Kakobe: Acheni Siasa za Chumbani, Siasa za Haramu

Kiongozi anapozungumzia jambo ni vyema akajitazama mwenyewe kwanza kwa wanaomfahamu Kakobe ni mtu alieanza shughuli za kwa kuuza kanda za kaset pale Temeke mwisho akiwa na studio yenye jina la Edition Mlanga

Baada ya hapo ndipo alipobadilisha biashara na kuingia katika dini ambayo imemletea utajiri mkubwa mpaka sasa watoto wake wanasoma Marekani.

Suala la kujiuliza utajiri aliokuwa nao ameupata wapi na kwa nini asitumie utajiri huo aliokuwa nao kuwaendeleza hata waumini wake tu.

Kama kweli anauchungu na wananchi wa taifa hili badala yake anawachangisha michango mpaka mara nyingine wanakosa nauli ya kurudi majumbani kwao mara ngapi tunawapa lift waumini wake pale Mwenge.

ACHENI UNAFKI VIONGOZI WETU WA DINI MUOGOPENI MUNGU MNAYOYAFANYA NI ZAIDI YA WANA SIASA.
 
Kiongozi anapozungumzia jambo ni vyema akajitazama mwenyewe kwanza kwa wanaomfahamu Kakobe ni mtu alieanza shughuli za kwa kuuza kanda za kaset pale Temeke mwisho akiwa na studio yenye jina la Edition Mlanga

Baada ya hapo ndipo alipobadilisha biashara na kuingia katika dini ambayo imemletea utajiri mkubwa mpaka sasa watoto wake wanasoma Marekani.

Suala la kujiuliza utajiri aliokuwa nao ameupata wapi na kwa nini asitumie utajiri huo aliokuwa nao kuwaendeleza hata waumini wake tu.

Kama kweli anauchungu na wananchi wa taifa hili badala yake anawachangisha michango mpaka mara nyingine wanakosa nauli ya kurudi majumbani kwao mara ngapi tunawapa lift waumini wake pale Mwenge.

ACHENI UNAFKI VIONGOZI WETU WA DINI MUOGOPENI MUNGU MNAYOYAFANYA NI ZAIDI YA WANA SIASA.

Hakika wewe ndiye unaye stahili kumwogopa Mungu kwa kusema uongo. Alikwisha tangaza kitambo tu kwamba yeyote anayejua mali alizonazo zaidi ya nyumba anayoishi sasa ajitokeze na kusema, hakuna hata mmoja,hata wewe umekaa kimya. huo utajiri ni wa kufikirika?

Lakini pia inawezekana kuna Kakobe mwingine ambaye wewe unamjua. Huyu tunayefahamu sisi ana kanisa lake pale Mwenge, watoto wake wote wapo hapa Dar, anaishi nao, na tunawafahamu kwa majina. Uwe umdadisi kidogo basi utajua mengi badala ya kulishwa maneno.
 
Katika salaam zake za Christmas jana katika Kanisa la F.G.B.F, Mwenge, Dar es Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe amezungumza kwa takribani saa mbili nzima mambo mazito sana kuhusu Uchaguzi Mkuu, Tume huru ya Uchaguzi, Ukabila na Ukanda, kufukuza viongozi katika vyama vya siasa na Serikali na mambo mengine mengi kuhusu mustakabali wa Taifa na mambo ya Kiroho. Kalamu na wino havitoshi kuyaandika. Tafuta wasaa wa kusikia hapa unedited full version ya mahubiri yake ya Christmas.

 
Last edited by a moderator:
Katika salaam zake za Christmas jana katika Kanisa la F.G.B.F, Mwenge, Dar es Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe amezungumza kwa takribani saa mbili nzima mambo mazito sana kuhusu Uchaguzi Mkuu, Tume huru ya Uchaguzi, Ukabila na Ukanda, kufukuza viongozi katika vyama vya siasa na Serikali na mambo mengine mengi kuhusu mustakabali wa Taifa na mambo ya Kiroho. Kalamu na wino havitoshi kuyaandika. Tafuta wasaa wa kusikia hapa unedited full version ya mahubiri yake ya Christmas.





Kweli jf ni kisima cha taarifa, ni zaidi ya habari.
 
Last edited by a moderator:
DAH ...
Kwa hiyo Kakobe naye kaamua Kuungana na zito ?

Siasa za chumbani ndio zipi ?

Au ndio yale tuliyoambiwa ....CHADEMA CHUMBANI NA CHADEMA SEBULENI
 
Tz ina hazina ya watu wenye hekima aina ya Bishop Kakobe,serikali inatakiwa kuomba ushauri kwao.hongera mtumishi wa Mungu
 
Yes,tujadili. Na mimi naanza kwa kusema HONGERA ZCHARIA KAKOBE na mimi naongeza kama ifuatavyo;

Akihubiri katika Ibada ya Christmas kanisani Mwenge, Mtumishi wa Mungu Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship alisema kuwa wametokea baadhi ya wanasiasa hapa nchini ambao wanajiona ni miungu watu na kujaribu kuwazuia watu wengine hususani viongozi wa dini wasiongelee mambo ya siasa kwa kigezo kwamba eti Biblia inasema ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu, hivyo viongozi hao wa dini hawastahili kuongelea au kujihusisha na mambo ya siasa. Akitolea ufafanuzi maneno hayo alisema watu hao hawajui Biblia na wanajaribu kuwapotosha watu. Alisema Yesu aliwajibu wanafunzi wake baada ya kuulizwa juu ya uhalali wao (wanafunzi) wa kulipa kodi ya Kaisari wakati wao waliamriwa na Musa kulipa kodi ya Mungu. Ndipo akawajibu kwamba ya Kaisari wampe Kaisari na ya Mungu Wampe Mungu akimaanisha kwamba walipe kodi ya Kaisari na walipe kodi ya Mungu pia kama walivyo amriwa (Luka 20: 21-25; Hesabu 31: 25-39). Hivyo yeye kama mtumishi wa Mungu hawezi kuacha kukemea mahali penye uovu na atapongeza panapostahili kupongezwa.

Viongozi wa nchi na Rasilimali zetu.

Aliendelea kusema kuwa Tanzania ni nchi iliyo barikiwa sana kwa kuwa na Rasilimali nyingi lakini wananchi wake ni maskini. Alisema, hii inatokana na kuwa na viongozi ambao hawana maono ya kuwaletea wananchi maendeleo badala yake wao wanajiangalia wenyewe na familia zao. Akasema ndio maana mtu akipata uongozi anasema "ameula". "Kiongozi bora ni yule mwenye kipaji cha kuzaliwa cha uongozi na sio vyeti vya darasani pekee. Sio kila mtu anaweza kuwa Rais wa nchi, ni lazima tuhakikishe tunamchagua kiongozi ambaye ana maono ya kututoa kutoka katika Umaskini tulionao na kuleta maendeleo ya kiuchumi".

Nani wengine sasa? Ni CCM hakuna wengine,hakuna viongozi huko....Serikali yote ni MZIGO WA MAGUNIA YA MISUMARI na wala hakuna cha mawaziri sita,kumi,wanne au mmoja.Narudia tena serikali yote CHINI YA
CHAMA CHA MIZIGO NI MZIGO tuliokwisha kuchoka kuubeba wananchi,watazania!!

Usije shangaa Kakobe kanisa lako kufungiwa kwa madai kuwa halina usajili,au (hulipi kodi?).....Kisa? Kwa sababu masultani wa
CCM hawa hawataki kuambiwa ukweli.hawataki kukosolewa,hawataki kuambiwa kwamba walishashindwa.......na sasa wanaoweza wameshapatikana!!


Siasa za chumbani, siasa haramu.
Askofu Kakobe aliwataka wanasiasa na wananchi kwa ujumla kudumisha umoja wetu badala ya kuleta siasa za chuki. Alisema wako baadhi ya wanasiasa ambao wamechoka kisiasa hivyo wanaleta propaganda za udini, ukabila na ukanda. "Watu wanadiriki hata kusema chama fulani ni cha dini fulani, eti hatutaki Rais atoke ukanda fulani. Hizi ni siasa haramu na wanaoeneza propaganda hizo nao ni haramu".

Duuh, askofu hapa ni Bonge la nail la nchi sita kwa CCM!!......Tena hapa wanajibu tayari kuwa wewe ni wa DR W.P.SLAA na CHADEMA......Kwa hiyo na wewe unaingia kwenye kapu lao la udini. Hawa jamaa ni washenzi sana na kwa propaganda hii ya UDINI,UKABILA na UKANDA kamwe hawatabaki salama na hii ndiyo itakayowatoa ktk uongozi wa nchi hii nzuri. CCM ni hatari,tuwaondoeni wakafanyie propaganda hizi chafu kuzimu na kmwe tusikubali sisi kupelekwa kuzimu na maCCM.......Hapa askofu subiri na wewe,watasema ni kutoka Kilimanjaro au kaskazini na ni MCHAGA wakati wewe ni from west kwa ZZK na Muha!!..


Aliendelea kusema kuwa hatumchagui mtu au malaika wa kutupeleka Mbinguni bali mtu wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa kwa faida ya wananchi wote. Aliwaasa wanasiasa waache siasa za chumbani za kunyoosheana vidole kuhusu ndoa zao. "Tusiendekeze siasa za chumbani,hatumchagui kiongozi wa kutupeleka mbinguni bali tunamchagua kiongozi wa kutuletea neema hapa hapa Tanzania. Watu leo wanamsifia Mandela kwamba alikuwa kiongozi bora lakini wanasahau kwamba Mandela huyuhuyu maisha yake ya ndoa yalikuwa na kasoro kubwa. Aliweza kuwasamehe makaburu lakini alishindwa kumsamehe mkewe Winnie. Ni nani Kiongozi wa nchi hapa Tanzania anaweza kusema yeye ni msafi?Kwani sisi atujui maisha ya JK? Tuache siasa za chumbani, tuchague kiongozi bora.

