Kakobe apinga waraka wa wakatoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe apinga waraka wa wakatoliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HM Hafif, Sep 3, 2009.

 1. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na Waandishi Wetu

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe amemhisi Rais Jakaya Kikwete, kuvunja ukimya na kuzima mijadala kuhusu nyaraka za kidini, inaoendelea nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Askofu Kakobe alisema nyaraka hizo zinaelekea kuwagawa watu na hatua zisipochukuliwa, zinaweza kusababisha vita ambavyo havitakwisha.

  “Rais wetu ni mpole sana, mcheshi na ni mtu wa watu, hilo si tatizo kubwa kwake, lakini ukiwa na rais mpole sana ni tatizo, hata ukiwa mkali sana ni tatizo pia, namhisi hili aliingilie kati,” alisema Kakobe.

  Kakobe alisema baadhi ya viongozi wa kisiasa, wamekuwa wakiogopa kukemea vitendo vinavyofanywa na viongozi wa dini kwa sababu tu wanawaogopa.

  “Napenda kusema kuwa, viongozi wa kisiasa kunyamazia maovu yanayofanywa na viongozi wa dini kwa sababu tu kuwaogopa, kunaweza kuwaingiza watu wote kwenye uovu,” alionya Kakobe.

  Mbali na hayo Kakobe amepinga vikali tamko la kiongozi mmoja wa kanisa aliyejibu hoja ya kiongozi mmoja wa kisiasa aliposema wanasiasa hawawezi kuwafundisha kazi maaskofu.

  “Nichukue nafasi hii kukemea vikali tamko la kiongozi mmoja wa dini, ambaye alitamka rais akiwa jukwaani kwamba wanasiasa hawapaswi kutufundisha wachungaji. Alitamka maneno hayo kwa jeuri, kuonesha kabisa ana msimamo usioyumba na hataki kushauriwa,”alisema Kakobe.

  “Kama tunasema maadili ya viongozi wa serikali yamemomonyoka wa kwanza kukemewa ni viongozi wa dini kwa sababu wao ndio chanzo kikubwa,” alisisitiza.

  Pia Kakobe alimpongeza mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, kwa hatua yake ya kuupinga hadharani, waraka wa Kanisa Katoliki na kwamba kiongozi huyo, anaona mbali.

  Alisema kwa huyo hiyo, mzee Kingunge amedhihirika kuwa hata watu wasio na dini, wanaweza kuongoza vizuri.


  Habari imendikwa na Hussein Kauli, Levina Chengula na James Magai

  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli mchungaji Zacharia kakobe umenena.

  Nakupa tano mkuu
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  We huoni anajigonga gonga? kaanza vizuri kuongea mwishoni kaharibu!!
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Inanikumbusha suwala lililoulizwa hapa jamvini eti ..".kwanini BAKWATA wanaupinga waraka wa Maimamu".
  Isipokuwa sina budi kukiri kuwa KAKOBE ana point lakini BAKWATA wanatafuta favour kwa Serikali.
   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimependa sana maneno hayo ya Askofu.
   
 6. K

  Kadudu Member

  #6
  Sep 3, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kakobe hajasoma huo waraka,angesoma angeona kuwa unaelekeza jinsi ya kuchagua viongozi wasio MAFISADI.Vinginevyo naye atakuwa sehemu ya hao MAF.........kama anavyofanya yeye kwa kuwaregister waamini wake wanapata shilingi ngapi hata kama anauza mihogo mitaani kariakoo
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani mbona sisi ni watu wa kusahau kirahisi?! Juzi juzi tu Kakobe amenukuliwa na magazeti nchini akihamasisha watanzania tususie uchaguzi wa serikali za mitaaa na baadee uchaguzi mkuu na sikuona hata comment moja toka serikalini au kwa wanaharakati. Leo hii waraka wa wakatoliki unaowaelimisha wananchi kuchagua viongozi bora imekuwa nongwa? Nani mchochezi kati ya Kakobe anayewambia wananchi kususia uchaguzi au waraka unaotoa elimu ya uraia? Labda niulize swali. Kama ingekuwa ni Kardinali Pengo amesema wananchi wasusie uchaguzi mwaka huu na 2010, reaction ingekuwaje? Si angeitwa mhaini? Mbona Kakobe haijaitwa hivyo? Why should people see a "snake" in every little shrub?

  Anachoifanya Kakobe ni opportunist ya hali ya juu. kama alivyosema Askofu Kilaini leo Kanisa Katoliki na Kakobe ni paka na chui kwa hiyo Kakobe amepata mwanya wa kuleta uchonganishi tu kati ya Pengo na serikali. Hata hivyo nina imani kanisa litampuuza na hakuna haja ya kuendelea na malumbano kwa sasa.
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Amenena ili na yeye aonekane yupo...
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kakobe ni sawa na jambazi tu, hata wanaabudu ktk kanisa lake nina wasiwasi nao. Dhahabu alizokuwa anakusanya amepeleka wapi? kwanza anatakiwa ashitakiwe.

  Hata siku moja mhuni kama kakobe hataweza kujilinganisha na Pengo mpaka atakufa, wala hiyo FGBF haitaweza kuifikia RC mapa mwisho wa dunia. Wataishia kupora sadaka za waathirika na wagonjwa wengine tu, na hii ni dhambi.

  Huwezi kuwa na akili timamu ukaenda kuabudu kwa kakobe, labda uwe mgonjwa na umekata tamaa ya kuishi.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kwanza kakobe ni darasa la ngapi mpaka akosoe waraka ulioandaliwa na wataalam waliobobea?

  Nakumbuka wakati anauza kanda za nyimbo pale temeke, sijui kama alienda shule zaidi.
   
 11. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari za shughuli wana JF. Nimesoma habari ya huyu bwana Askofu kuhusu waraka wa wakatoliki nimebaki kujiuliza kama huyu Askofu ameenda shule au laa. Fikiri mtu anayejiita askofu anapoteza muda wake kuwakalisha waandishi wa habari kujadili jambo ambalo kurasa zake zilishafungwa. Je anataka kujiosha kwa JK? Mtakumbuka wakati wa Mkapa alimuunga mkono sana mzee wa Kiraracha na kuikandia sana serikali ya Mkapa. Leo hii namshanga kukandia waraka ambao unawaelimisha wananchi wote na siyo wakristu tu kiongozi anayefaa kuchaguliwa. Najiuliza kama ameenda shule kwa sababu mtu aliyeenda shule akiusoma waraka husika hawezi kuukandia hata kidogo. Jambo la kushangaza amekaa muda mrefu sana tangu waraka huu utoke bila kusema chochote ndo anakumbuka shuka wakati kumekucha na mbu wameshamtafuna kisigino. Nawaomba waumini wake wale wasomi wamshauri asiwe anazungumza na waandishi wa habari bila kushauriana na wasomi kwa maana naamini atakujaishia pabaya. Anaweza kujilinganisha na Pengo mwenye PhD na anayefikiri kabla ya kusema ama kutenda. Aende shule kwanza huyu ndo ajiite askofu.Anasema anachukua nafasi ya waandishi wa habari kumkemea Pengo kwa kuthubutu kutamka bila woga mbele ya Rais kuwa kuwa wanasiasa hawawezi kufndisha wachungaji kuhusu nyaraka zao. Je hii si kweli? Kama ni kweli kwa nini ajifarague mbele za watu? Naamini ni ujinga na umemtawala na kutojua wajibu wake kama mchungaji mbele ya wanasiasa. Aache kuficha madhambi yake kwa kujipendekeza kwa Rais. Hebu tujadili jambo hili kwa wale wenye nafasi. Karibuni.
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hana lolote
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Atakuwa hajasoma waraka,kasikiliza tu malumbano.Hajatuambia kama alishatubu alipowadanganya watz kwa mrema ni chaguo la mungu.Mapepo tu tamemjaa......
   
 14. K

  Kadudu Member

  #14
  Sep 3, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  alipokosa dili la kuuza kanda za ASSMBLESS OF GOD KARIAKOO ndio akaamua kujitoa na kuanzisha DHEHEBU lake linalokataliwa na Viongozi wengine wa dini
   
 15. M

  Mchili JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kakobe sasa anatapatapa, tumweke upande gani?

   
 16. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  sipendi kuwazungumzia watumishi wa mungu lakini hili la Kakobe nitalizungumzia. Kakobe anapenda kuja na vitu contraversial ili kutafuta attention n
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Uovu uliopo katika waraka wa RC upo wapi? mbona hajautaja?
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kuna nyeti kuwa huyu bwana Kakobe ni msilamu, na jina lake ni Zahoro. Hivyo sistushwi saaana na sarakasi zake. Tutegemee kuona mengi kabla ya 2010.
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Kwanza hao waandishi wameishia darasa la ngapi? mara mbili wameandika amemhisi badala ya amemsihi...maana mbili tofauti kabisa!

  Pili, kakobe anajulikana, wala watu wenye akili zao hawawezi kupoteza muda kumsikiliza. Ndo maana anamsifia Kingunge. Ni opportunist tu hana lolote, anatafuta attention
   
 20. N

  Ndaga Senior Member

  #20
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 164
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Magezi,
  Angalia hayo maneno highlighted;Toa hoja,usitukane,tujadili hoja ya Kakobe!Je viable? au ina utata gani? usiwe na hasira.
   
Loading...