Kaka zangu jitahidini kuulinda uanaume wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaka zangu jitahidini kuulinda uanaume wenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Maty, Sep 21, 2010.

 1. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Waume wengi wa siku hizi (sio wote) ndio maana tunawaita wanaume suruali mwanaume kazi kupiga mizinga mara nitumie vocha, au anakuita kukupa ofa halafu anasema mimi nalipia chakula vinywaji unalipa wewe, sasa uliniitia nini kama unaona huna hela. Acheni kujidharaulisha kaka zangu mwanaume mzima utamuombaje mwanamke vocha? nisiwafiche kaka zangu ni bora usimpe mwanamke hela wewe ukumuita mpe ofa ya nguvu kisha mrudishe kwao atakuheshim lakini wewe usiombe hela kwa mwanamke ni dharau kubwa mno hata kama huna kipato kikubwa mwanamke kakuzidi we jikaushe tu anaweza kukupa mwenyewe (NOTE: MWANAUME NI AIBU KUPIGA MZINGA NI MWIKO)
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Naona umeandika out of emotion inawezekana ulikutana na mario huko akawa ana do the nidful kwako. Swali kwako unapoitwa kupewa ofa kwanini uende mikono mitupu bila kutembea na hela mtu anapokuita kukupa ofa unajua ana kaisi gani mfukoni? Je ukiitwa ukaishia kupewa ofa ya soda? Jinsi nyie wanawake mnavyotuomba vocha basi mkae mkijua kuwa na sisi hiyo tabia yenu inatukera kama inavyokukera wewe kuombwa vocha na mwanaume ila i guess tabia hii ya kuomba vocha wanawake ndio mmekubuhu.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii Topic ngoja nikajipumzishe kidogo nikirudi nitakuwa na la kusema ...
  Mabinamu kuna hoja hapa ya kuchangia:confused2:
   
 4. Kidege

  Kidege Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa maisha ya ki-magharibi nikikutoa out haina maana nitalipa expense zote. kila mtu ana-clear alichokula. Na hii ni kwa sababu kila mtu anafanya kazi kwa hy anakipato.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hakuna hoja hapa inaonyesha alizoea kupiga mizinga sasa kaombwa yeye imekuwa ishu namna hii.
   
 6. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Dadangu mambo yanabadilika hivi sasa. Suala la kutoa ofa si la mwanaume tu. Nyie wenyewe kila siku mnalia na 50 kwa 50. Sasa ukiambiwa tu ulipie vinywaji unapiga kelele. Je ukiambiawa ulipie guest na bado jamaa anakutafuna utafanyaje. Unatakiwa ubadilike lipia ofa kwa furaha
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mpwa naona alikutana na mtu aliye do ze nidful kwake vilivyo
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  Yamekukuta nini? pole saana
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha unakuta demu anakuja na nauli tu sasa kama upo mbali ni balaa hapo hapo yupo na wapambe wawili amekuja nao ambao kwa vyovyote vile ni mzigo kwako dah na wewe hapo ulikuwa unapiga hesabu mkisha kunywa uende ukamege sasa kaja na wapambe wawili sijui pesa ya mjengo kama itatosha.
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Pole sana.
  Usawa mnaoulilia siku zote ni pamoja na kulipa bili za namna hiyo. Ukikua utaacha tu, ni vijimambo vya muda.
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha jamaa mmoja alikuwa anamfukuzia demu mmoja siku moja akamuita huyo demu sehemu moja sasa si unajua dada zetu hawa walivyo wakiitwa na wao wanabeba na mashoga zao juu tena sio mmoja wanakuwa wawili au zaidi, sasa jamaa kufika pale yuko na mshikaji wake wakakaa stori zikaendelea mabinti wakaanza kuagiza BLACK LABEL, JACK DANIELS halafu ngoma per tot inauzwa buku tano jamaa kuona hivyo akamwambia mshikaji atangulie nje baada ya jamaa kutangulia nje akawaambia mabinti kuwa anapiga simu mara moja jamaa akala kona nduki unaambiwa wadada ilibidi waache simu zao pale siku ya siku jamaa akakutana na huyo mwanamke, mwanamke akamuuliza jamaa vipi umeacha usanii wako jamaa naye akamuuliza mwanamke vipi na wewe umeacha kutembea na rafiki zako ukiitwa sehemu baada ya hapo ilibidi wawe washikaji tu.
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  eeh....maty!

