Kakobe asalimu amri kwa serikali

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Lile sakata la kupitisha umeme mbele ya kanisa la Mch. Kakobe hatimaye linaonekana limefikia tamati baada ya waumini waliokuwa wanalinda kanisa hilo usiku na mchana kwa siku zote toka sakata hili lilipoanza kutawanyika rasmi hivyo kupisha njia kwa TANESCO kuendelea na mradi wao, hiyo ndiyo taswira iliyopo kanisani hapo leo asubuhi kwani hakuna 'mlinzi' hata mmoja anayeonekana.,inasemekana hii ni kutokana na kauli ya serikali iliyotolewa na waziri husika jana.
 
Kama madhara hakuna acha kazi ziendelee!!! Ila what I know huwezi kushindana na serikali
 
People, u have to talk MATERIAL, na sio porojo!

Ongeeni kilichotokea, na si kuripoti tu vitu pasi na kufanya rejea!

Kwa waliokuwa makini kufuatilia hili suala, Kakobe amesimama Firm KABISA kutetea maslahi ya kanisa lake hadi dakika ya mwisho ambapo MUAFAKA umefikiwa kati yake na Waziri Ngeleja.

Actually hii ndo SPIRIT ambyo Wabongo wote tunatakiwa kuwa nayo kila uchao.
Kakobe ameweza kuwa na Msimamo wa juu kabisa na kuifanya serikali ifikirie mara ya pili, na hatimaye kutuma ujumbe wake ukiongozwa na waziri!...Hata hivyo, waliotazama mchakato huo siku hiyo, ni kwamba ilibidi waziri na Kakobe waingie mahali pa faragha ili kuongea kwa ukaribu kabisa, ndipo muafaka ulipatikana!

Mikataba ya kishenzi inaingiwa na serikali, wabongo kimyaaa!
Watu wanachukua vijisenti serikalini, wabongo kimyaa, mbaya zaidi wanawalaki watu hao wezi kama mashujaa!

KAKOBE umeonyesha kwamba mambo haya yanawezekana, na serikali iko kwaajili ya kuwatumikia watu kwa njia ya kusikilizana nao, na si kuwaburuta!
BIG-UP KAKOBE!
 
Muafaka gani ulifikiwa wakati imethibitika Kakobe alitoa vipimo visivyo sahihi? Au alitaka kukutana tu na waziri kupiga nae stori?
 
Back
Top Bottom