kristo unasema kusiwe hata chuki moyoni, (Mathayo 5:21-22). Uvuli katika torati pia inasema “Usizini” lakini ukweli katika Kristo unasema hata usitamani (Mathayo 5:27-28).

  Tunajadili juu ya “Sheria”ya ngapi na wapi kutoa, tutakuwa tunatazamia uvuli na kukosa ukweli wa Kristo - Yeye ni Bwana wa WOTE! Tunapoangazia macho yetu kwa Kristo, tutatoa.

  Tutatoa kwa ukarimu, “Si kwa huzuni, wala si kwa lazima” (2 Wakorintho 9:7). Tutatoa kwa furaha kwa wakati wetu, talanta, na fedha kwa mahitaji yale Anayotuelekeza. Akiwa Bwana kweli kweli, hatutatoa tu kwa “mtindo”unaoshrutishwa na torati, tutaishi katika neema zake na kutoa kulingana na kanuni ya torati. Akiwa Bwana tutaacha kumwibia Mungu na kutoa kwa furaha maisha yetu kama tutoavyo kutoka moyoni.

  Kuwa Na Siku Njema
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  May 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  Unapoint zinanikuna ila uilinza vibaya, tu-support your arguments!

  1. No More Tithing
  2. [ame=http://video.google.com/videoplay?docid=-4387981217836322043]Tithing is Not a Christian Doctrine[/ame]
  3. Should the Church Teach Tithing? Taboo Answer
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Naona sarakasi zimeanza ..lol

  Mimi binafsi siamini kuna justification yeyote ya muumini kuorodhesha mapato yake kwa mchungaji wako. This is absurd. Jinsi ninavyo-manage finance zangu ni Mola tu anajua, na hapaswi yeyote kuanza sarakasi za kuniconvince kwa kutumia his misplaced understanding of Biblical verses.

  Ndio maana mimi nilishaacha zamani kutoa zaka sijui sadaka ili mchungaji akanunue suti kali au gari wakati kuna wahitaji mtaani wanavaa midabwada na hawajui mlo unaofuata utatoka wapi. Pesa alonijalia Mungu nashea na wenye shida na un-preveleged people ONLY. Na inapobidi kuchangia ujenzi au chochote, inabidi kiwe well documented ili nitoe mchango wangu, bila hivyo watanisikia tu kwenye bomba. Hawa wachungaji its time waige mfano wa Paulo aliyekuwa akila kwa jasho lake mwenyewe pamoja na ontransit nyingi tu za kuhubiri injili ktk mazingira magumu.
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  mahesabu utoaji una siri nyingi sana ninachongnganiana na wewe ni kwamba tunaitaji kujua dhumuni la utoaji nini nini??kuwaelimisha wapendwa kwa nini tunaitaji dhaka...unaweza ukawa multimillionea kama ROSTAM AZIZ ukataka kutoa kwa ajili ya kuonekana mbele ya watu wa mungu end of the day mungu anaona unapoteza muda ndugu...so dhumuni langu ni kuwafundisha watu wajue ufahamu wa mungu kwanza badala ya kuwalazimisha kuandika mapato yao ambapo mwisho wa siku hata yule mchungaji anaekula pesa za dhambi nae anapata dhambi.....ukiwa unatoa narudia tena ukiwa unatoa lzima uwe na msimamo na mungu wako unamtolea akutendee nini ama unaitaji nini kutoka kwake??u get me...unaweza ukawa na waumini wanatoa zaidi ya million kumi kila wiki kwa zaka na sadaka kama hawamjui mungu wanapoteza muda wao na we unaehubiri kutoa mapato unapoteza muda wako..laa maana ni kimoja watumishi wa mungu wamekuwa wakiongelea kila siku kanisani suala la utoaji like if hakuna mengine katika bibilia....muelekeze mtu ajue umuhimu wa kutoa wanza ,na mafanikio yake
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Rostam akanwa kwa kujikosha


  Mimi ni mkristo jamani,lakini naona kanisa nalo limekurupuka na kumkwepa Rostam Aziz katika hali ambayo naamini si nzuri.kanisa lingejikita tuu kuzungumzia suala la ukiukwaji wa taratibu na kukana suala la kujua kama Rostam ni msafi au siyo msafi.lakini walivyoelezea ni kama vile wanaamini kwamba Rostam si msafi,hii naiona si sawa kwani hata wao hawawezi kujua dhamira ya mtu huyo.Kusema kwamba kanisa halikumbatii mafisadi nk ni kama vile maneno yaliyopitiliza,kwani kanisa lina maana Rostam ni fisadi??Kanisa halijui jambo hilo,naamini kanisa linachojua ni kwamba Rostam ni mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, aweza kuwa na dhambi yoyote,kwani binadamu hatujakamilika(lakini dhambi yake sio kitu cha kushabikia) na kwamba alialikwa kwa nia njema kusaidia kutunisha mfuko,tatizo tu ni kwamba taratibu hazikwenda vizuri katika ujio wake huo,na kwamba mgeni huyo amekosea kutumia mimbara ya kanisa kuzungumzia siasa.Kanisa tujikite katika kukanusha na kuelekeza kwamba kanisa sio jukwaa la siasa,basi.hayo mengine ya sijui...Rostam si msafi au sijui fisadi,yasisemwe na kanisa,ni mambo ya siasa.

