Kakobe: Acheni Siasa za Chumbani, Siasa za Haramu

RIGHT

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
252
100
Akihubiri katika Ibada ya Christmas kanisani Mwenge, Mtumishi wa Mungu Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship alisema kuwa wametokea baadhi ya wanasiasa hapa nchini ambao wanajiona ni miungu watu na kujaribu kuwazuia watu wengine hususani viongozi wa dini wasiongelee mambo ya siasa kwa kigezo kwamba eti Biblia inasema ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu, hivyo viongozi hao wa dini hawastahili kuongelea au kujihusisha na mambo ya siasa. Akitolea ufafanuzi maneno hayo alisema watu hao hawajui Biblia na wanajaribu kuwapotosha watu. Alisema Yesu aliwajibu wanafunzi wake baada ya kuulizwa juu ya uhalali wao (wanafunzi) wa kulipa kodi ya Kaisari wakati wao waliamriwa na Musa kulipa kodi ya Mungu. Ndipo akawajibu kwamba ya Kaisari wampe Kaisari na ya Mungu Wampe Mungu akimaanisha kwamba walipe kodi ya Kaisari na walipe kodi ya Mungu pia kama walivyo amriwa (Luka 20: 21-25; Hesabu 31: 25-39). Hivyo yeye kama mtumishi wa Mungu hawezi kuacha kukemea mahali penye uovu na atapongeza panapostahili kupongezwa.

Viongozi wa nchi na Rasilimali zetu.

Aliendelea kusema kuwa Tanzania ni nchi iliyo barikiwa sana kwa kuwa na Rasilimali nyingi lakini wananchi wake ni maskini. Alisema, hii inatokana na kuwa na viongozi ambao hawana maono ya kuwaletea wananchi maendeleo badala yake wao wanajiangalia wenyewe na familia zao. Akasema ndio maana mtu akipata uongozi anasema "ameula". "Kiongozi bora ni yule mwenye kipaji cha kuzaliwa cha uongozi na sio vyeti vya darasani pekee. Sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa nchi, ni lazima tuhakikishe tunamchagua kiongozi ambaye ana maono ya kututoa kutoka katika Umaskini tulionao na kuleta maendeleo ya kiuchumi".

Siasa za chumbani, siasa haramu.
Askofu Kakobe aliwataka wanasiasa na wananchi kwa ujumla kudumisha umoja wetu badala ya kuleta siasa za chuki. Alisema wako baadhi ya wanasiasa ambao wamechoka kisiasa hivyo wanaleta propaganda za udini, ukabila na ukanda. "Watu wanadiriki hata kusema chama fulani ni cha dini fulani, eti hatutaki Rais atoke ukanda fulani. Hizi ni siasa haramu na wanaoeneza propaganda hizo nao ni haramu".

Aliendelea kusema kuwa hatumchagui mtu au malaika wa kutupeleka Mbinguni bali mtu wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa kwa faida ya wananchi wote. Aliwaasa wanasiasa waache siasa za chumbani za kunyoosheana vidole kuhusu ndoa zao. "Tusiendekeze siasa za chumbani,hatumchagui kiongozi wa kutupeleka mbinguni bali tunamchagua kiongozi wa kutuletea neema hapa hapa Tanzania. Watu leo wanamsifia Mandela kwamba alikuwa kiongozi bora lakini wanasahau kwamba Mandela huyuhuyu maisha yake ya ndoa yalikuwa na kasoro kubwa. Aliweza kuwasamehe makaburu lakini alishindwa kumsamehe mkewe Winnie. Ni nani Kiongozi wa nchi hapa Tanzania anaweza kusema yeye ni msafi? Kwani sisi atujui maisha ya JK? Tuache siasa za chumbani, tuchague kiongozi bora.

Pia Askofu Kakobe alishauri Chama Tawala kikubali uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuondoa malalamiko toka kwa vyama vya upinzani. Pia alishauri siku ya uchaguzi mkuu isiwe Jumapili, Jumamosi au Ijumaa bali serikali itenge siku yoyote katikati ya wiki ili wananchi wengi zaidi waweze kujitokeza kupiga kura.

N.B:Tunaweza kujadili maoni ya huyu mtumishi wa Mungu kwa mustakabali wa Taifa letu.
 
Anapomzungumzia kiongozi bora mwenye maono ya nchi hapa anamaanisha ZZK.
Kiongozi mwenye maono ni yule anayejadili changamoto zinazo likabili taifa na namna ya kuziondoa,kiongozi asiye na maono yeye focus yake ni kuwa rais na kuingia Ikulu hata akipata nafasi hiyo hajui aanzie wapi aelekee wapi hatutarudia makosa hayo.
 
Haswa, Hapo umenena.
 
kama ungeweza kumshauri agombee urais, naamini angetuondolea umaskini, kwani maoni yake yanatosheleza
 
Alisema kazi aliyo nayo ya kumtumikia Mungu inamtosha. Lakini akiwa kama mtumishi wa Mungu na raia wa nchi hii hataacha kutoa maoni, kukemea na kupongeza wakati anapohitajika kufanya hivyo.
 
Hotuba isiyo na Chembe ya Shaka Siku zote hutolewa na watu makini....asante Baba Askofu Kakobe.
 
Kakobe ni mmoja wa viongozi adimu wa dini ambao ni jasiri katika kukemea,kuonya na kushauri bila kupindishapindisha mambo
 
Hii ndio hekima nani asijeyua maisha ya Jk?rais ata kututumia wananchibwake heribya sikukuu asemi yeye yupo USA Anapimwa afya sasa kwa taarifa tangu Jk awe rais amesha kwenda safari zaidibya 380
 
Back
Top Bottom