Kakobe: Hatuchagui malaika bali Rais; afuta Ibada za FGBF siku ya uchaguzi

kama mtu anataka kupiga kura anaweza tuu, KKKT na RC wana misa nyingi sana (tatu nakuendelea) na kila misa haichukui zaidi ya masaa 2 na zinaanza 12 asubuhi, so kusali sio kigezo labda kwa hao wanaosali asubuhi mpaka jioni
Nimekusoma. naamini watu wa kila kada watahamasishwa kupiga kura. Sipati picha watakaokuwa safarini siku hizo tutakosa kura zao
 
Kakobe...safi sana.
Kikwete na serikali yake walitaka kutudhulumu haki yetu hii ya msingi.
nadhani kuna watu wanafurahi wakristo wengi wasipige kura, safari hii tumefanya juhudi nyingi; lakini nec imeng'ang'ania, na hatuwezi kuacha kwenda kupiga kura kwani tunaweza kuchaguliwa kiongozi asiyefaa tukajutia kwa miaka mitano.

"hivyo natangaza rasmi siku hiyo ya uchaguzi hakutakuwa na ibada katika makanisa yote ya fgbf, milango ya makanisa hayo siku hiyo ifungwe na ibada ya siku hiyo ifanyike siku ya jumamosi," alisema askofu huyo.
 
Kakobe anazidi kuzihirisha kuwa ni askofu mwenye karama ya mfalme suleimani. Nakumbuka kile kisa cha wanawake wawili ambao mmoja wao alifiwa na mtoto. Kakobe anawafuasi kama 2M tanzania nzima najua watu hawatakubaliana na mimi!
 
KAKOBE ATEMA CHECHE KANISANI

1.jpg

Kikundi cha kwaya cha kanisa hilo kikiwa katika maombi maalum kwa ajili ya kuliombea taifa leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe amesema kuwa Oktoba 31, mwaka huu ambayo ndiyo siku ya kupiga kura kuwachagua rais, wabunge pamoja na madiwani itakuwa ni Jumapili, siku ambayo waumini wengi watakuwa makanisani.

Kwa upande wa kanisa lake, Kakobe amesema kuwa watafanya ibada siku moja kabla ya uchaguzi ili kutoa nafasi kwa waumini wake nchi nzima kwenda kupiga kura asubuhi na mapema.

2.jpg

Wazee wa kanisa hilo nao hawakuwa nyuma katika kusali kwa pamoja wakilenga uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu.

3.jpg

Hizi ni pikipiki ambazo hutumiwa na waumini wa kanisa hilo hasa viongozi zikiwa zimepaki nje ya kanisa hilo.

4.jpg

Waumini wa kanisa hilo wakiwa kwenye maombi maalum.
 
Kinachomata ni kwenda kupiga kura. Haijarishi ni mda gani!! Inatakiwa tuwe na desturi ya kupanga mida yetu, mtu anaweza kwenda kanisani kusari na harafu akarudi kupiga kura, au kama ibada ni ndefu saana (siamini kama kuna ibada ya zaidi ya kutwa nzima) ndipo mtu mwenyewe aschedule mda wake ili mradi tu akapige kura.
 
Safi Kakobe, kupiga kura na kuchagua kiongozi aliye bora kwa maslahi ya raia hata hiyo ni Ibada.
 
Kakobe anazidi kuzihirisha kuwa ni askofu mwenye karama ya mfalme suleimani. Nakumbuka kile kisa cha wanawake wawili ambao mmoja wao alifiwa na mtoto. Kakobe anawafuasi kama 2M tanzania nzima najua watu hawatakubaliana na mimi!

Chaguzi zote tangu uhuru zinafanyika Jumapili na waumini wa RC, KKKT na Anglican pote nchini wanapata muda wa kusali na kwenda kupiga kura bila shida. Makanisa mengi yana misa kama tano, nyingine za Jioni zinaanza saa 10. Kakobe alihitaji kufanya hivyo kwa kuwa ibada zake zinachukua siku nzima.


Kwamba ana karama kama ya mfalme Sulemani, inaonesha you are brainwashed by him. Na bila shaka wewe ni mfuasi wake, twakuomba usipige propaganda hapa, sio mahali pake. Sio wote tunamwona hivyo!
 
kakobe1.jpg

Askofu mkuu wa kanisa la (FGBF),Zachary Kakobe

Waandishi Wetu


ASKOFU mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe jana aliamua kutoa darasa la elimu ya urais kwa waumini wake na kuwataka kutompima mgombea kwa kuangalia matukio kwenye maisha yake ya ndoa.