  hapo kwneye red.....exactly thats the way to go...maadamu siku hizi hakuna kazi zinayobagua mwanamke ( and for that matter salary-wise), in fact kuna wanawake kibao wana earn kuliko wanaume..so hakuna excuse kwanini tusichangie bill,

  Hapo kwenye green, hiyo heshima ya mwanamke kwa mwanaume ambaye anapendw akupewa vocha yeye, kupewa hela ya saluni yeye, mafuta ya gari yeye, kodi ya nyumba yeye apewe, ada ya mtoto wa shangazi yake yeye, ...kama kufanyiwa heshima ndo huko basi huyo heshima bora nisiipate.

  halafu, hivi mnalilia usawa upi hasa ndo ninaposhindwa kuwaelewa

  kama sualani kidude, si twapeana? kama utendaji kazi 'unashuka' kunako 6x6 basi hiyo ni issue nyingine lakini chonde2 msitumie vidude eti kutublackmail manake wengine hatudanganyiki

  (hapa infidelity haihusu wajameni naongelewa 'ideal' situation)

  Mwalimu Gaijin unaweza kusoma ila usichangie tafadhali. Asante
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Ila jamani wanaume wa siku hizi wanapenda sana kutunzwa sio siri. Tuliwahi kukaa Mango garden hapo kinondoni siku moja tukaanza mada hii mwishowe tukaishia kusema tuone wanawake wangapi wanalipa bill? Tulihesabu karibuni meza ishirini hivi tukakuta meza 16 ni wanawake ndo wanalipa bill na ukiangalia mwanaume aliyekaa nae anaonyesha kabisa ni boy/mume wake tukaishia kukubaliana wanaume wa siku hizi wanapenda sana kutunzwa na wanawake hata kama anafanya kazi.
   
 14. c

  cool guy Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bro F hii ya mwisho safi imeniburudisha kabisa na nipo hapa ofisini na wind up ili niingie Gym kidogo nikapige body pump kiasi hivi
   
 15. c

  cool guy Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dena, katika sehem hii ya ulimwengu mimi ninapoishi opposite na uchunguzi wako wa siku hiyo, lakini nakubali haya mambo yapo but for it boils down to communication baina ya wahusika wawili na it could go either way-ni masikilizano2
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kumbuka wanaume tuna mambo mengi makubwa ya kutake care kwahiyo mimi hata mke wangu au girlfriend akilipa bili naona ni poa tu kwani kuna sehemu imeandikwa wajibu wa kulipa bili ni wa mwanaume au ukilipa bili ndio unaonyesha uanaume wako well mmekuwa mkitaka usawa natumaini usawa una apply kwenye mambo kama hayo pia
   
 17. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mimi sijakataa kwamba ni kweli mambo yamebadilika, usubiri nikuite nikupe ofa na nilipie mimi sio unaniita halafu unaanza kunipa mzinga. Na hiyo 50 kwa 50 ni ya kwenye majukwaa tu katika uhusiano hamna mwanaume anabaki kuwa mwanaume tu na lazima abebe majukumu yake
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  cjaelewa unazungumzi uhusiano wa aina gani, hata akiwa mume/mchumba haruhucwi kuomba kama amekwama?
   
 19. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  hatukatai gf au mkeo kulipa bili lakini apende yeye sio mwanaume mzima unaanza kukomalia gf alipe bili wakati wewe ndio umemuita aamue yeye mwenyewe kukusaidia
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,018
  Likes Received: 23,938
  Trophy Points: 280
  Pole sana dada maty.....siku nyingine tafuta vidume kama sisi ambao tunaamini katika infidelity......Tuna rule yetu moja inayosema ni jukumu la infideleta kugharamia zoezi zima la infidelity kwenye first date. Usisahau second date inategemea na kilichotokea kwenye first date........
   
Loading...