Kakangu ana mwanae ambaye anaingia mwaka wa tatu kozi ya Udaktari (MD) kwa chuo ambacho nisingependa kukitaja. Mwanetu huyo pamoja na kuomba mkopo mara ya tatu mfululizo amekuwa akinyimwa. Siku zote amekuwa akilalamikia sana vipngozi wa Bodi ya Mikopo na hapa viongozi wetu hawa. Amekosa upendo nao kabisa. Huyu anatamani aanze upya ili hiyo miaka mitatu iliyobaki asome hata degree ingine tu ambayo haina gharama kama za Udaktari. Hii yote ni kwa sababu akiwa likizo humsaidia mzazi wake ilia apate anagalau karo.
Sidhani kama huyu kijana akija kuwa Daktari kisha Badru au Nyahende au familia zao wakienda kutibiwa na yeye atawapokea vizuri. Huyu kanyimwa mkopo hivi hivi kwa kuwa eti mzazi wake mmoja yupo kazini Serikalini. Huyu ni mmoja tu je wengine walioumizwa huko itakuwaje? Serikali ishsuriwe wadau wote wawekwe sawa kuepuka maslahi binafsi.