  frm dar hotwire
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Ibada
  Katika Biblia Yako Soma
  Ufunuo 4 na 5
  Mstari Wa Kukariri
  Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza (Kut 23:25, 26).
  Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
  Taja baadhi ya sanamu na miungu ya uongo ambayo wanadamu huitumikia na hivyo kumfanya Mungu aone wivu na kukasirika.
  Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
  Andaa hafla maalum kwa ajili ya kumfanyia Mungu ibada wakati wa jioni. Watafute na kuwashirikisha wapakwa mafuta, na kumfurahisha Mungu kwa nyimbo za kusifu na kuabudu.
  Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
  Andaa orodha ya mistari mbalimbali katika Zaburi inayoonesha njia mbalimbali zilizotumika kumwabudu Mungu.
  Tafakari Andiko Hili Neno Kwa Neno
  Waefeso 5:19,20
  Tumia Dakika Moja Kuubadili Ulimwengu
  Ombea taifa la Albania; Idadi ya watu: 3,500,000;
  Ni taifa la kwanza ambalo awali kabisa halikuamini kwamba kuna Mungu. Na sasa limeharibiwa na kutokuwepo na serikali pamoja na tatizo la wakimbizi. Kitakachotamalaki sasa ama ni Injili au Uislamu.

  Kimsingi mwanadamu ni kiumbe anayeabudu. Ibada ni sehemu ya asili yake. Swali pekee la kujiuliza ni nani mungu anayemwabudu? Ye yote tunayemwabudu, hatimaye huyo ndiye tutakayemtumikia. Kanuni ni kwamba, kwa kadiri tunavyoendelea kuabudu cho chote au ye yote tunayemwabudu ndivyo hivyo tutakavyoendelea kujitoa kwake, na kwa kasi iyo hiyo tutaendelea kufanana na kile tunachokiabudu.
  1. Kuabudu Kuna Maana Gani?
  Neno la Kiebrania shachah lina maana ya kuabudu, kusujudia, kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la Agano la Kale proskuneo halikadhalika lina maana ya kubusu mkono, au kupiga magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso kwa unyenyekevu mkuu. Maneno mengine mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika, kufanya ibada takatifu na kumtolea Mungu sadaka.
  2. Waache Watu Wangu Waondoke, Ili Wapate Kunitumikia
  Dai hili Mungu alilolirudia mara kwa mara lilipelekea Farao kuwaruhusu watu wa Mungu kutoka Misri. Tangu wakati huo, Mungu, Mungu mwenye wivu, amekuwa akipambana na watu wake akiwazuilia kuabudu miungu mingine na sanamu, na badala yake wamwabudu Mungu aliye hai na wa kweli.
  Ibada ni kumtukuza Mungu na kumfurahia daima. Mungu anawatafuta watu wa kumwabudu, na kufanya ibada ndiyo wito wetu wa kwanza (Yn 4:23). Ibada ya kweli ni pale tunapomruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutoka katika roho zetu au mioyo yetu kuabudu katika roho na katika kweli (Flp 3:3).
  Ibada ni tendo la thamani kubwa, ni la kipekee na linamhusu Mungu na Mwanaye Yesu Kristo ambao peke yao wanastahili. Lucifer, aliyekuwa mhusika mkuu wa ibada huko mbinguni, alitaka ibada hiyo iwe kwa ajili yake, maana yake aabudiwe yeye; na hilo ndilo lililopelekea kuanguka kwake (Isaya 14 na Ezekieli 28). Hata wakati fulani alitaka Yesu amsujudie ili eti ampe falme zote za dunia lakini Bwana alikataa (Mt 4:8-10).
  3. Ibada Hukifanya Chumba Kujawa Na Mungu
  Katika nyakati za Biblia watu wengi wake kwa waume walipakwa mafuta na Mungu na kisha kuteuliwa na viongozi wao kuwaongoza watu wa Mungu zamani hizo, kufanya ibada ya kinabii na si kama sisi tanavyofanya katika siku zetu kwa kuimba tu nyimbo katika makusanyiko yetu (1Nya 25:1,6-8).
  Ibada huandaa njia ya Mungu kushuka na kukujaza wokovu maishani mwako (Zab 22:3) (Zab 50:23). Ibada ya watoto ina uwezo wa kumnyamazisha adui (Zab 8:2).
  4. Nitambariki Bwana Nyakati Zote