Kakobe, ambaye aliwahi kumpigia debe Augustine Mrema wakati akigombea urais kwa tiketi ya TLP kabla ya kugeuka na kuisifu CCM, alisema maneno hayo jana wakati akihubiri kwenye ibada iliyofanyika kwenye kanisa lake lililo Mwenge, jijini Dar es salaam.

Pamoja na kutotaja jina, mahubiri ya kiongozi huyo shupavu wa kidini yalionekana kumgusa mgombea urais wa Muungano kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa ambaye amekumbwa na tuhuma za masuala ya maisha yake ambazo zimefika mahakamani ambako anadaiwa fidia kwa madai ya kumtangaza mke wa mtu kuwa mchumba wake.

Dk Slaa, ambaye anawania kuwa mgombea wa kwanza kutoka nje ya CCM kuingia Ikulu baada ya utawala wa miaka 49 wa chama hicho kikongwe, amesema yuko tayari kupambana na mashtaka hayo mahakamani na anaendelea kuzunguka na mwanamke huyo kwenye mikutano yake ya kampeni.

Lakini Kakobe aliwaambia waumini wake kuwa masuala kama hayo yameshawakumba viongozi wengi wa barani Afrika na Ulaya lakini waliongoza mataifa yao kwa ufanisi na kuwa na maendeleo hadi leo, akisema huo ni mfano wa kuigwa kwenye nchi zinazoendelea.


Kakobe, ambaye jana alitangaza kufuta ibada zote zilizopangwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu ili kutoa fursa kwa waumini wake kushiriki uchaguzi mkuu, hakumtaja Dk Slaa kwa jina wakati akihubiri lakini alitumia mifano ya viongozi mbalimbali waliowahi kukumbwa na kashfa hizo lakini wakapewa dhamana ya kuongoza nchi zao.

"Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela alikuwa na kashfa ya kuoa na kuacha na hadi sasa mke wake anayeishi naye ni wa tatu, lakini pamoja na kashfa hizo wananchi wake walimkabidhi nchi na amefanya maajabu na kuifanya nchi hiyo kuaminiwa na mataifa makubwa na hata kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia," alisema Kakobe.

Mbali na huyo pia alimtaja rais wa sasa wa nchi hiyo, Jackobo Zuma kuwa alikumbwa na kashfa ya kumbaka mwanamke aliyekuwa na Ukimwi kabla ya uchaguzi, lakini wananchi hawakuangalia hayo na badala yake waliona kuwa ana kipaji cha uongozi wakamchagua.

Pia alimtaja rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy aliyedai naye alikuwa na kashfa kuoa na kuacha na hata mke wake wa pili alikuwa mke wa mtu, lakini alioa na kuzaa naye mtoto mmoja halafu wakaachana na sasa mwanamke huyo ameolewa nchini Marekani.

Alisema pamoja na kashfa hizo wananchi wa nchi hizo hawakuangalia hayo na badala yake waliwachagua na kuwapa mamlaka ya kuwatumikia na wakafanya vizuri.

Ufafanuzi huo uliwafanya waumini hao kushindwa kujizuia na kushangilia licha ya Kakobe kuzuia watu kufanya hivyo ili anachokizungumza kiweze kueleweka miongoni mwao.

Kuhusu umuhimu wa kupiga kura, Askofu Kakobe alisema hiyo ni haki na wajibu wa kila raia na kusisitiza hata Mungu anataka watu kujichagulia viongozi wao.

Kutokana na msingi huo wa kutambua umuhimu kwa uchaguzi, kanisa hilo limefuta ibada za siku ya Oktoba 31 ili waumini wake wakapige kura na kwamba ibada hiyo sasa zimehamishwa Oktoba 30.

Alisema uamuzi huo unatokana na vikwazo kadhaa vinavyowakwamisha wakristo wengi nchini kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi kutokana na siku hiyo kuangukia Jumapili ambayo siku ya ibada kwa baadhi ya makanisa ya Kikristo.

"Natangaza rasmi kufunga ibada za kanisa hili nchi nzima Oktoba 31 mwaka huu. Siku hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya uchaguzi mkuu kutokana na umuhimu wa kuchagua viongozi wanye sifa za kuongoza taifa hili," alisema Kakobe.

