Kakarata ka Pesa katika BSS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakarata ka Pesa katika BSS

Discussion in 'Entertainment' started by IshaLubuva, Sep 14, 2009.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwenye kipindi cha Bongo Star Search kinachorushwa hewani na Runinga ya ITV, jana wale vijana wawili (Msechu na mwenzake anayewakilisha DSM) ambao mmoja wao ndiyo anatarajiwa kvikwa taji la BSS wa 2009 walijikuta wakiwa kwenye Ukanda wa Hatari (Danger Zone). Kwa mujibu wa Majaji wa Kipindi hicho hiyo ilitokana na watazamaji na washabiki wao kutowatumia ujumbe wa simu wa kutosha. Lakini mimi nilipata mashaka kwa kiasi fulani kwa kuzingatia ufanisi ambao umekuwa ukionyeshwa na vijana hawa hasa Msechu ambaye hata wao Majaji wamakiri kila mara kuwa huwa anawashangaza kila wakati anapotakiwa kupanda jukwaani kwani amekuwa na kawaida ya kuweka ubunifu wa hali ya juu katika nyimbo na hivyo kuweka mvuto wa kumtazama na kumsikiliza. Siamini kama hawa vijana hawakupata kura za kutosha bali wameingizwa kwenye ukanda wa hatari kwa malendo ya kibiashara zaidi na ndo maana naona kama wamewafanyia watazamaji kiini macho kama kile kinachofanywa kenye kamari ya kakarata kekundu/ka pesa. Mnasemaje wadau
   
 2. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Saluti mkubwa.....!!!
  Inawezekana kabisa ukawa ni ujanja wa waandaaji.....hivi michezo michafu itakwisha lini....??
  Anyway lets wait and see.... i think there might be some unfair game they want to play....Lets wait.
  2po pamoko......
   
 3. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2009
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  teh teh, unajua hivi vitu ni kama siasa. mwaka 1995 Mr Mrema alikuwa na mashabiki wengi sana,walikuwa tayari hata kusukuma gari lake umbali wowote aliotaka. lakini siku ya kupiga kura wengi hawakupiga kwa sababu kadhaa ikiwemo kutojiandikisha na kauvivu tu. katika hili ni kibiashara zaidi ila nikikuuliza wewe mleta mada umepiga kura mara ngapi kuwatetea hawa watu? vijana wamejipanga wanapiga kura kwa malengo ya kumshindisha ndugu/jamaa yao kama unafikiri unawakubali piga kura nyingi mpaka uishiwe Mama Rita ajipatie Return ya investment yake..
   
 4. M

  Middle JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni wizi mtupu pale,mie jana niliwai kurudi home,uwaga nasimuliwa na jamaa nikawona yule msechu na yle kijana mwengine,hata wao akina majani waliwasifia,then naona mwisho wapo katika hatihati yao wawili watoke,na kuwanusulu ni tutume mgs nyingi,kama siyo kawizi fulani hapo.
  mie situmi na wala sitoangalia tena na BSS tenu
   
 5. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #5
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  Kwani ujui hapa Bongo kila kitu kina kwenda kiwizi wizi? jana walichotuonyesha pale ni kwamba kura zinazo pingwa ni chache hivyo wao wana kusa pato la kutosha,ndio maana amewaweka danger zone Peter na Kelvin wakiamini hawa watu wana wapenzi wengi na wakifanya hivyo watu wengi watapiga kura na kuongeza kipato shao....Jana hawaja onyesha idadi ya kura walizipigia washiriki hii ni ilikuficha ukweli kwani kuna uwezekano Peter Msechu akawa anaongoza kwa kupigiwa kura nyingi..kitu kingine wapepandisha bei ukipiga kura moja unakatwa Tsh.250/= toka tsh. 150/=
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi ndo maana iwa siharibu pesa yangu kutuma viujumbe hivyo mnawanenepesha wajanja endeleeni kuliwa hakuna cha kura wala nn wizi mtupu.
   
 7. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #7
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Unapiga kura unaliwa visent vyako mwisho wasiku wana mchangua mshindi wanao mtaka wao na sio kutokana na kura za wananchi.....
   
 8. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi mbona programs za kitanzania na adverts zinakuwaga hazina mvuto? The singing in bss is poor!! wanaojua kuimba hawaendi kushiriki au ni nini?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yeah wezi tu mkuu ni ujanja wameubuni kuvuna pesa za walalahoi eti kura hazijatosha huu ni wizi mkuu.
   
 10. Amosam

  Amosam Senior Member

  #10
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnakumbuka ya Misoji na Rogers?
   
 11. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #11
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hapo ndipo nilipo choka kabisa kwani Rogers alikuwa mkali kuliko Misoji.
   
 12. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiki Kipindi mimi huwa nakiangalia "by the way" tu lakini kimsingi nilikosa mvuto kwake tangu mwaka ule tu kilipoanza kwa msingi kwamba Majaji wake walikinyima mwelekeo uliostahili kama jina lake lilivyo (Bongo Star Search) badala yake walikielekeza kwenye kutafuta Bongo Singer Seach. Kwa nini nasema hivyo, kwa sababu Washiriki wengi waliyoingia huku wakiwa na ujuzi wa kucheza Gitaa walivunjwa moyo vibaya mno kuwa walikuwa hawajui kuimba na badala yake walibebwa na vyombo walivyokuwa wanavicheza. Kama utakumbuka vema hata huyo Peter Msechu alianza akiwa amaimba pamoja na kucheza Gitaa, lakini wakamponda sana hadi akalazimika kuachana na Gitaa. Lakini kama alivyosema mchangiaji mmoja, ni dhahiri kuwa kura za watazamaji hazina uzito wowote kwani kila Majaji wanapomponda mshiriki ni nadra sana kwake kusalimika. Kwa msingi huo sijawahi na sitarajii kupiga kura.
   
Loading...