  Je, ni wakati gani tuabudu? Nyakati zote. Kwa nyakati zilizotengwa Zaburi ya 100 inatuelekeza namna ya kuanza, lakini zaidi ya yote tunapaswa kuishi maisha ya ibada bila kukoma. Kwa kila tunapopumua, kwa kila wazo, kwa neno na tendo, tunapaswa kumwabudu Mungu wetu mzuri tunayemtumikia milele na milele (Zab 145:1,2).
  5. Ibada, Zamani, Sasa Na Wakati Ujao
  Watu walianza kuliitia jina la Bwana zamani sana. Wakati Abramu alipokuwa akiiendea ile Nchi ya Ahadi, jambo la kwanza alilolifanya kila alikokwenda ni kujenga madhabahu kwa ajili ya ibada (Mwa 4:26) (Mwa 12:6).
  Siku zilipita na watu wakafanyia ibada kwenye Hekalu na kwenye masinagogi; lakini siku hizi miili yetu ni hekalu la Mungu (1Kor 6:19). Maana yake ni kwamba sisi tunaweza kuabudu bila kukawia, mahali po pote, katika mazingira yo yote. Paulo na Sila walifanyia ibada gerezani (Mdo16:25).
  Lakini ibada yetu hapa duniani ni picha tu ya ibada ya mbinguni. Yakupasa kusoma aya za utukufu za Ufunuo 4, 5, na 19:1-10 ili upate kuona kwamba ibada ya mbinguni imejawa na rangi, nuru, sauti, miondoko na shughuli. Ibada yetu inapaswa kufanana na hiyo ya mbinguni.
  6. Je, Tunafanyaje Ibada?
  Biblia inatufahamisha jinsi watu walivyotumia mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na midomo yao katika uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza, kusifu, kubariki na kushukuru.
  Maneno kama halal na haleluya kutoka katika Zaburi yana maana ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana. Neno Yadah lina maana ya kunyoosha mikono hewani, na neno barak lina maana ya kupiga magoti katika ibada ya kumbariki Mungu.
  Kuitoa miili yetu katika kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu katika sanaa zao, katika uandishi wao, katika michezo ya kuigiza, katika muziki, katika usanifu wa majengo, na hata katika utoaji wa fedha zao kwa ajili ya Injili.
  7. Ibada Kanisani
  KatIka kanisa makusanyiko yetu yanapaswa kujawa na zaburi, nyimbo, na tenzi za rohoni ambazo zinaweza kuongozwa na Roho katika lugha mpya anazotupatia Yeye. Kwahiyo mikutano mingi ya kisasa haina tofauti sana na burudani za kikristo kama kwenye kumbi za starehe. Watu huwa wanaangalia tu, lakini je, wanaabudu? Uwepo wa Mungu na Roho wake katika ibada zetu utawafanya watu wasioamini kuanguka chini na kuabudu (Kol 3:16) (1Kor 14:15,16,25,26) (Efe 5:19) (Mdo 2:4).
  Je, Kusifu Na Kuabudu Ni Kitu Kilekile?
  Tunapaswa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo na kwa matendo yake; lakini Mungu mwenyewe anawatafuta na anawataka wafanya ibada, na si mradi ibada tu.
  Kusifu kwaweza kufanywa hadharani, lakini ibada mara zote ni jambo la ndani ya moyo.
  Kusifu mara zote kunaweza kuonekana au kusikika, lakini ibada yaweza kuwa ya kimyakimya na iliyofichika.
  Kusifu kunaonekana, kuna kutumia nguvu, kuna misisimko na furaha; lakini ibada mara zote ni heshima na hofu katika uwepo wa Mungu.
  8. Ibada Ya Kweli Ina Gharama
  Biblia inazungumzia habari za sadaka za kusifu. Daudi alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, na akakataa kumtolea Mungu kafara ambayo isingemgharimu cho chote (2Sam 6:14; 24:24). Wale mamajusi wa Mashariki walitoa zawadi za gharama kubwa walipokuja kumwabudu Yesu (Mt 2:9-12), na mwanamke mmoja alimpaka Yesu kwa mafuta ya gharama kubwa, akamwosha miguu yake kwa machozi yake, na kuifuta kwa nywele zake (Lk 7:36-50).

  iwapo mungu atakufunulia ufahamu wa kujua baadhi ya mambo hapo juu hakuna ubishi utajua umuhimu wa dhaka na sadaka zake....
   
Loading...