  1. Hakuna wasafi askofu!!...Tena wa CCM walio madarakani ni wachafu kupindukia,wezi na wauaji wa kutisha.!!...Watawala kwa damu
  2. Maisha ya JK tunayajua vilivyo tunamuheshimu tu kwa sababu ndiye kiongozi wetu kwa sasa. Tulifanya makosa kumchagua,acha amalize muda wake aondoke zake

Pia Askofu Kakobe alishauri Chama Tawala kikubali uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuondoa malalamiko toka kwa vyama vya upinzani. Pia alishauri siku ya uchaguzi mkuu isiwe Jumapili, Jumamosi au Ijumaa bali serikali itenge siku yoyote katikati ya wiki ili wananchi wengi zaidi waweze kujitokeza kupiga kura.

  1. TUME HURU YA UCHAGUZI ni piga ua na garagaza kabisa,lazima ipatikane before 2015, ongeza na UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA........Wakiendelea kuuvaa ujinga katika katika haya tutawaonesha kuwa hii nchi sio ya kwao bali ni ya wananchi!!
  2. Uchaguzi/kupiga kura iwe siku ingine na si J2,J'mosi au Ijumaa? Yes, naunga mkono hoja kwa 100%.......Natangaza na maslahi binafsi mimi ni MKRISTO huwa tunapata taabu sana siku ya J2 wakristo!!

N.B:Tunaweza kujadili maoni ya huyu mtumishi wa Mungu kwa mustakabali wa Taifa letu.

Bwana akubariki sana ASKOFU ZACHARIA KAKOBE,Fanya kazi ya Mungu kwa kuwakumbusha viongozi wajibu wao na ni lazima wafahamu kuwa MAMLAKA YOTE YA KUWATAWALA BINADAMU inatoka kwa Mungukwa sababu binadamu ni wake yeye Mungu , na wewe ni mtumwa wa MUNGU HUYU MTAKATIFU MWENYE ENZI YOTE!!..Wakidharau tu wamekwisha!
 
Ulimi ni kitu cha kuchunga sana, mwanzoni ameongea vizuri mpaka mimi nilitaka kumpa pongezi, mwishoni na yeye amekifanya hichohicho anachokipinga. Mimi naona ana maono ya chuki, eti tumpe uraisi kwa kwa lipi. Kiongozi ni kioo cha jamii akifanya vibaya lazima asemwe bila kujali ni nani, hatuwezi kuficha maofu kwa kivuli hakuna malaika, kulikuwa na haja ya kusali wakati sisi sio maika.
 
Kakobe ni Mtumishi wa kweli wa Mungu. Wale akina sijui mzee wa.upako na dokta rwakatare hawawezi kuikemea serikali yao. Wao ni funika kombe mwanaharamu apitw
 
Askofu anataka tuongozwe na vipofu, si tutatumbukia shimoni
mtu anayeisaliti ndoa yake bila woga hawezi kuogopa kusaliti taifa.
Askofu anaitaji askofu mwingine ili ampe neno! Kapitiwa!
 
Mtumishi Wa Mungu yuko sahihi.

Hili la kukataza watumishi wa Mungu kutojihusisha Na siasa si sahihi Kwani watumishi Wa Mungu ni raia Na hakuna kifungu chochote cha katiba wala sheria kinachokataza.

Huu ni uoga tu Wa watawala kwa sababu watumishi Wa Mungu wana wafuasi wengi.

Pia hii ni double standard ya CCM Kwani ni CCM hii hii ilimchagua Mtumishi Wa Mungu Mchungaji Getrude Lwakatare kuwa mbunge!
 
Kakobe ni Mtumishi wa kweli wa Mungu. Wale akina sijui mzee wa.upako na dokta rwakatare hawawezi kuikemea serikali yao. Wao ni funika kombe mwanaharamu apite
 
Ulimi ni kitu cha kuchunga sana, mwanzoni ameongea vizuri mpaka mimi nilitaka kumpa pongezi, mwishoni na yeye amekifanya hichohicho anachokipinga. Mimi naona ana maono ya chuki, eti tumpe uraisi kwa kwa lipi. Kiongozi ni kioo cha jamii akifanya vibaya lazima asemwe bila kujali ni nani, hatuwezi kuficha maofu kwa kivuli hakuna malaika, kulikuwa na haja ya kusali wakati sisi sio maika.

Hajapotoka Mkuu Hebu wachambue viongozi wetu Wakuu ndani ya CCM nakuhakikishia Kama kigezo kingehusisha Na uadilifu ndani ya ndoa Hakuna hata mmoja ambae angepita
 
Baba Askofu Kakobe kamaliza yote, kamsema vilivyo Mwigulu Nchemba.
 
Back
Top Bottom