Katika ibada hiyo Kakobe alitaja vikwazo vitano vya kitaifa vinavyosababisha watu wengi kushindwa kushiriki katika kupiga kura huku akidai vikwazo viwili vinawahusu wakristo pekee.

Alivitaja vikwazo hivyo kuwa ni dhana ya baadhi ya waumini kuamini kuwa viongozi huchaguliwa na Mungu hivyo kutoshiriki katika upigaji kura, hali aliyosema inachangia kupatikana kwa viongozi wabovu.

Alitaja vikwazo vingine kuwa ni dhana potofu ya baadhi ya wapiga kura ambao hudai kura moja haiwezi kubadili matokea; hofu ya kuibiwa kura na imani ya baadhi yao kuwa hata ukichagua viongozi wengine hali haiwezi kubadilika.

"Dunia ya sasa inazungumzia maendeleo na ndiyo maana mataifa yametengwa katika mafungu matatu, maendeleo katika nchi huletwa na kiongozi bora kwa kuwa kiongozi ni kama dereva mkipata dereva rafu atapitisha gari hata kwenye mashimo na mkipata dereva safi ataifikisha gari mahali panapotakiwa kwa usalama," alisema.

Kwenye mahubiri hayo ambayo Kakobe aliita ni elimu maalum ya urai kwa waumini wake na wa madhehebu mengine, aliwataka wakristo kutochagua viongozi kwa vigezo vya Biblia au uumini wao bali waangalie uwezo wao wa utendaji katika kusimamia misingi ya katiba.

"Kwenye uchaguzi mkuu hatuchagui malaika wa kutupeleka mbinguni bali kiongozi wa kuliongoza taifa... tuchague kwa kufuata kanuni na taratibu za katiba, kwa kuwa viongozi wote wana sifa, kinachotakiwa ni kuangalia nani ana kipaji cha uongozi," alisema Kakobe.

Kakobe aliwataka wakristo kuhudhuria kwenye kampeni na kusikiliza sera za vyama ili kubaini ahadi na kuzifanyia utafiti kabla ya uchaguzi.

"Wapo wanaosema msichague viongozi kwa majaribio chagueni wazoefu, hizi ni siasa nyepesi... nani kakwambia Ikulu panahitaji uzoefu? Nelson Mandela alipata wapi uzoefu; Barrack Obama amekuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani, amepata wapi uzoefu," alihoji Kakobe na kuongeza kuwa anayekataa mabadiliko anakataa maendeleo.

Alisema kila kitu duniani chenye mafanikio huanza kwa majaribio akitoa mfano wa wanasanyansi ambao alisema hawawezi kuruhusu kufanyika kwa kitu bila majaribio.

Chanzo: Kakobe ajitosa kwenye kampeni
 
jee kujitokeza tena kumuunga mkono dk slaa kwa madai ya elimu bure na matibabu bure huku ahadi kama hiyo ikitolewa na lipumba ya elimu bure tena hadi chuo kiku na afya bure

Itakuwa huyu Kakobe ni mchaga si bure au sio MS?
 
Wakristo wa kweli hawapigi kura, maana vita yao si ya nyama wala damu, wala si ya dunia hii.
 
Wakristo wa kweli hawapigi kura, maana vita yao si ya nyama wala damu, wala si ya dunia hii.

Our culture has a shrinking preference--and even aptitude--for reading books, especially complex ones. The Bible is complex, so we should not be surprised to see a growing biblical illiteracy in the electronic age.
 
Kakobe...safi sana.
Kikwete na serikali yake ya kiislam walitaka kutudhulumu haki yetu hii ya msingi.

Mkuu, hii ya kuiita serikali ya JK ya kiislam hapana. Haikubaliki. Acha udnini.

Cha msingi, siku ya kupiga kura ibadilishwe na kuwa neutral for all!!
 
Katetea WAZINZI wote MAARUFU duniani. Kamsahau Mswati, Bill Clinton, JK, David Blunket, Wayne Rooney, John Terry, Juma Kaseja, Kitwana Kondo,......!
 
Siasa kuzungumzwa Makanisani poa kabisa, misikitini ni "kuchanganya dini na siasa" fungeni makanisa yote tarehe 31 Oct lakini huyo Padri wenu Ikulu ataiona paa!
 
wakristo wa kweli hawapigi kura, maana vita yao si ya nyama wala damu, wala si ya dunia hii.
please do not quote the bible out of context. Kama hujui biblia kaa kimya sio kuibua mstari usiohusiana na uchaguzi na kuubandika kwenye maswala ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom